DOKEZO Naibu Waziri na Mbunge Pauline Gekul adaiwa kumfanyia Ukatili wa Kimwili Mtoto

DOKEZO Naibu Waziri na Mbunge Pauline Gekul adaiwa kumfanyia Ukatili wa Kimwili Mtoto

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Huu ukatili uliofanywa na Mbunge wa Babati Paulina Gekuli haupaswi kufumbiwa macho hata kidogo, @tanpol wajibu wenu ni upi? Kwanini mnalea udhalilishaji huu mkubwa mpaka sasa waliofanya hivi vitendo wapo uraiani?

View attachment 2823504
Hashimu Ally Phillemon, mkazi wa Babati Mjini, anaeleza kwamba alikamatwa eneo lake la kazi, Paleii Lake View Garden, mali ya mbunge wa Babati Mjini, Pauline Gekul, Naibu waziri sheria na katiba na kupigwa, kujeruhiwa na kuwekewa chupa katika maeneo ya haja kubwa.

Hashimu Ally anasema, Pauline Gekul alitoa bastola, akamueleza achague kukalia chupa mwenyewe au apigwe risasi na mwili wake wakautupe katika Ziwa Babati. Akagoma, wakampiga sana, wakamuingizia chupa sehemu ya haja kubwa. Huu ni unyanyasaji wa hali ya juu sana. Unyama.

Hashimu Ally anasema alituhumiwa na boso wake (Pauline Gekul) kutumwa kuweka sumu ili kumuua Pauline Gekul, tuhuma ambazo hazijathibitishwa popote hata na jeshi la polisi. Akasulubiwa sana kisha kukabidhiwa polisi Babati na kumpiga kila siku asubuhi na jioni, kwa siku nne.

Hashimu Ally alikana tuhuma zote hizo akiwa kituo cha polisi Babati Mjini na hata chini ya mikono ya mateso ya Pauline Gekul. Baada ya kupigwa kwa siku nne mfululizo akiwa polisi Babati, alidhaminiwa na baba yake mzazi. Lakini leo ameitwa ofisi za Manyara ili kutoa maelezo. Tunafuatilia.

Ujambazi huu unafanywa na Pauline Gekul ambaye hadi sasa ni naibu waziri wa Sheria na Katiba. Wizara ambayo inapaswa kuongoza kwa vitendo ulinzi wa haki za binadamu, utawala bora wa sheria. Pauline Gekul umepata wapi uhalali wa kupiga watu kwa tuhuma za kipuuzi?

Serikali ya CCM imechukua majambazi na kuwapa madaraka makubwa namna hii? Ni wizara hii ilisema kwamba watanzania wanatakiwa kupewa elimu ya katiba kwa miaka mitatu? Kimsingi Pauline Gekul hatakiwi kuwa Naibu Waziri wa masuala ya sheria na katiba.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Manyara, tunataka kuona haki ikitendeka. Waliotenda jinai wote kuanzia walinzi wa Pauline Gekul, wafanyakazi wa Paleii Lake View Garden na polisi waliompiga Hashimu wachukuliwe hatua za kisheria. JAMBAZI PAULINE ASHTAKIWE.

Tunauatilia na tutaujulisha umma kila hatua. Hatuwezi kuishi nchi ambayo naibu waziri anaweza kuamua kutunga tuhuma, kutoa adhabu za kikatili na tena kuwakabidhi polisi waendeleze unyanyasaji. Hatuwezi kuruhusu Taifa letu pendwa likawa na MAJAMBAZI ofisi za umma

MMM, Martin Maranja Masese


View: https://m.youtube.com/watch?feature=shared&v=04BSzpoa6xo

Ingekua mbele sahvi mbunge hana ubunge wala unaibu wowote na kesi ipo inafuatiliwa kiundani sio kiCCM.
 
Huyo waziri Bado hajawajibika tuu mpaka muda huu natambua maana Bora ya uwajibikaji sababu tuhuma nzito zimekuja kwake hapa haijalishi kuwa umefanya au hukufanya ila Ili kuheshimu utawala Bora anapaswa kuachia ngazi Ili kupisha uchunguzi.

Aviache vyombo vingine viwe huru kumchunguza
Kitendo cha kutumia polisi kukamata mwandishi habari aliyekuja kumhoji ilipaswa aondolewe katika hicho cheo.
 
Ukiwa Ccm Ni Untouchable Kama Huamini Hili Litaisha Kama La Dkt F Dugange Tu
Wanaoneaga wajinga tu mm mmoja alinipiga na chupa baa nkamshitaki akaniletea ujinga wa kutetewa nliwambia polisi duniani kuna mahakama zingine.nlipiga mke wake nkamtumia picha akapata stroke cha ajabu mke hakuacha .
 
Very serious accusations!

Uchunguzi ufanyike. Haki itendeke pande zote.

-Kaveli-
 
CCM imfukuze ubunge haraka sana Pauline Gekul, huyu ni muuaji, jambazi mkubwa, kisha serikali na haki za binadamu wampeleke mahakamani haraka sana
 
Back
Top Bottom