Naibu Waziri na Waziri Makamba wajiuzulu. Ni kwa kulidanganya Bunge kuwa mgao utaisha Desemba 2022

Naibu Waziri na Waziri Makamba wajiuzulu. Ni kwa kulidanganya Bunge kuwa mgao utaisha Desemba 2022

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2020
Posts
4,170
Reaction score
6,757
Nipo hapa home umeme umekata.

Na hii ni Desembe 3.

Mlisemea Kinyerezi 1 itakuwa imekamilika.

Sasa mbona mmedanganya bunge?

====
Walichokisema November 2, 2022

Serikali imesema makali ya mgao wa umeme nchini yanaweza kupungua mwezi ujao wa Novemba baada ya kukamilika kwa miradi ya umeme ukiwemo wa Kinyerezi I uliopo jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri wa Nishati, Stephen Byabato ameliambia Bunge leo Novemba 2, 2022 jijini Dodoma kuwa mwezi ujao mradi wa Kinyelezi I utakamilika na kuingiza megawati 185 katika gridi ya Taifa.

Amesema megawati hizo zitapunguza makali ya mgawo wa umeme unaendelea hivi sasa katika maeneo mbalimbali nchini ambao umeibua mjadala mpana miongoni mwa Watanzania wakiwemo Wabunge.

Aidha, Serikali ina mpango wa kutenga Sh500 bilioni kwa ajili ya kusaidia ukarabati wa miundombinu chakavu, jambo likalkosaidia kuokoa umeme unaopotea na kuongeza ufanisi wa uzalishaji wa umeme nchini.

Kwa nini mgao wa umeme?

"Tatizo tulilonalo ni upungufu katika vyanzo vya kuzalisha umeme, mheshimiwa Spika, kwa sasa tuna upungufu wa megawati 190 katika vyanzo vya kuzalisha umeme nchini," amesema Byabato.

Byabato ametoa kauli hiyo baada ya Spika wa Bunge Dk Tulia Akson kumtaka kueleza kuhusu kukatika katika kwa umeme nchini, jambo ambalo limekuwa likileta usumbufu mkubwa kwa wananchi wakiwemo wafanyabiashara.

Dk Tulia alimtaka Naibu Waziri huyo kutoa kauli ya Serikali baada ya Mbunge wa Ndanda (CCM), Cecil Mwambe kutaka kujua mkakati wa Serikali kumaliza kero ya kukatika kwa umeme mara kwa mara ikiwemo mikoa ya kusini.

Spika Tulia ameitaka Wizara ya Nishati, kulitazama upya suala la mgawo wa umeme kwa kutoa kipaumbele kwa baadhi ya maeneo ambayo yanahitaji umeme zaidi ikiwemo shughuli za viwanda na huduma muhimu ikiwemo afya.

Amesema hiyo itasaidia kupunguza hasara wanayopata watu hasa wafanyabiashara katika maeneo yao.
 
Taifa la mabwege nani ajiuzulu??!!
Uachie nani asali aseee!
 
Marope anavyopenda wadhifa ajiuzulu [emoji23][emoji23][emoji23] najisaidia pale mfugale.

Hawa mawaziri wapo kupiga michongo yao hivyo hawez sema anajiuzulu kakua haoni uchungu kwa wanavyokwamisha wananchi na watakuja na sababu kem kem kama walivyo mpandikiza majaliwa kwenye ajali ndo maana dogo bungeni alikua amekaa kwa masononeko akijua nn kinaendelea
 
Back
Top Bottom