Naibu Waziri Nditiye aagiza TCRA kukagua mabasi yote yanayosafirisha vifurushi bila kuwa na leseni

Hawana mtandao wa usafirishaji kama wa mabasi. Wanataka kusema wana magari ya kusafirisha vifurushi Dar-mikoani-wilaya zote, Mwz-mikoani-wilaya zote, Kigoma-mikoani-wilaya zote, Mtwara-mikoani - wilaya zote n.k kila siku?. Ukweli network hakuna na bila network hakuna fast mvnt of goods na mzunguko wa pesa unadorola.
 
Na Thadei Ole Mushi.

Naibu Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi Mhandisi Atashasta Nditiye apiga marufuku kutuma kifurushi au barua kwenye magari ya abiria.

Kuna kitu nakisema kila Siku Serikali ianze mchakato wa kushindanisha vijana kwenye kutafuta vyanzo vipya vya mapato.

Yaani waweke dau na atakayefanikiwa kuleta chanzo cha uhakika cha mapato ambacho hakitaleta bughudha kwa wananchi apewe tuzo, atambulike na awe sehemu ya kusimamia chanzo hicho cha mapato (Yaani aajiriwe hapo hapo).

Tukimbizane kufungua fikra na ubunifu wa vijana na wananchi kwa ujumla katika kufikiri na waisaidie Serikali yao katika kutafuta vyanzo vipya vya mapato. Hizi marufuku za kila siku zitaua uchumi wa wananchi wa chini kabisa.

Kuna vijana wanauza vitu vyao kwa kutuma kwenye mabasi. Sasa umeshamkamua elfu ishirini ya kitambulisho cha Ujasiriamali halafu hawezi tena kutuma mzigo Tanga ufike kwa wakati. Kuna biashara zinaenda kufa hapa.

Sisi tulio mikoani tulikuwa tunatuma Samaki kijijini au sukari, mafuta na bidhaa nyingine kwa mama yangu na wazee wetu. Sijui nitatuma Samaki posta sijui watanitumiaje tena ndizi. Tunazidi kuyafanya maisha ya mlalahoi kuwa magumu.

Shirika letu la Posta linatakiwa livutie Wateja na sio kulazimisha watu kuwatumia. Hivi ni maeneo yote yana Ofisi za Posta? Hutumia muda gani kifurushi kufika? Tunarudi nyuma au tunaenda mbele?

Kama shirika haliingizi faida si mnabadilika mnafanya biashara nyingine? Shirika la Posta kwa miaka ya Nyuma lilikuwa linafanya kazi kutokana na mazingira sasa hivi mazingira yaliyopo haliwezi kusurvive kwa kiwango walichokitarajia.

Hapa ndipo Naibu waziri alipoacha kufikiria afanye nini. Rais anataka kodi kweli ila anataka maisha ya mtanzania yaboreke. Kumsaidia Rais angelitakiwa akae chini ajiulize shirika libadilike liweje ili liingize mapato.

Hawa wajamaa wamegoma kufikiria kabisa, tunapaswa kutafiti ni kwa nini Posta yetu wananchi wanaikimbia, nini cha zaidi wanakipata kwenye mabasi yaani ni kwa nn wanakimbilia kwenye mabasi.

Huku jalalani tumepiga marufuku kuongea Kiingereza.

Ole Mushi
0712702602




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waige ata kwa jirani zetu Kenya. Shirika lao la Posta liko vizuri sana.
 
Hii ndo maana nawakataa kabisa Viongozi wenye mawazo ya KIJAMAA!
Watanzania watakapo kuja kugundua kuwa siri ya umasikini wao ni haya mawazo ya kipuuzi ya KIJAMAA watakuwa wamechelewa sana!
UJAMAA ni kulazimisha UJINGA wako ubwebwe kwa gharama za wengi!
 
Sifa za awamu hii
Teuzi na tenguzi'
Maagizo'
Marufuku'
Sifia'
Jifyatue'
Pika data'
 
Ukishaona nchi inaua ushindani na kuleta monopoly Karne hii, ujue nchi hiyo lazima idondoke kiuchumi.
 
Hayo ni mazingira mapya ya usafirishaji vifurushi.

Mazingira hayo yanaleta ushindani kati ya wasafirishaji.

Kwani naibu waziri hafahamu kwamba kuna kusainishana kabla ya kukabidhiana mizigo?

Kama kifurushi kinatoka Dar-es-Salaam asubuhi na kufika salama Songea jioni kwa mtumiwaji , tatizo liko wapi?

Lakini kuna tatizo kama shirika la posta linasafirisha kifurushi kwa siku mbili!!!

Suluhisho si kupiga marufuku bali ni kuacha biashara ieendelee lakini kwa kuhaikikisha kila msafirishaji anapata leseni.

Leseni ya mabasi iongezwe kuipenegele cha kusafrisha vifurushi na mizigo na wasafirishaji wengine mbali ya posta waruhusiwe kusafirisha hata kwa pikipiki.

Naibu waziri asiwe mgumu sana hata kwenye mambo rahisi kuyashughulikia.
 
Hili tamko likiangaliwa kwa mapana na marefu lina mapungufu.
Posta wana mapungufu mengi sanaaa ambayo inpaswa yafanyiwe kazi kabla ya tamko hili.

Haingii akilini....unaagiza bidhaa kutoka china au singapore inafika hapa nchini kwa usalama mkubwa na umakini wa hali ya juu kisha bidhaa hio inakaa miezi ama kupotelea kwenye ofisi za posta zetu kwa sababu za kizembe.

Unafata percel yako posta ukiwa na tracking number wanakwambia mizigo ni mingi sana huko store uje siku nyingine wapate muda wa kuitafuta.

Uzembe wa posta unatukosesha fursa nyingi sana watanzania za kuuza bidhaa zetu nje kama ambavyo wenzetu wachina na mataifa ya nje wanatuuzia sisi.

Posta waache kuwa kizuizi cha maendeleo bali waboreshe huduma zao na wananchi tutaona na kuhamasika kuwatumia.

Hapa nitatoa mfano rahisi wa fursa kwa vijana, lakini tunashindwa kushiriki sababu posta hawana ufanisi.

Hapo chini kuna picha ikionesha pochi ya ngozi nzuri iliyotengenezwa kwa mikono na inauzwa mtandaoni kwa gharama ya Tsh. 42,000/=. Muuzaji yupo china na anaweza kumuuzia mtu yeyote duniani.

Naamini kijana mbunifu wa kitanzania anaweza kutengeneza pochi nzuri zaidi na kuiuza bei chini kidogo ili kupata soko kwa kuweka bidhaa yake mtandaoni. Changamoto inajitokeza kwamba ukishapata mteja nchi za nje akihitaji hio bidhaa yako ni jinsi gani utaitima huko nje????

USHAURI: Posta waachane na magari ya mizigo. Wajiboreshe wao kwanza na kipimo chao cha ubora ni pale huduma zao zitakapokuwa bora kuliko huduma za mabasi ya mizigo.

Miaka ya zamani ilikuwa mbinde sana kutuma pesa kutoka mkoa mmoja hadi mwingine. Pesa za watu zilipotelea posta. Lakini watu wa mabus walisaidia sana utumaji wa pesa ukawa rahisi, haraka na kwa uaminifu, na kadri miaka ilivozidi ikaja huduma ya mpesa, tigo pesa, ttcl pesa na hata sasa utumaji wa pesa umerahisishwa sanaaa.

Shirika la posta wamelala sanaaaa, huu ni muda waamke na wafikiri nje ya box na kuja na creativity na kasi mpya. Wajifunze kwa shirika la posta la China.

TZS 42,458.08 40%OFF | Handmade Vintage Crazy horse Genuine Leather Wallet Men Wallet Leather Men Purse Clutch Bag Male purse Money Clips Money bag
 
Tofauti na barua sitaitumia posta kutuma mzigo wala kifurushi chochote

jana tu nimepokea gunia la mahindi na mchele kilo 50 toka Mbeya kwa basi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anataka turudi kwenye analogue.
Mabasi ni chapchap na yana hakika.



Postal urasimu mwingi na ujinga mwingi.


Basi mabasi yasipakie mizigo. Airia wakisafiri mizigo itangulie kupitia posta.


Tunarudishana kwenye ujima is nn?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…