Hili tamko likiangaliwa kwa mapana na marefu lina mapungufu.
Posta wana mapungufu mengi sanaaa ambayo inpaswa yafanyiwe kazi kabla ya tamko hili.
Haingii akilini....unaagiza bidhaa kutoka china au singapore inafika hapa nchini kwa usalama mkubwa na umakini wa hali ya juu kisha bidhaa hio inakaa miezi ama kupotelea kwenye ofisi za posta zetu kwa sababu za kizembe.
Unafata percel yako posta ukiwa na tracking number wanakwambia mizigo ni mingi sana huko store uje siku nyingine wapate muda wa kuitafuta.
Uzembe wa posta unatukosesha fursa nyingi sana watanzania za kuuza bidhaa zetu nje kama ambavyo wenzetu wachina na mataifa ya nje wanatuuzia sisi.
Posta waache kuwa kizuizi cha maendeleo bali waboreshe huduma zao na wananchi tutaona na kuhamasika kuwatumia.
Hapa nitatoa mfano rahisi wa fursa kwa vijana, lakini tunashindwa kushiriki sababu posta hawana ufanisi.
Hapo chini kuna picha ikionesha pochi ya ngozi nzuri iliyotengenezwa kwa mikono na inauzwa mtandaoni kwa gharama ya Tsh. 42,000/=. Muuzaji yupo china na anaweza kumuuzia mtu yeyote duniani.
Naamini kijana mbunifu wa kitanzania anaweza kutengeneza pochi nzuri zaidi na kuiuza bei chini kidogo ili kupata soko kwa kuweka bidhaa yake mtandaoni. Changamoto inajitokeza kwamba ukishapata mteja nchi za nje akihitaji hio bidhaa yako ni jinsi gani utaitima huko nje????
USHAURI: Posta waachane na magari ya mizigo. Wajiboreshe wao kwanza na kipimo chao cha ubora ni pale huduma zao zitakapokuwa bora kuliko huduma za mabasi ya mizigo.
Miaka ya zamani ilikuwa mbinde sana kutuma pesa kutoka mkoa mmoja hadi mwingine. Pesa za watu zilipotelea posta. Lakini watu wa mabus walisaidia sana utumaji wa pesa ukawa rahisi, haraka na kwa uaminifu, na kadri miaka ilivozidi ikaja huduma ya mpesa, tigo pesa, ttcl pesa na hata sasa utumaji wa pesa umerahisishwa sanaaa.
Shirika la posta wamelala sanaaaa, huu ni muda waamke na wafikiri nje ya box na kuja na creativity na kasi mpya. Wajifunze kwa shirika la posta la China.
TZS 42,458.08 40%OFF | Handmade Vintage Crazy horse Genuine Leather Wallet Men Wallet Leather Men Purse Clutch Bag Male purse Money Clips Money bag
Smarter Shopping, Better Living! Aliexpress.com
s.click.aliexpress.com