Naibu Waziri Nditiye aagiza TCRA kukagua mabasi yote yanayosafirisha vifurushi bila kuwa na leseni

Naibu Waziri Nditiye aagiza TCRA kukagua mabasi yote yanayosafirisha vifurushi bila kuwa na leseni

Kama watu wanapenda mabasi kwa nini Posta na wao wasiyatumie?

Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye, ameitaka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), kuhakikisha wanasimamia na kukagua mabasi yote yanayosafirisha vipeto, bahasha na vifurushi bila ya kuwa na leseni kutoka Mamlaka hiyo na kuwataka wanaofanya hivyo kuacha mara moja.

Nditiye ametoa maagizo hayo leo Jijini Dodoma wakati akifungua mkutano wa 26 wa Baraza la wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania, waliokutana kutathmini na kuweka mipango mipya ya kuimarisha Shirika hilo.

Nditiye amesema licha maagizo yake ya awali, lakini bado mpaka sasa kuna mabasi ya abiria yanasafirisha vipeto bila ya kuwa na leseni na kutaka TCRA kufanya ukaguzi wa kina kuhakikisha wanayabaini mabasi hayo na kuyachukulia hatua Kali za kisheria.

"Nataka nitoe maagizo TCRA mkafanye msako licha ya maagizo niliyotoa lakini bado Kuna mabasi bado yanasafirisha vipeto, bahasha na vifurushi wakafanye msako kuhakikisha mabasi yote yanayosafirisha yanakuwa na leseni, na yafuate taratibu zote za kusafirisha vifurushi hivyo" amesema Naibu Waziri Nditiye.

Amesema lazima Shirika la Posta waendelee kuimarisha huduma zao na kutoa huduma bora kwani Kuna baadhi ya mizigo ni Siri na nyingine ni Mali za Serikali na lazima zisafirishwe na shirika hilo na si vinginevyo na shirika ndilo lenye uwezo wa kusafirisha mizigo vizuri.

Aidha amefurahishwa na utendaji kazi mzuri wa Shirika hilo hali iliyopelekea Shirika hilo kuondolewa miongoni mwa mashirika yaliyo katika hatari kuondolewa huku akiwataka watumishi hao kujiamini na kusema wanapoona wanakwazwa na vitu wasisite kutoa taarifa.

Pia amemtaka Posta Masta Mkuu wa Shirika la Posta kuhakikisha wanafungua ofisi za kubadilisha fedha katika miji yote mikuu na kuweka watu maalumu na kuhakikisha hazifungwi kwa wakati wote.

"Siku si nyingi nilikuwa na dola nikataka kubadilisha nimeenda ofisi zote nikakuta zimefungwa nikashangaa na ofisi za Posta nazo zimefungwa, Sasa nataka mkafungue ofisi kwenye miji yote mikubwa na kuhakikisha hazifungwi" amesema.

Kwa upande wake Posta Masta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Hassan Mwang'ombe, amesema mkutano huo ni wa mwaka na huwakutanisha Mameneja wa Mikoa na watumishi wa makao makuu wanaokutana kujadili utendaji kazi na kupanga mipango mipya ya mwaka ya Shirika hilo, ambapo pia amesema wamejipanga na wameanzisha huduma kwa njia ya Mtandao kuboresha huduma hiyo.

Huku kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Kitolina Kippa amesema licha ya kazi kubwa zinazofanywa na shirika hilo bado kunachangamoto katika kwa baadhi ya Wilaya kutokuwa na ofisi za Posta.

Wakati inaelezwa kuwa Kuna ofisi za Posta 158 lakini Kuna baadhi ya Wilaya zikiwa hazina Ofisi za Posta Kama Wilaya ya Nyang'wale ikiwa ni miongoni mwa Wilaya zisizokuwa na Ofisi za Posta.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna alichozuia...na wala serikali haijazuia biashara ya vipeto inafanywa kwa utaratibu na kwa kupatiwa leseni...sio kienyeji, duniani kote biashara ya kusafirisha vipeto iko regulated na hapa Tanzania TCRA ndie anaehusika....kama Mmiliki wa basi anataka kusafirisha vipeto vyakutumwa awe na leseni ya TCRA kama ilivyo kwa posta na courier companies....huwezi kujinufaisha kwa biashara usiyolipia...that's why yupo LATRA EWURA nk..."utaratibu ni hekima"
Anataka turudi kwenye analogue.
Mabasi ni chapchap na yana hakika.



Postal urasimu mwingi na ujinga mwingi.


Basi mabasi yasipakie mizigo. Airia wakisafiri mizigo itangulie kupitia posta.


Tunarudishana kwenye ujima is nn?

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani Bahasha yangu niitume posta ichukue 5 days kufika wakati Kimbinyiko wanaifikisha within 10 hours? Posta waachwe wapambane na sisi raia tuachwe tuchague kilicho bora kwetu
 
Hakuna sekta inayoajiri mabongolala, wadumavu wa akili, mapunguani, sukuma liende, nk kama sekta ya umma! Mimi pia ni miongoni mwao, Ameen!
 
Hii habari ya serikali kulazimisha biashara, kufunga biashara na kuchagua mshindi, ni moja kati ya sababu zinazotufanya tuwe masikini.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hawa naona kama wamekuja kuharibia mipango ya watu.....
Wao posta Miaka nenda rudi wameshindwa kutoa huduma hii ya kuweza kumfikishia mtu mzigo wake hapo alipo kitu ambacho Wenye mabasi wameweza

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawa naona kama wamekuja kuharibia mipango ya watu.....
Wao posta Miaka nenda rudi wameshindwa kutoa huduma hii ya kuweza kumfikishia mtu mzigo wake hapo alipo kitu ambacho Wenye mabasi wameweza

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
Serikali inaua ubunifu na mashindano ya kibiashara.

Halafu tunashangaa kwa nini hatuendelei.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna jema litakalofanywa na viongozi likaonekana na tija.

By the way tuliachwa holela sana, now tunatakiwa kufuata njia tunasema NO!, but mwenye haki na usafirishaji vifurushi nchini ni posta na kampuni zilizosajiliwa.
Sidhani kama unatafakari sawasawa,hawa posta wamejipangaje?Yani mtu yuko mrimba huko ambako posta hakuna,mtu akitaka kutuma kibahasha chake apande basi aje ifakara kuifuata posta?
Hiii nchi tunaviongozi wa ajabu sana!
 
Back
Top Bottom