Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Mwanachama huyo alidai Wananchi wanapata wakati mgumu ikiwemo hasara katika biashara zao wakati upande wa pili, Kitunda Center wao hawana shida ya umeme na kwamba wakipiga Simu wanaambiwa “Umeme utarejea katika hali ya kawaida baada ya muda.”
Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga amejibu kwa kusema: Nimpe pole Mdau na Wananchi wa Kitunda kwa changamoto hiyo.
“Kukatika kwa umeme kitunda kunatokana na hitilafu zinazojitokeza katika miundombinu lakini pia laini ya umeme inayolisha Kitunda imetembea na laini nyingine 2 kwenye nguzo moja, hivyo kunapotokea hitilafu kwenye laini moja inaathiri laini zote 3.”
“Kwa sasa tunajenga line kutokea kituo kidogo cha kupoza umeme cha Gongolamboto ili kuweza kutenganisha line hizi 3, Laini hii inatarajiwa kuwashwa hivi karibuni hivyo itasaidia sana kupunguza tatizo.”
Kusoma hoja ya Mdau, bofya hapa ~ Mtaa wa Kitunda - Machimbo tuna kero ya umeme, unakatika zaidi ya mara tatu kwa siku, TANESCO hawatupi majibu ya kueleweka