Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deus Sangu amezitaka Mamlaka za Serikali za Mitaa kuandaa kanzidata za wanafunzi waliohitimu Vyuo Vikuu waliotoka Kaya za walengwa wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) ambao ni wanufaika na mikopo ya elimu ya juu kwa asilimia 100 katika vyuo mbalimbali hapa nchini.
Simbachawene amesema lengo la serikali la kuandaa kanzidata hiyo ni kutaka kuwa na takwimu sahihi na kuendelea kufuatilia maendeleo yao ya kujikwamua kutoka kwenye lindi la umaskini.
Hivi karibuni TASAF na Bodi ya Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) iliingia makubaliano ya ushirikiano (MoU) na kuweza kuunganisha kanzidata zake ili kuwezesha waombaji wa mikopo ya elimu ya juu kutoka kaya za walengwa kutambulika kirahisi na kuwa wanufaika wa Mikopo hiyo ya elimu ya juu kwa asilimia 100 ambapo jumla ya wanafunzi 11,524 kutoka Kaya maskini zilizotambuliwa na TASAF wamenufaika na mikopo hiyo kwa asilimia 100m kwa mujibu wa takwimu.
“Idadi hiyo ya wanafunzi waliopata mkopo huo ni kuanzia mwaka wa fedha 2019/2020 hadi 2024/2025, kitendo ambacho kimepelekea watoto hao kutimiza ndoto zao za kujiendeleza kielimu ikizingatiwa kuwa ni wa kutoka katika kaya maskini.” Amesema Waziri Sangu.
Serikali kupitia HESLB imeweza kutambua na kuendeleza rasilimali watu kutoka Kaya maskini katika maeneo mbalimbali hapa nchini, hivyo ni jukumu la Mamlaka za Serikali za Mitaa kujua maendeleo yao pindi wanapohitimu.
Mmoja wa wanufaika wa mradi huo, ambaye ni mhitimu wa Chuo Kikuu cha Mbeya (MUC) Obeid Mwasaga amesema alianza kunuafaika na TASAF akiwa darasa la kwanza lakini baada ya kudahiliwa na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) hakuwa na taarifa kuwa kupitia TASAF anaweza kupata mkopo, hivyo alilazimika kuacha chuo akiwa mwaka wa pili kwa kushindwa kulipa ada na baadae alijiunga na MUC baada ya kuandikiwa barua na TASAF.
Waziri Sangu ametembelea na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kupitia Mradi wa TASAF katika Kata ya Iziwa na Kata ya Tembele zilizopo Halmashauri ya Jiji la Mbeya na kuzungumza na wananchi na walengwa wa mradi huo.