Naibu Waziri TAMISEMI Dkt. Festo Dugange: Utoaji wa Taarifa kwa Wananchi Uwe Endelevu

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
UTOAJI WA TAARIFA KWA WANANCHI UWE ENDELEVU - Dkt. Dugange

Naibu Waziri TAMISEMI Dkt. Festo Dugange: Utoaji wa Taarifa kwa Wananchi Uwe Endelevu

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Festo Dugange amewataka Wakuu wa Mikoa na Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhakikisha utoaji wa taarifa za utekelezaji wa miradi kwa wananchi unakuwa endelevu na si kusubiri kampeni au tukio maalum.

Dkt. Dugange ametoa wito huo leo Novemba 1,2023 wakati akizindua Kampeni ya Tumewasikia, iliyoandaliwa na Idara ya Habari Maelezo.
‘Wizara inawasisitiza Wakuu wa Mikoa na Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhakikisha utoaji wa taarifa za utekelezaji wa miradi ya maendeleo unakuwa endelevu,’ amesisitiza Dkt. Dugange

Amesema Serikali inataka kuona Wakuu wa Mikoa, Wakurugenzi, Wakuu wa Idara na wataalam wote wa Serikali wanatoa taarifa kwa wakati ili wananchi wajue hatua zilizochukuliwa na Serikali kuwaboreshea huduma.

Ili kuhakikisha wananchi wanapata taarifa,Dkt. Dugange amewataka watendaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kutoa ushirikiano kwa msemaji Mkuu wa Serikali kila atakapohitaji taarifa za kuuhabarisha umma.

Dkt. Dugange amewataka viongozi hao kuwashirikisha katika matukio na kuwapa ushirikiano maafisa habari waliopo katika maeneo yao ili waweze kutekeleza jukumu la kuuhabarisha umma kwa ufanisi.

Ili kuboresha utendaji kazi, Dkt. Dugange amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri ambao hawana maafisa habari kuhakikisha wanaaajiri maafisa hao kwa mikataba wakati wanasubiri Serikali ikamilishe taratibu za kuwaajiri.
 

Attachments

  • F93eoCcXsAA_qb2.jpg
    208.5 KB · Views: 4
  • F93eoCfWQAAsUnP.jpg
    261.2 KB · Views: 4
  • F93eoCcXsAEgRs_.jpg
    202.9 KB · Views: 6
  • F93eptVXsAADERf.jpg
    227.2 KB · Views: 3
  • F93eptaWsAAzkvL.jpg
    222.7 KB · Views: 2
  • F93eptXWYAAwZ6u.jpg
    287.1 KB · Views: 3
  • F93eptXWMAATR6G.jpg
    195.7 KB · Views: 4
Lile V8 alishakitoa gereji?


Atoe hiyo taarifa ndipo wakuu wa mikoa nao watoe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…