BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Naibu Waziri Exauds Kigahe amewataka Wahitimu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kutumia elimu waliyoipata kujiajiri ikiwemo kuanzisha biashara badala ya kuwa sehemu ya kulalamikia ukosefu wa ajira.
Amesema “Ni jukumu la kila mhitimu kuukubali na kuuchangamkia zaidi msukumo wa Sayansi na Teknologia kuliko misukumo mingine iliyozagaa kwenye mitandao ya kijamii".
Kwa mujibu wa taarifa ya Sekretarieti ya Ajira ya Desemba 17, 2018, maombi ya Ajira Serikalini kati ya Novemba 2015 na Desemba 2018 yalikuwa 594,300, lakini waliopata kazi ni watu 6,554.
======================
Wahitimu wa kada mbalimbali wametakiwa kutumia elimu waliyoipata kujiajiri ikiwemo kuanzisha biashara badala ya kuwa sehemu ya kulalamikia ukosefu wa ajira.
Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Exauds Kigahe amesema badala ya kulalamikia ajira wahitimu hao wakawe suluhisho la ukosefu wa ajira kwa kuwa wabunifu na kuajiri Watanzania wengine.
Akizungumza leo Jumamosi Novemba 26, 2022 katika mahafali ya 57 ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) na ya 15 kwa Kampasi ya Mwanza, Naibu Waziri huyo amewataka pia wahitimu kuchangamkia msukumo wa sayansi na teknolojia ili kuleta maendeleo yao binafsi na ya nchi.
“Ni jukumu la kila mhitimu kuukubali na kuuchangamkia zaidi msukumo wa sayansi na teknologia kuliko misukumo mingine iliyozagaa kwenye mitandao ya kijamii.
“Ikumbukwe maendeleo hayaji kwa lele mama, bali kwa mchakato unaohitaji kujitoa, kujinyima kwa faida ya kesho na kila mmoja anafaa akumbuke methali isemayo ‘mchumia juani, hulia kivulini,” amesema Kigahe.
Amepongeza uongozi wa CBE kampasi ya Mwanza kwa usimamizi mzuri wa mapato ya ndani, akisema yamewezesha kuwaendeleza watumishi kielimu, kuboresha miundo mbinu ya ufundishaji, kuanzisha program mpya za chuo, kuandaa mitaala atamizi za biashara na kuanzisha mafunzo ya uanagenzi.
MWANANCHI
RECAP:
Rais Samia Suluhu Hassan, alipozungumza na vijana jijini Mwanza Juni 15, 2021, aliweka wazi kuwapo upungufu mkubwa wa vijana walioko kwenye ajira, ilhali uwezekano wa kuongezeka bado uko gizani.
Kwa mujibu wa Rais Samia, hadi sasa Tanzania kuna jumla ya vijana milioni 20.7 wenye umri kati ya miaka 15 na 35, lakini ndani ya kundi hilo, asilimia 11.4 ya wenye sifa za kuajiriwa, hawako kazini.