Naibu Waziri wa Afya Faustine Ndugulile aelezea aina za Barakoa za kuvaa na Utaratibu wa kutengeneza ya kitambaa

Naibu Waziri wa Afya Faustine Ndugulile aelezea aina za Barakoa za kuvaa na Utaratibu wa kutengeneza ya kitambaa

Huu ni upingaji wa kipumbavu sasa ,lengo la barakoa ni kukukinga usirushe matone ya mate au chafya kwa mtu wa jirani yako unapoongea, pia itakinga mikono yako kukugusa midomo na pua.

Makonda yupo sahihi.



Sent using Jamii Forums mobile app
Nadhani tungeruhusu wataalamu wa afya,

what if matone yakadondokea kwenye barakoa na vitundu vyake vinapitisha kirusi?
inakuwa imekusaidia nini?
 
  • Thanks
Reactions: amu
Kuna haja kubwa sana kwa Masuala ya Afya kuzungumzwa na wataalam wa Sekta hiyo tu na si vinginevyo , mtu aliyesomea Kahawa na vitunguu hawezi kuyajua mambo haya .
Bashite kwanini anaachwa apoteze raia na elimu yake ya fafafafafafafafa div zero? Yaani anatamka kabisa watu wafunge vitambaa vya jasho kufunika pua na mdomo kujikinga na corona?? Jackma kagawa barakoa bure,matajiri wamechangia bil 6 kwanini wasinunue "santaiza na max" na kuwapa wananchi bure?
 
Ngoja tuone hizi

Ova
IMG-20200419-WA0015.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acheni kupotosha watu, barakoa za vitambaa bado zina msaada, hata nchini ujerumani watu wameambiwa wanaweza kuzitumia, ukifuata kiki za hao wanasiasa utapotea. Kwa akili ya kawaida ni asilimia ngapi ya watu wanamudu kutumia N95 ukizingatia kwamba matumizi yake ni ndani ya siku moja. Wanasiasa wanaoleta utaalamu uchwara kwenye swala serious la korona ni bora rais angeanza nao mapema kabla hawajasababisha majanga zaidi...
 
Kuna haja kubwa sana kwa Masuala ya Afya kuzungumzwa na wataalam wa Sekta hiyo tu na si vinginevyo , mtu aliyesomea Kahawa na vitunguu hawezi kuyajua mambo haya .
Heri nusu shari kuliko shari kamili.

Hizo mask za kuzuia virusi vya Corona zinapatikana wapi?
 
Hapa anahitajika mganga mkuu wa serikali kutoa msimamo wa kitaifa juu ya Barakoa tunazopaswa kutumia na namna ya matumizi yake.

Tumeshalisikia agizo la RC Makonda kwamba tuvae barakoa hata za Leso na vitambaa vingine na tumemsikia pi Naibu waziri wa afya Daktari Ndugulili kwamba kitambaa hakizuii virusi wala bakteria kumdhuru mtu. Wote tunawashimu na mawazo yao pia.

Ndiposa namuomba mganga mkuu wa serikali atoe ufafanuzi wa kitaifa utakaojikita kwenye sayansi na uchumi.

Naomba kuwasilisha.

Maendeleo hayana vyama!
 
Back
Top Bottom