Naibu Waziri wa Ardhi abaini Hati 420 za Ardhi hazijachukuliwa na Wamiliki Kilimanjaro

Naibu Waziri wa Ardhi abaini Hati 420 za Ardhi hazijachukuliwa na Wamiliki Kilimanjaro

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Siku chache tangu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. #AngelineMabula abaini Wamiliki 65 hawajajitokeza kuchukua Hati zao Wilayani #Makete, Njombe, Naibu Waziri wake #GeophreyPinda amekutana na hali hiyo mkoani Kilimanjaro.

Pinda amebaini hali hiyo baada ya kufanya ziara katika Ofisi ya Msajili wa Hati Msaidizi wa mkoa ambapo alikuta Ofisi imeandaa #Hatimiliki ambazo Wamiliki hawajazichukua na hivyo kuagiza Uongozi kutumia Vituo vya Redio kuwajulisha Wahusika.

Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya JamiiForums kuendesha Mjadala kuhusu Mchakato wa Umiliki wa Ardhi ambapo Wananchi wengi walilalamikia Urasimu, Vitendo vya #Rushwa na Kutojulikana kwa Taratibu za Kufuata ili Kupata Hatimiliki za Ardhi Nchini.
 
Usanii.com. Hilo nalo la kubaini Waziri? Si ndo michezo yao hiyo watu wa land nchi nzima!
 
Back
Top Bottom