Sio kila mtoto wa mkubwa, but watoto wa mawaziri karibu wote wa Nyerere walisoma hapo,
Primary yangu ni O/Bay tulikuwa na
Watoto wa Malecela akiwa VP II na PM mmoja darasa moja.
Watoto wa Kawawa,
Watoto wa Warioba
Watoto wa mawaziri karibu wote
Watoto wa waserikali karibu wote wakiwemo Watoto wa Jaji Mkuu, Nyalali mkewe ni mwalimu wetu, na Watoto wa Prof. Sarungi, Isaac Sepetu, na wakubwa serikalini enzi hizo.
Huyu Dr. Mwinyi alinitangulia madasa mawili Primary.
Mimi mwenyewe baba na mama walikuwa serikalini.
Sekondari nikaenda Tambaza huko nikasoma na mtoto mmoja wa kwa Nyerere pale Msasani, na mtoto wa Mkapa darasa moja, A level kulikuwa na Mtoto wa Malecela akipiga PCM, akaja binti Malecela form V akipiga PCB, darasa moja na Husein Mwinyi.
A Level nikaenda Ilboru, darasa moja na mtoto wa Warioba.
UDSM sheria nikakutana na Riz1.
Mtoto wa Mkapa alihamia US, hivyo nilipokwenda US, akaniconnect na Mshure wake.
One good thing about me na watoto wa wakubwa, nawaona ni watu wa kawaida sana, sijipendekezi kwao kutaka favours zozote kwa wazazi wao.
Nime interact na Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete, Magufuli na Samia by virtue of my journalistic professional na sio kwasababu nimesoma na watoto wao na sijawahi ku lobby uteuzi kwa yeyote!.
P.