Naibu Waziri wa Maliasili asema kuleni nyama ya Mamba, ni tamu kinoma

Naibu Waziri wa Maliasili asema kuleni nyama ya Mamba, ni tamu kinoma

Analogia Malenga

Platinum Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,292
Reaction score
10,842
“Mamba ana nyama tamu sana, anzeni kula nyama yake badala ya kutegemea kitoweo cha samaki pekee” amesema Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu

Amesema kuwa licha ya nyama hiyo kuwa tamu, lakini kwanza mvunaji wa mamba aombe kibali kutoka kwa maofisa wanyamapori cha kuwavuna kinachotolewa kila Julai Mosi.

“Kuacha nyama yake kuwa tamu, lakini pia ngozi yake ni biashara yenye tija ndani na nje ya nchi,” amesema. Aidha, Kanyasu ameeleza kuwa Serikali ina mpango wa kufungua mabucha yatakayouza nyama za wanyamapori katika maeneo mbalimbali nchini.

“Wizara imeanzisha utaratibu wa uwindaji wa ndani (resident hunting) ambapo nyama zitakazo kuwa zikipatikana zitakuwa zikiuzwa kwenye mabucha hayo,” amesema.

Amesema hiyo itasaidia wananchi kupata nyama za pori kwa urahisi pale wanapokuwa na uhitaji. “Hivyo wawindaji watatakiwa kufuata taratibu za kuomba vibali kwa ajili ya kuwinda ambavyo vitaainisha aina ya wanyama ambao watakwenda kuwawinda.”

Chanzo: HabariLeo
 
Kwanini hayo mabucha hayafunguliwi sasaaa.?
Kila siku stori ni hizi hizi.
Ila mzingatie Halal
 
Utamaduni wetu watu weusi mara nyingi ni kutokula wanyama walao nyama, but huko asia mashariki nawatizama sana kupitia wale vijana youtube"primitive technology" wanakula sana mamba, nyoka, hata kenge poa tu.

Wanawabanika vyema mpaka mate yanajaa mdomoni.
Wale madogo wa primitive technology wameshindikana. Walinchosha walivyopika supu ya nyoka wakailost na spices hahahahah
 
Hii.issue.ya mabucha imekuwa hadithi....kuna kazi kupitisha sheria hizo za uwindaji na kutoa vibali watu waanze.kufanya biashara..kuna mambo mengine yanakera sana sijui wizara inafanya kazi gani kama issue ndogo kama.hizi ambazo rais alishatoa go ahead wanashindwa kuimplement
 
Badala ya wananchi kupata kitoweo safi cha choroa, swala, kiboko na wanyama wengine kama hao, wanaambiwa wale mamba. Kile kinacholika kinakatazwa. Kile kisicholika kinataka kuhalalishwa. Si sawa.
 
Atuoneshe mfano kwanza yeye akiwa anakula

Ova
 
Leo waziri husika nimemsikia redioni asubuhi...... akikisisitiza wananchi waombe leseni ya uvunaji wa Mamba kwa ajili ya kitoweo....

Amesisitiza nyama yake ni tamu mno.
 
Ni kweli nyama ya mamba ni tamu sana, afu ni nyama nyeupe na kwa mara ya kwanza niliila Uganda na congo na nilipata supu na hadi ya kuchoma ni nzuri mno hasa upate na ugali wa muhogo
 
Back
Top Bottom