Naibu Waziri wa Maliasili asema kuleni nyama ya Mamba, ni tamu kinoma

Naibu Waziri wa Maliasili asema kuleni nyama ya Mamba, ni tamu kinoma

Wawauzie Wazungu wakawafuge. Ukinunua nyama ya mamba na kuiweka kwenye friji kibongobongo utaambulia kukimbiwa na mke
 
Nasikia pia ni nzuri sana kwa wanaume 🤣 🤣🤭
 
Uchumi wa kati nazani unaenda vizuri sana nategemea kuingizwa nyama ya mamba uchumi tutaupeleka uchumi wa kwanza
 
Amesema kuwa licha ya nyama hiyo kuwa tamu, lakini kwanza mvunaji wa mamba aombe kibali kutoka kwa maofisa wanyamapori cha kuwavuna kinachotolewa kila Julai Mosi.

“Kuacha nyama yake kuwa tamu, lakini pia ngozi yake ni biashara yenye tija ndani na nje ya nchi,” amesema. Aidha, Kanyasu ameeleza kuwa Serikali ina mpango wa kufungua mabucha yatakayouza nyama za wanyamapori katika maeneo mbalimbali nchini.

“Wizara imeanzisha utaratibu wa uwindaji wa ndani (resident hunting) ambapo nyama zitakazo kuwa zikipatikana zitakuwa zikiuzwa kwenye mabucha hayo,” amesema.


Naona kila dalili za kotokomeza wanyama pori, nashauri angenyamaza kimya, ila amwachie waziri wa vitoweo ahamasishe ufugaji ambao unaimarisha biashara kuliko kuvuna viumbe ambao ongezeko na punguzo lao ni la kiasili sana
 
Nyama ya mamba unataka na pilipili nyingi tamu sana.
 
Utamaduni wetu watu weusi mara nyingi ni kutokula wanyama walao nyama, but huko asia mashariki nawatizama sana kupitia wale vijana youtube"primitive technology" wanakula sana mamba, nyoka, hata kenge poa tu.

Wanawabanika vyema mpaka mate yanajaa mdomoni.
Unafahamu kuwa hata kuku na samaki hula nyama?
 
Tatizo ni hadi umkamate huyo mamba
 
Hapo kwenye kufungua mabucha pamenikosha.
 
Back
Top Bottom