Naibu Waziri: Wananchi wapunguze matumizi ya sukari, kwanza sio nzuri kiafya

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amekutanisha wizara ya Viwanda na Biashara na wadau wa sukari nchini kuangalia uwezekano wa kushusha bei bidhaa hiyo kuelekea mfungo wa mwezi wa Ramadhani.

Mfungo huo unatarajiwa kuanza takriban siku tisa zijazo. Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Stella Manyanya wakati akizungumzia kupanda kwa bei ya sukari kunakosaidiwa kusababishwa na upungufu wake sokoni. Aidha alisema kuwa kutokana na kupanda kwa bei ya sukari, amewataka wananchi kutumia asali kama mbadala.

“Wananchi wapunguze matumizi ya sukari, kwanza hata kiafya sio nzuri sana, kama mtu asali haimdhuru basi ni bora akatumia asali,” alisema Manyanya.

Asali kwa sasa inauzwa kati ya Sh 12,000 hadi 15,000. Akielezea sababu za zaidi alisema kutokana na mlipuko wa virusi vya corona, nchi nyingi zimesimamisha uzalishaji na pia mvua nyingi katika baadhi ya maeneo imesababisha uzalishaji kuwa mdogo.

“Mvua nyingi zinasababisha changamoto katika uzalishaji wa sukari, ile miwa ikiwa na maji mengi uzito wa sukari unapungua,” alieleza Naibu Waziri.

Hata hivyo, gazeti hili limebaini katika sehemu kubwa ya Jiji la Dar es Salaam na baadhi ya mikoa wafanyabiashara wanaficha sukari na kuuza kwa kificho kwa bei juu ambapo wananchi wanalazimika kutoboka mifuko yao na kununua bidhaa hiyo kati ya Sh 3,000 hadi 4,000 kwa tofauti ya kati ya Sh 800 hadi 1,800 ya bei elekezi.

Upandaji huo wa sukari umeelezwa na wafanyabiashara wa rejareja kuwa unatokana na wao kupandishiwa kwa sasa mfuko wa kilo 50 .

Mfanyabiashara wa rejareja, White Tarimo akizungumza na gazeti hili, alisema, “Kwa sasa hata sisi tunapandishiwa wiki iliyopita mfuko wa kilo 50, tuliuziwa kati ya shilingi 136,000 mpaka na 140,000 maduka ya jumla na sisi tukauza rejareja kati ya shilingi 3,000 hadi 3,600.

Chanzo: HabariLeo
hivi huyu bei ya asali anaijua au anajitamkia tu?
 
Huyo alishazoea, maana hata kwenye bei ya mbaazi kushuka alitoa shombo hiyo kuwa mbaazi ni nzuri kiafya hivyo wananchi wamepata fursa mara ya baada ya bei kushuka.
Hata kujiita Engineer naona aibu

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwenye Ile TUME ya Mwakyembe kumuondoa EDO, huyu Stella, alikuwa vema sana.

Siku hizi sijui anakula mbaazi za wapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ANASEMA TUTUMIE SUKARI KIASI MAANA SIO NZURI KIAFYA ANASEMA HAYA BAADA YA SUKARI KUWA ADIMU
Na viwanda walivyokuwa wanazindua kila uchao vimeishia wapi? Pwani kilizinduliwa ,Babati kilizinduliwa,Morogoro ,kiwanda cha magereza mbigili kilizinduliwa.
 
Yaani "raia mnyonge" anayestruggle kununua kilo moja ya sukari kwa Tshs. 4000 harafu aweze kununua mbadala wake kwa Tshs 12,000 mpaka Tshs. 15,000!? Huyu Stella vipi? Hesabu za wapi hizi?
 
Hiyo ndio kauli ya Waziri baada ya tatizo kutokea! Mbona hakusema kabla?

Shida wengi wakurupukaji! Walishaharibu toka mwanzo walipojaribu maamuzi yao ya protectionism za sukari inayozalishwa ndani huku uwezo wa viwanda vyetu mdogo kukidhi mahitaji!

Waache kuungilia soko huria.
Huyu dada sidhani kama yupo sawa sawa, alishawahi kutuambia wakulima wa MBAAZI tule wenyewe kama hamna bei ya kuridhisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ANASEMA TUTUMIE SUKARI KIASI MAANA SIO NZURI KIAFYA ANASEMA HAYA BAADA YA SUKARI KUWA ADIMU
Hvi huyu naibu waziri kasema hayo akiwa amelewa, anatania au akimaanisha?

Mada ni kutatua kero na upungufu wa sukari uliopo nchini, iweje aingize wazo hilo leo, kwanini hayo asishauri kabla?

Anatamka kwa maneno yake kabisa kuwa kilo1 ya asali ni kati ya elf15, kuendelea!

Sasa hiyo bidhaa kila raia ana uwezo wa kuipata hata kwa vibaba kama sukari?

Na ni madhara gani ya kimsingi kitaalamu yatokanayo na matumizi ya sukari?

Kama sukari ina madhara kama anavyoshadadia, kwanini isipigwe marufuku kunusuru afya za walaji?

Hawa viongozi wabinafsi wa namna hii ni Mungu ndiye anayetuonesha kwa kuwaumbua uozo uliojificha nafsini mwao.

Na bahati kauli yenye ukakasi kama hii, kaitoa muda muafaka ambao sisi raia tuwanapima viongozi kama wanafaa kurudi kwenye nyadhifa zao kwa njia ya sanduku la kura.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amekutanisha wizara ya Viwanda na Biashara na wadau wa sukari nchini kuangalia uwezekano wa kushusha bei bidhaa hiyo kuelekea mfungo wa mwezi wa Ramadhani.

Mfungo huo unatarajiwa kuanza takriban siku tisa zijazo. Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Stella Manyanya wakati akizungumzia kupanda kwa bei ya sukari kunakosaidiwa kusababishwa na upungufu wake sokoni. Aidha alisema kuwa kutokana na kupanda kwa bei ya sukari, amewataka wananchi kutumia asali kama mbadala.

“Wananchi wapunguze matumizi ya sukari, kwanza hata kiafya sio nzuri sana, kama mtu asali haimdhuru basi ni bora akatumia asali,” alisema Manyanya.

Asali kwa sasa inauzwa kati ya Sh 12,000 hadi 15,000. Akielezea sababu za zaidi alisema kutokana na mlipuko wa virusi vya corona, nchi nyingi zimesimamisha uzalishaji na pia mvua nyingi katika baadhi ya maeneo imesababisha uzalishaji kuwa mdogo.

“Mvua nyingi zinasababisha changamoto katika uzalishaji wa sukari, ile miwa ikiwa na maji mengi uzito wa sukari unapungua,” alieleza Naibu Waziri.

Hata hivyo, gazeti hili limebaini katika sehemu kubwa ya Jiji la Dar es Salaam na baadhi ya mikoa wafanyabiashara wanaficha sukari na kuuza kwa kificho kwa bei juu ambapo wananchi wanalazimika kutoboka mifuko yao na kununua bidhaa hiyo kati ya Sh 3,000 hadi 4,000 kwa tofauti ya kati ya Sh 800 hadi 1,800 ya bei elekezi.

Upandaji huo wa sukari umeelezwa na wafanyabiashara wa rejareja kuwa unatokana na wao kupandishiwa kwa sasa mfuko wa kilo 50 .

Mfanyabiashara wa rejareja, White Tarimo akizungumza na gazeti hili, alisema, “Kwa sasa hata sisi tunapandishiwa wiki iliyopita mfuko wa kilo 50, tuliuziwa kati ya shilingi 136,000 mpaka na 140,000 maduka ya jumla na sisi tukauza rejareja kati ya shilingi 3,000 hadi 3,600.

Chanzo: HabariLeo
Huyu Waziri wa viwanda au waziri wa Afya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom