Naibu Waziri: Wananchi wapunguze matumizi ya sukari, kwanza sio nzuri kiafya

Anaitwa Eng. Stella Manyanya ni Naibu Waziri wa kilimo, biashara na uwekezaji, anasema kama HUMUDU bei ya sukari tumia ASALI kwanza sukari sio nzuri kwa AFYA.

Haa ukiamua kunywa chai kwa muwa au pipi fresh tu yaaani.

My life is mine to remember
 
Anaitwa Eng. Stella Manyanya ni Naibu Waziri wa kilimo, biashara na uwekezaji, anasema kama HUMUDU bei ya sukari tumia ASALI kwanza sukari sio nzuri kwa AFYA.

Haa ukiamua kunywa chai kwa muwa au pipi fresh tu yaaani.

My life is mine to remember
 
Asali yenyewe iko wapi? gram300 tu inauzwa elf 3000 maana yake Lita ni kama elfu kumi halafu hiyo kauli inaweza pandisha zaidi asali zaidi.
 
Labda itokee gharika kuu kizazi chote kiwe ardhini lakini kama kauli ni hizi tunasafari ndefu sana
 

Attachments

  • 1l-PAgS2oWD9LZbW.mp4
    319.1 KB
Huyo mama nae mpumbavu tu,mbona yeye hapandi pikipiki kupunguza gharama ya matumizi ya mafuta kwa vx v8

Sent using Jamii Forums mobile app
 
BONGOland REVOLUTION bado sana,mnataka kauli gani zaid ili mdai viongozi bora??

When your toddler was learning to walk, you’d encourage her to get back up after she fell down,Parents should practice that approach as their children get older.
 
WALALAHOI ASALI KWAO NI ANASA.



Mwaka 1879 Malkia aliyekuwa anaiongoza Ufaransa Bi Marie Antoniette aliambiwa wananchi wake hawana Mikate akajibu kwa kifaransa “Qu’ils mangent de la brioche” kwa maana ya kiingereza “Let them eat cake" kwa kiswahili kisicho rasmi Sana ni kuwa Waambie wale Keki.

Inatajwa kuwa Brioche waliyoambiwa wale kilikuwa Chakula Cha matajiri Sana Ufaransa, ambacho kwa walalahoi wa Ufaransa walikuwa hawawezi kukinunua ndio maana walikuwa wanahitaji mikate. Baada ya kauli ile Kutoka Malkia alipinduliwa na wananchi wenye hasira Kali.

Leo naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Bi Stella Manyanya ameambiwa Sukari imepanda Bei na kufikia shilingi 3000 kwa kilo Moja yeye akajibu watu watumie asali. Kitu ambacho Manyanya hajui ni kuwa asali Ni ghali kuliko Sukari na asali kwa Sasa Ni Chakula Cha matajiri.

Lita Moja tu ya asali ni shilingi 10,000 sawa na kilo tatu za Sukari za mlalahoi. Manyanya yeye kununua hata ndoo ya Asali si big issue kipato kinaruhusu. Nafikiria familia ya watu watano pale kijijini ambao kipato cha Kaya Ni shilingi elfu 3 kwa siku au chini ya hapo wanaweza kununua lita Moja ya Asali? Je wataitumia siku ngapi? Asali siku hizi ni anasa kubwa Sana kwa watu Manyanya asitutukane.

Najiuliza je asali inafaa kutumika kwenye kuoka Mikate? Kwenye utengenezaji wa vinywaji huku kijijini? Kwenye maandazi tutaweka asali?

Ni kweli kuwa Manyanya hawezi kutengeneza Mbinu za Sukari kushuka Bei? Yaani akili yake imeshindwa kumnasua mlalahoi wa Tanzania ambaye Chai ndio kinywaji chake Cha kifahari? Sasa tunamlipa mshara na kumpa V8 la Nini Kama hata Jambo dogo hivi anashindwa kulitatua?

Akili kubwa ni Mali ya Rais, ndio wanaotakiwa kumzunguka Rais hawa ndio akili kubwa ya Tanzania ambayo inatakiwa kuhudumia watanzania?

Albert Einstein aliwahi kusema "We can't solve problems by using the same kind of thinking we used when we created them" huyu jamaa alikuwa na akili sana yaani akili iliyotengeneza tatizo haiwezekani ikatatua tatizo hilo. Tunawaza kidogo sana Manyanya aangalie hata wenzetu huko njee wanafanyaje hasa katika kipindi hiki Cha Korona.
 
leo nimenunua packat 1 ya kilo 1 kwa tzs.2,900/= ilhali siku sita zilizopita nilinunua kiasi hicho cha sukari kwa tzs.2,600/= je stockist mwenye tani 3 anatengenezewa utakatishaji wa laki 9!! an astornishing black market!! and its very blue that covid.19 makes +ve impacts among others. why our government smiles for such act?
 
''Asali kwa sasa inauzwa kati ya Sh 12,000 hadi 15,000.'' ni kwa Litre ngpi hii bei?
 
Sikuwa nimefikiria suala la kupanda bei, bali ilikuwa kwaajili ya kupunguza mizunguko ya mjini kipindi hiki kigumu cha maambukizi, mwezi uliopita nilinunua sukari mfuko 1, mahindi gunia 3 (mawili nikawagawia ndugu), mchele 100kg (50kg nikawagawia ndugu), viazi mviringo 80kg (60kg nikawagawia ndugu), unga wa mahindi 40kg, maharage 40kg, mafulta 20l, unga wa ngano 25kg, dawa muhimu, na vingine vidogo vidogo. Kumbe niliepuka na bei pia bila kupanga.

Ushauri - hata kama vitu vimepanda, kama inawezekana, ni vema kufanya manunuzi in bulk. Hatujua hali ya mbeleni. Bei zinaweza kupanda zaidi.
 
Sukari na asali nadhani ni substitute products kwa hiyo kama asali itakuwa ni alternative ya sukari ni wazi kuwa asali nayo itapanda bei zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…