Nailaumu CHADEMA kuwa hawajui wanataka nini

Pascal Mayalla,
Nakiri nilidhani namfahamu Mwambe, kumbe I was wrong!. Just imagine kama mtu kama huyu ndiye angekuwa Mwenyekiti wa Chadema!.
I was terribly wrong, nisameheni!.
P
Paskali, ukiona mtu anashabikiwa sana na wipinzani wako kuwa ndiyo anayofaa kukalia hicho kiti chako ujue kuna jambo nyuma ya pazia. Hata vumbi halijatulia, umma umejua Mwambe alikuwa anatetea maslahi ya nani.
 
Pascal Mayalla,
Nakiri nilidhani namfahamu Mwambe, kumbe I was wrong!. Just imagine kama mtu kama huyu ndiye angekuwa Mwenyekiti wa Chadema!.
I was terribly wrong, nisameheni!.
P
Aisee,au mkuu nawe ulikuwa unajuwa mpango mzima na ukawa chachu ya kuiangusha CDM?Leo hii angekuwa mwenyekiti kwa msaada wako,hatma ya upinzani nchi hii ingekuwaje?
 
Eti Mwambe atai transform Chadema! Duh Paskali buana...
 
Chadema ni chama kikongwe ambacho it never learns, hakijifunzi kwa makosa, and it keeps repeating makosa yale yale yanayokuja kukigharimu chama mbele ya safari.

Mimi ni miongoni mwa watu wachache humu jf ambaye niliisoma katiba ya Chadema kuliko hata baadhi ya wanachadema wenyewe.

Hawa japo wamefukuzwa, kufukuzwa huku hakukufuata utaratibu.

Ila kwa vile Bunge linavunjwa tarehe 28 ya mwezi huu, nawashauri waliofukuzwa wakubali tuu matokeo na kuachana na Chadema kwa amani bila kuibua mgogoro wowote kwasababu Spika atawalinda Bungeni wasifukuzike hadi Bunge livunjwe.

Swali ni when will Chadema learn from its past mistakes?!. Katiba ya Chadema ipo, taratibu za kufuata zipo, kwanini hawafuati katiba yao, sheria zao, taratibu zao na kanuni zao?. Tukiwaambia huu ni uhuni.
P
 

Vyama vya Tanzania ndugu yangu ni pasua kichwa tu

Hope unakumbuka na Lipumba alifukuza wabunge 8 kwa mara moja kwa stail ya aina hii na hakuna mtu alisema chochote

Me nadhani kuna ugomvi kati ya spika na mbowe, coz I'm sure pesa watarudisha but watapata wapi vipimo?

Hapo sasa ndio patamu,
 
Paskali, ukiona mtu anashabikiwa sana na wipinzani wako kuwa ndiyo anayofaa kukalia hicho kiti chako ujue kuna jambo nyuma ya pazia. Hata vumbi halijatulia, umma umejua Mwambe alikuwa anatetea maslahi ya nani.

Mwambe was just a MERCENARY kwa lugha yetu MAMLUKI! Kama CHADEMA ingejichanganya angeliuza Chama chote kwa CCM. Yaleyale ya Mzee wa Kiraracha na TLP yake kumwunga Mkono Magufuli apite bila kupingwa! Pambaf.
 
Busara ya kukaa kimya ni nzuri sana kama kuna watu wanaielewa
Ndiyo maana kwangu mfano wa uongozi ni maaskofu( hawawahi wala hawachelewi ili wasisababishe kifo na yeye asijiue)
Maamuzi ya kiongozi lazima yawe na chembe ya wema na haki kwani wanaperfom kazi ya Mungu hivyo wakishindwa wao wanakuwa wamehesabiwa dhambi

Je adhabu hii inawema? Imetoa haki kati ya aliyekosewa( chama) na mkosaji (mbunge)?
Adhabu hii haijasababisha kifo kwa mkosaji( all aspects) au mkosewa ( chama) hajajisababishia kifo?

Ukitazama Cdm hasa viongozi wakuu wanaonekana kuzishiriki shida zote za magu yaani hawana tofauti( inaonekana cdm hakuna watu wenye hofu kamili ya mungu na kuogopa makosa ya sharia ya maumbile pia sharia zingine za Mungu )



Kamati kuu inawatu kama mdee, mnyika, Jacob, na wengine ambao asili ni waropokaji, wajeuri na hawana utii hivyo si rahisi kuona wema wa mkosaji au safari ya gari lao, msipobadili Hali ya akili na tabia ya viongozi hasa kamati kuu ni ngumu kuona mayai ya nyoka
 
Pascal Mayalla chadema ni usiniguse.
Chama kina wapenzi wa damu, sema huko juu ndiko kuna matatizo.
Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna neno umelisema kuhusu huko juu, naomba nisilirudie, ila wakati wa tathmini ya matokeo fulani, nitakumbushia...
P
 
Mkuu Mshana Jr, kwanza heshima mbele, hakuna mtu yoyote anayeiombea Chadema ife, kosa langu ni kuwa mkweli too much.

Humu jf tuna members wa aina 3, tuna
  1. Simple minds, discuss people, wao badala ya kujadili hoja iliyo mezani, hawa watamjadili mtoa hoja.
  2. Ordinary minds, discuss events, hawa watadili matukio, nini kimetokea etc
  3. Great minds discuss ideas, hawa watajadili hoja iliyo mezani.
Hivyo naomba keep on being free, kujadili watu, matukio na hoja, katika mabandiko yangu, ukiweza kujibu hoja, nitashukuru, ila hata ukinijadili, sikulaumu na likes nakutwangia.
Ukipata muda karibu ujibu hoja za bandiko hili.

Asante
P
 
Ukipitia comments katika hili bandiko ni rahisi kugundua mambo mawili kwa haraka.
1. CHADEMA ni chama kikubwa lakini kinaendeshwa kama taasisi ndogo. Wakiweza kubadilika katika eneo hili wanaweza kuvuta wengi kwenye chama.
2. Wanachama wengi wa CHADEMA hawana muda wa kuwa na "free reasoning" katika mambo yanayotokea katika chama chao. Dalili kubwa la hili ni wote kuwa na matumizi ya neno moja katika baadhi ya matukio. Mtu akifukuzwa hoja huwa "alikuwa msaliti", sasa unajiuliza nani aligundua huyu kuwa ni msaliti? Nani amethibitisha usaliti huo?
3. CHADEMA kinapigwa vita, hii ni wazi lakini CHADEMA haina mbinu bora za kupambana katika vita hiyo.
4. Mwenyekiti wa CHADEMA anaweza kuwa ana mawazo mazuri sana ama anazungukwa na watu ambao wanamtegemea yeye kuamua na wao kuunga mkono. Simlaumu Mbowe kwa uwezo wake ninalaumu viongozi wenzake kwa udumavu wa mawazo kiasi ambacho inaonekana mawazo, mipango na maamuzi yote ni ya Mbowe. Wale wanaokimbia kambi ndicho wanachosema sio kwa sababu ya udikteta wa Mbowe bali kwa sababu ya uzembe wao.
5. Wameelekeza nguvu mahali pasipopaswa; CHADEMA imegeuka kuwa chama cha harakati na kukosoa mitandaoni badala ya kujenga chama. Matokeo yake inapoteza mvuto kwa watanzania wa kawaida ambao ndio wanaoathirika na sera mbovu za nchi hii.

6. Epukeni tabia ya kushambulia mtu aliyehama chama. Inakuwaje chama pamoja na viongozi wake mnatumia muda wenu kumjibu mtu mmoja tena mgeni kwenye chama. Kwanini chama kisitoe taarifa moja kukanusha madai ya mbunge mmoja aliyehama chama na sio kumjibu kila mtu kwa wakati wake? Hii haina faida kwa CHADEMA.

CHADEMA iwekeze kwenye siasa, ijijenge kama chama kikuu cha upinzani, kiwe na nyenzo kama redio au hata televisheni bila kusahau kuwa na majengo ya ofisi yanayoeleweka katika kila mkoa na wilaya. Huwezi kuwa na chama ambacho hakina hata ofisi ya kueleweka licha ya ruzuku na michango kutoka kwa wabunge.
Mkibadilika ni rahisi kuchukua hii nchi, ila mkiona mpo sahihi katika kila kitu kuna hatihati ya kuwa na wabunge watano October 2020.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chadema ni chama bora sana cha siasa kuwahi kuwepo Tanzania, ni chama ambacho kimejengwa katika misingi imara na thabiti, miaka hii mitano ya uongozi wa awamu ya tano ya ccm uongozi ambao umekubuhu kwa kuvunja katiba ya nchi, kutawala kwa kuvunja sheria kanuni na taratibu imetuthibitishia hilo.
 
Si kweli inawezakana wewe ndio haujui wanataka nini lakini wao wanajua na wanapata wanchokitaka.
 
Baada ya wana Hai kusema kupitia kura zao, naamini sasa hoja hizi zitazingatiwa, Mhe. Mbowe apumzike.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…