Nailaumu CHADEMA kuwa hawajui wanataka nini

Nailaumu CHADEMA kuwa hawajui wanataka nini

Huyu Bwana Pascal Mayalla ni Janga kweli, bado anaamini kuwa Rais atamfikiria kama wakina Mtatiro, lakini ndiyo hivyo ni kama Fisi anangojea Mkono wa Binadamu Udondoke.
Jamii ya Kujipendekeza na Kusifu tu! Hovyo kabisa.
 
Ili CHADEMA iendelee kuwepo wamuchague Mwambe!!? Uache masihara.
Pamoja na mapungufu ya Mbowe, bado ni mtu sahihi wa kuingoza Chadema kwa sasa.

Kwa style Serikali ya Jiwe inavyonyanyasa wapinzani, sifa kuu ya Mwenyekiti wa chama ni lazima awe na uwezo wa mkubwa wa kiuchumi, kumkabidhi mtu dhaifu kiuchumi jahazi litazama, ndicho unachoshauri!

Pia uenyekiti unaweza kumpa Tundu Lissu, kwa sababu ya ufahamu wake mkubwa na kujiamini kwake kunakopita viwango vya watu wengi.

Vinginevyo wewe Paskali utakuwa ni malaika kuzimu. Tunakukataa, ushindwe na ulegee!
 
Pascal Mayalla,
We Paskali acha unafiki, wakati CDM inahujumiwa waziwazi huwa upo kimya, CHADEMA na wapinzani wamefungiwa kufanya siasa karibu mwaka wa 4 sasa wakati Katiba na Sheria ya nchi inaruhusu mbona kalamu yako hatujawahi kuisoma ikiandika uonevu huo.

Unajua kwamba CHADEMA ni taasisi inayojitambua, Kiongozi mkuu wa taasisi ndiyo mboni ya taasisi husika, kuna vetting lazima ifanyike before na pre-agreement nzito na bodi nzima ijiridhishe kwamba huyo anayetaka kuongoza taasisi kashiba nondo, viatu vinatosha na anaendana na philosophy ya taasisi husika.

Sasa huwezi kulala ukaibuka ati unataka kuongoza CRDB benki kisa una Masters ya Uchumi na CPA, hapana mambo huwa hayaendi hivyo.. unajua kila kitu ila kwa sababu unapenda kuandika kuhusu CHADEMA in negative well and good.
 
Nimejiuliza swali moja baada ya kusoma mchango wa Wakudadavuwa hapo juu, jee makala hii ukiipeleka HabariLeo na mhariri akawa na akili za "kaka" yetu Wakudada atakimbilia kuichapa makala hii kwa wazo kuwa umehitimisha kuwa Chadema kama wanajitambua sasa watamchagua Mwambe ili chama kisife?
Kweli ukongwe katika fani wakati mwingine ni safi sana kama utatumia kikamilifu.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
CHADEMA sio kachama kadogo na tulitaka wafanye uchaguzi na mimi nawaombea uchaguzi mwema usio na figisu. Kama uchaguzi wao utakuwa huru basi ni wao wenyewe kuamua nini wanataka na nani awaongoze.

Hakuna ubaya kuwashauri na kutoa sababu za msingi kwa ushauri huo, lakini naona wengi wetu tunatumia hisia tu.
Kwangu mimi la msingi wakisha fanya uchaguzi wao kazi yao kubwa ni kutuaminisha sisi tusio wanachama CHADEMA inasimamia nini-hasa baada ya lile timbwili la 2015 lililokwenda na kubadilisha gia angani.

Binafsi sikujua yule Bw. Lowassa anasimamia nini, na hata angeshinda akashika dola je angekuwa mtiifu kwa yale chama kilituaminisha au angekuja na yake na kuanza kukiburuza chama. Na kweli mpaka ameondoka sijui alikuwa anasimamia nini.

Wote Lowassa na Sumaye wameshatoka sasa tuwasikie CHADEMA kwa nini wanataka kura zetu. Uchaguzi wa mwenyekiti ukienda vizuri utaboost msimamo wao. Pili waliangalie swala la utawala bora (hapa TL) ni hazina lakini wafikirie jinsi ya kuunganisha utawala bora na maendeleo na ILANI ZAO ZILIZOPITA. Kwa mfano mambo ya SGR tuliyasikia kwanza kutoka kwa SLAA/CDM, Elimu bure. Wazo lingine ni lile la nyumba bora na kadhalika.

Pamoja na hayo yote KATIBA na UCHAGUZI HURU pamoja na kuwa na bajeti ya kupeleka kesi mahakamani inapobidi ni mambo ya msingi.

Katika kuchagua viongozi wao ni wazi wanatakiwa wapate timu inayoweza kupambana kimbinu na Jiwe.
 
Mwandishi wa habari hujui kuandika? KKK vipi zilikupita kushoto? Hujui sifa ya swali? Unatumia nini kufikiri? unatumia nini kuandika?
Anatumia moyo! ndio maana ana huba na mahaba, sudi na husuda,nyongo na kinyongo!
 
Back
Top Bottom