Kuna mtu kwenye uzi mmoja alikua anaomba ushauri kuhusu mradi wa kuku.
Nilimpa ushauri huu ambao nimeona niupost hapa huenda wanaofuatilia uzi huu wakapata kitu kidogo cha kujifunza.
πππ
Mwaka 2019 nilikua nna wazo kama lako, na ni mawazo ya wafugaji wengi sana. Tofauti yangu na wewe ni idadi ya mifugo mi nilitamani nifikishe 1000 ndani ya mwaka mmoja we unahitaji kufikisha 5000 ndani ya mwaka na nusu.
Nilianza vizuri japo sikufikia malengo na nnaendelea kufuga mpaka leo lakini nilijifunza yafuatayo;
KWANZA
Kufuga kuku chotara ili umuuze kwa ajili ya nyama (kwa kutegemea soko la kawaida tofauti na special oder) zaidi ya miezi mitatu haitakulipa. Wanunuzi wengi wananunua kuku si zaidi ya 10,000 (ila inategemea na eneo ulipo hii ni kwa experience ya eneo nililopo.)
Hivyo basi hakikisha mipango na malengo yako yanachezea humo.
PILI
Hakuna tija(wala sio sifa) ya kuwa na kuku wa nyama 5000 kwa wakati mmoja ambao running cost inapanda kuliko selling price (mfano kuku 100 wanaweza wakala mfuko mmoja wa 80,000 lakini gharama yake ya kuuzwa ikalingana na kabla kula mfuko huo( labda wawe wa mayai ambao utakua unaokota mayai kila siku.
Hivyo basi ni bora ukawa na batch ya kuku wachache ambao watatoka kwa wakati tofauti tofauti ili kuepuka gharama za ziada ambazo zinapunguza faida. Mfano unaweza ukaamua kila wiki unauza kuku 100 au 200 au 300, so unakua unaingiza vifaranga 100 au 200 au 300 kila wiki wanaenda kwa mfululizo huo na idadi itaongezeka kila uhitaji wa soko utakavyoongezeka.
TATU
Chakula bora ni gharama sana hivyo unatakiwa kuanzisha mpango wa kutengeneza chakula mbadala kama vile hydroponic, azola na funza.
NNE
Ili kufikia malengo kwa wakati na kwa gharama nafuu fanya yafuatayo;
*Andaa kuku wazazi kwa ajili ya kutaga mayai ya kutotolesha kutokana na malengo yako ya mwezi. Kwa mfano unahitaji vifaranga 400 inahitaji kuku wazazi 100 tu.
Kuku hao watakua na uwezo wa kutaga sio chini ya tray 2(mayai 60)(za mayai yanayofaa kutotolesha) kwa siku na kwa siku 10 itakua una mayai 600. Kati ya mayai 600 huwezi kukosa kuku 400 kuanzia vifaranga mpaka kufikia kuku anaefaa kuuzwa. Hapa ni kwa malengo ya kuuza kuku 100 kila wiki, kwahiyo kwa mwezi kuku 400
Kumbuka idadi hii nnayokupa ni idadi ya chini kabisa ambayo hata zikitokea changamoto ni ngumu sana kushuka chini ya idadi hiyo.
Mfano kuku wazazi 100 wanaweza kuzalisha mpaka mayai 75 kwa siku, na mayai 600 yanaweza kutototewa mpaka vifaranga 500.
Hapo ukiangalia maelezo vizuri utagundua mayai ya kila mwezi wa kutotolesha yanapatikana ndani ya siku 10 tu, hizo siku zilizobaki utauza mayai ili kuendelea kupata hela ya kuhudumia kuku wazazi.
Biashara ikiwa nzuri utaongeza idadi ya kuku wazazi na mpango utakua kama hapo nilivyo eleza.
MWISHO
Kumbuka biashara ni hatua, so huwezi kuingia sokoni na kuku 1000, lazima uanze kuuza kidogo mpaka soko likutambue na upate wateja wa kutosha ili uuze mpaka zaidi ya idadi hiyo.