Mrejesho 1
Tarehe 26/04/2022 nilichukua box mbili za vifaranga vya sasso kutoka makota Iringa kila box lilikuwa na vifaranga 102 ivyo ikafanya idadi na kuwa 204
Maandalizi ni kama yafuatayo
1 Chakula (Nilitengeneza mm mwenyewe kama ifuatavyo)
starter inabid iwe na 20-18 % ya Digestible Crude Protein ( DCP) ili kufanya kifaranga kiote manyoya haraka ili kujikinga na baridi, Chakula hichi watakula kwa miezi miwili then nitabadilisha mfumo wa kuchanganya
Mahindi yalio balazwa 65 Kg
Mashudu yalio balazwa 22 kg
Uduvi ule mdogo wa langi ya red-silver 8 kg
Diphosphate calcium (DCP) 1 kg
Chokaa ya kuku 2.50 kg
Mifupa 1 kg
Chumvi ya jikon 500 g
Nilitengeneza 100 kg Kwa awamu ya kwanza lengo la kufanya ivyo ili chakula kisikae muda mlefu kikawa na Sumukuvu maana huwa inasababisha kuku kufa
Ili kupata Mahindi na mashudu yalio balazwa inabidi uende mashineni wanapo saga unga wa ugali then unamwambia yule operator atoe ile chekeche kwenye machine ya kusagia then akipitisha ayo Mahindi zinatokea chenga chenga ambazo kifaranga kitaweza kula vizuri
2 Jiko
Nilinunuwa Yale majiko special kwa ajili ya vifaranga yapo kama chungu ivi lkn kina matundu pembeni na mfuniko juu
Ivyo kama moto ukiwaka tayali nafunika juu na ule mfuniko ivyo joto linaweza kudumu kwa muda wa masaa 5-6 endapo ukifunika lkn ukiacha wazi 2-3 masaa tayali joto linapotea
3 Sehemu vifaranga vinapo shinda
Nilinunuwa magazeti kilo 3 na board moja, mbao ya 2 by 4 na mapumba ya mpunga ( rice husk )
Mapumba ya mpunga nilitandika chini ili kuzuia unyevu usipande juu na kunyonya maji endapo yakimwagika
Magazeti kwa ajili ya kutandika chini maana inabid utandike matabaka 3 ya magazeti then kila siku lile tabaka la juu unalitoa then unaweka lingine
Board kwa ajili ya kutengeneza round ili vifaranga wasife maana wanatabia ya kujikusanya kwenye Kona kwa pamoja ivyo ukutumia board sio lahisi kupata Kona
Mbao 2 by 4 izi ni kwa ajili ya kuunganisha board moja na nyingine ivyo nilizichana kidogo katikati ili kukutanisha board mbili na kutengeneza round
Eneo nililo tumia kwa hatua za mwanzo ni 1.5 m kwa 1.5 ili vifaranga wapate joto na muda mwingi watumie kula na kupumzika kuliko kutembea lkn baada ya week ya pili nitaongeza ukubwa wa eneo
4 Vyombo vya kulia
Nilinunuwa dinker 4 na feeder 6 Kwa awamu ya kwanza lkn kwa upande wa feeder natumia kile kisahani tuu
5 Mpangilio wa kimiminika ( Maji)
Ile siku nilio waleta ( hii siku sio siku ya kwanza maana siku inakuwa na masaa 24 ivyo inakuwa Zero day) niliwapa maji yenye mchanganyiko wa Glucose na Vitamin kwa masaa mawili kabla sija wapa chakula lengo la kufanya ivyo ni kuwapatia nguvu kutokana na uchovu wa safari na kufungua mfumo wa kumengenya chakula
Siku ya kwanza hadi ya Tano
Niliwapa maji yenye mchanganyiko wa Antibiotic lengo la kufanya ivyo nikukausha vitovu ili wasipate tatizo choo kuganda ( Constipation )
Siku ya sita ambayo ni Leo
Niliwapa maji ambayo ayana mchanganyiko wa kitu chochote kile
Siku ya Saba ambayo ni kesho
Nitawapa chakula then baada ya masaa manne nitawapa maji yenye mchanganyiko wa dawa ya kideli (Newcestle) kwa masaa mawili tuu then baada ya hapo nitawapa maji ya kawaida
Mafanikio
✓Hadi sasa akijafa ata kifaranga kimoja
✓Akuna kifaranga kilicho pata ulemavu
✓Asilimia 75 ya vifaranga mabawa Yao tayali yamefunikwa na manyoya ivyo inaonyesha chakula ni kizuri kwa hatua za mwanzo za ukuaji
✓Vifaranga vinakula sana mida ya asubuhi kuliko mchana ivyo inaonyesha afya Yao ni nzuri na mfumo wa umengenyaji umekaa vizuri
✓Akuna kifaranga aliye pata tatizo la choo kigumu
Changamoto
✓Kila baada ya masaa manne inabidi niwepo bandani ivyo inakuwa vigumu kufanya ivyo maana nakuwa nipo kwenye majukumu memgine kwaiyo inabid kila baada ya masaa sita ndio niwepo bandani
✓Kuamka usiku inakuwa ni tatizo maana sijazoea ivyo Kuna bahadhi ya siku huwa napitiliza hadi asubuhi
✓Vifaranga vinapendelea sana uduvi kuliko Mahindi na mashudu ivyo inabid nisubilie kwanza then ndio wanaanza kula Mahindi na mashudu
Mwisho
Mrejesho 2 nitauleta tena jumatatu ijayo Yani siku ya 13
View attachment 2208838View attachment 2208839View attachment 2208840