Naingia kwenye kufuga kuku chotara (Saso)

Mrejesho 2

Siku ya Nane niliwapa maji yenye mchanganyiko na vitamins kwa siku nzima

Then siku ya Tisa hadi ya Kumi na mbili niliwapo Amprolium 20% kwa ajili ya Coccidiosis maana huwa wanakula kinyesi chao ivyo nilazima niwepe dawa ili kuepusha vifo

Siku ya Kumi na tatu niliwapa maji bila kuchanganya na kitu chochote kile

Siku ya Kumi na nne ambayo ni Leo niliwapa chanjo ya Gumboro

Kuhusu eneo saiv nimeongezea ili wapate nafasi ya kucheza ili mifupa ikae sawa

Mafanikio

Saiv ukuwaji wao upo kwa kiasi Cha juu maana kila siku naona mabadiliko

Asilimia 100 saiv wameota manyoya ivyo naweza kutofautisha yupi jogoo na yupi tetea

Saiv siwashi tena moto mchana ivyo ni usiku tuu


Changamoto

Siku ya Nane walianza kuumwa na ugonjwa wa Coccidiosis ivyo sikuweza kuwapa dawa maana nilikuwa tayali nimewapa maji yenye vitamin ( vitamin C huwa vinazuia ufanyaji kazi wa Amprolium ivyo kama ningewapa isingeweza kufanya kazi) kwaiyo vifaranga 2 walikufa

Siku ya Kumi vifaranga 5 walikuwa awawezi kutembea ivyo ilinibid kuwapa maji yenye mchanganyiko wa chumvi, DCP, Mifupa na Chokaa kwa siku moja then siku ya Kumi na mbili waliaanza kutembea vizuri

Mrejesho 3 nitaleta week ijayo siku kama ya Leo
 
Vifaranga wakiota mabawa, unajuaje yupi ni Jogoo?! Yupi ni Tetea?
 
kedekede?
Unaweza fuga kuku wa mayai (layers) nakuwawekea majogoo wa kienyeji na wakataga vizuri tuu na kuweza kutotolesha ila uwe mpole angalau ule mwezi wa kwanza wakutaga ule mayai tuu halafu ukiwa umejiridhisha majogoo wamefanya kazi yao ndio hapo utapata mayai yenye mbegu
 
Mkuu iyo kitu usije kujalibu maana hao vifaranga watakuwa wazaifu sana bora jogoo awe wakisasa then tetea awe wa kienyeji lkn tofauti na apo uwezi pata kifaranga kitakacho kua
 
Mkuu iyo kitu usije kujalibu maana hao vifaranga watakuwa wazaifu sana bora jogoo awe wakisasa then tetea awe wa kienyeji lkn tofauti na apo uwezi pata kifaranga kitakacho kua
Niliona doctor mmoja anasrma nakapata vifaranga vizuri tuu hata sikufatiliaga kama vilitoboa,mimi nafuga layers wakisasa na chotara Sijawahi kuchanganya mambo nachukua tuu kwenye makampuni
 
Karibu kwenye ufugaji mkuu. Tuko pamoja
 
Karibu kwenye ufugaji mkuu. Tuko pamoja
Mkuu hongera sana kwa hatua uliyofikia, mimi pia ni mfugaji ila nafiga kienyeji tu kwa ajili ya kula ila nataka nifuge kitalamu zaidi.

Swali langu, ningependa unifafanulie je, naweza kuwafuga viraranga wakiwa juu ya wavu kwanzia day 1 ili kuepusha magaonjwa ama ni hadi wafike siku fulani ndo niwaamishie juu ya wavu? Manake naona hii njia ndo iko safe sana kwa kuzuia magomjwa.
 
Wadau, ni kampuni zipi kubwa ambazo naweza agiza vifaranga wa kuku chotara (F1) ?
 
Picha mkuu
 
S
Thanks boss, ni unazifahamu hizi mbili tu ? Kuna jamaa nliona sehemu alisema kuwa vifaranga wa kununua kutoka silverland wanapukutika sana.
asso uwe na banda zuri linye kupitisha hewa na uvilee kama mayai vikiwa wadogo kwa mtaokeo mazuri tumia chakula chao,wakipita mwezi wanakaa vizuri,sasso ni kwa ajili ya nyama na wala si watagaji sana sababu wanamaumbo makubwa,wahi kuchanja ndui kwa kuku yoyote utakayenunua if possible week ya tatu
 
Poa poa mkuu, but ndui si chanjo ya mwisho baada ya chanjo zote zile kuzirudia mara mbili ?
 
Poa poa mkuu, but ndui si chanjo ya mwisho baada ya chanjo zote zile kuzirudia mara mbili ?
Hakuna utaratibu maalumu wa utoaji wa chanjo mkuu, kuiweka chanjo ya pox mwisho ni utaratibu tu ambao uliwekwa kipindi ambacho ugonjwa wa Ndui haujawa pasua kichwa kama hivi sasa

Kwa sasa kumekuwa na mlipuko wa Ndui kuliko ata Mdondo, na ukisubiri hadi mwezi na week unaweza jikuta teyari vifaranga wako wamepata Ndui, ndomana hapo jamaa amekushauri uchanje ikiwezekana week ya 3

Kuna maeneo me nayajua siku hizi chanjo ya Ndui ndio inaanza na zingine zinafatia, hiyo yote imetokana na mlipuko wa Ndui kuenea Kwa kasi sana na kupelekea vifaranga wa week 1 tu wanapata Ndui

Kwahiyo we fatilia eneo lako Kwa wafugaji wengine kuhusu issue ya Ndui likoje, kama bado liko salama sawa, Kwa majibu utakayopata basi ndio utayatumia kwenye mpangilio wako wa Chanjo
 
Thank you for the lesson Boss🙏 nlikuwa sijui Hilo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…