Naingia Shambani very serious kulima Alizeti

Naingia Shambani very serious kulima Alizeti

Mayu

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2010
Posts
7,621
Reaction score
12,505
Wakuu,

Binafsi huwa na Bet sana na bahati nzuri nimemuotea muhindi kama Milioni 40

Na sasa nataka kubet kwenye kilimo

Mwaka huu naingia shambani kweli kweli sio utani, naingia FRONT na sio simu

Nakwenda kulima ekari 50 za alizeti MBUGANI kisha nikitoa naweka dengu

Eneo SINGIDA kwetu kabisa

Matumizi (makadirio ya juu kabisa) kwa ekari 50
  • Kukodi shamba m 2.5
  • Kulima shamba m 2.5
  • Kupanda m 1
  • Kupalilia shamba m 2.5
  • Mbegu lk 7
  • Uvunaji/upakiaji m 2
  • Mengineyo m 2

Jumla milion 13.2
Jumlisha hidden cost jumla iwe milioni 15

MAVUNO (makadirio ya chini)
Eka moja gunia 7 badala ya 15 za wataalamu
Ekari50 x Gunia 7
Jumla inakua gunia 350

Wastani gunia moja hutoa mafuta dumu 2 bei makadirio ya chini sh elf 50 kwa dumu( dumu linakwenda hadi laki+)

350 x 2 inakuwa dumu 700
Dumu700 x elf50 unapata Sh M35
Hapo nime-assume mashudu yamelipia gharama ya ukanuaji

JUMUISHO
M35 -M15 = M20 Faida


DENGU
Ukitoa tu alizeti unavizia nvua za mwishoni kabisa unalima dengu shamba hilo hilo hulipi gharama za kukodi tena

  • Kulima m 2.5
  • Mbegu m 2
  • Kupanda lk 5
  • Madawa (emergency) m2
  • Kuvuna/kupakia 2m
  • Mengineyo m 1
Jumla milioni 10
Hidden cost milioni 2
Jumla milioni 12

MAUZO
Wastani gunia 4 kwa eka badala ya gunia 8 hadi 10 kwa eka za wataalamu

Ekari50 x Gunia 4 unapata gunia 200
Gunia la dengu lina wastani wa sh Laki 1

Laki 1 x gunia 200 unapata M 20

JUMUISHO
M20 - M12 = M8 Faida

FAIDA KUU (alizeti na dengu)
M20 +M8 = M28

NB
Nimeweka makadirio ya juu sana kwenye matumizi

Na nikaweka makadirio ya chini sana kwenye mavuno na bei

Dua zenu jamani

Ntaleta MREJESHO iwe nime Lost au nime Win

MREJESHO (UPDATES) 24/03/2022

Wakuu kwema
So far mkeka wangu wa kilimo cha Alizeti unakwenda vizuri sana baada ya zile ODDS kubwa na ngumu kutick
ODDS ngumu kabisa zilikua ni MVUA na PALIZI

SHAMBA EKARI 20
Mpaka sasa nimelima ekari 20 tu...... hii ni baada ya wadau mbali mbali kushauri ekari 50 is too risk ikiwa huna UZOEFU na ikizingatiwa mamlaka ya hali ya hewa ilitabiri mvua zitakua chache

MBEGU (ASA)
Baada ya mchakato wa kitaalamu nikashauriwa nitumie mbegu za Serikali ASA na nilinunua mfuko wa kilo 2 kwa sh 5,000 tu, nilipata mchongo huu kwakuwa nilinunua kwa wingi

Sijatumia MBOLEA yoyote wala sijatumia viatilifu vyovyote kwasababu nimelima MBUGANI aridhi imeshiba na Alizeti haishambuliwi sana na magonjwa


UPDATES

Leo hii nimemalizana na PALIZI na mimea inakwenda vizuri kwa sehemu kubwa

Mpaka sasa SIJAKUTANA na gharama yoyote ambayo imenishtua kwa maana ya kwamba labda ni gharama ambayo sikuifikiria au gharama kuwa kubwa zaidi ya nilivyo KADIRIA
Zaidi mbegu imenipa UNAFUU mkubwa sana, nilipanga kutumia Hysuan Kg 2 kwa 35,000
Lakini nimetumia ASA Kg 2 kwa sha 5,000 na nilinunua mifuko ya Kg2 mifuko 80, yaani eka moja kwa mifuko 4, hapo nime save karibu 2m...... Naishukuru sana serikali kwa hili [emoji120][emoji120]
Ingawaje sijajua ubora wake baada ya mavuno

Ntaleta tena Mrejesho baada ya KUVUNA



MREJESHO (UPDATES)
GHARAMA so far

Shamba ekari 20
20 x 30,00 = 600,00
Shamba lilikua safii

Kulima
20 x 40,000 = 800,000

Mbegu (ASA)
80 x 5,000 = 400,000

Kupanda
20 x 30,000 = 600,000

Palizi
20 x 50,000 = 1,000,000

Mengineyo
1,000,000

Jumla kuu 4,500,000

Hadi sasa nimelaza shambani 4.5M
Bado gharama za kuvuna kupepeta na kuhifadhi


MREJESHO (UPDATES)

kuna kama eka nne na nusu nililima mwishoni naona zimepelea mvua maana mvua ndio imeindoka haijarudi na alizeti ndio inaanza kufunga maua

View attachment 2203797


MREJESHO (UPDATES)
Mavuno

GHARAMA za MAVUNO
Kuvuna Eka 20 x 30,000 = 6000,000
Kupiga na kupeta kwa mashine 1000 Guni 92,000
Mifuko. 50,000. 500
Usafiri 100,000
Vibarua na mengineyo 100,000

Jumla 1,000,000

Ukichukua gharama za awali kuanzia kukodi shamba, mbegu, kulima, palizi nk jumla ilikua 4,500,000
Ukijumlisha na hii ya uvunaji 1,000,000 jumla kuu ya GHARAMA ZOTE INAKUA 5,500,000

MAVUNO
Nimepata jumla ya gunia 92..........wastani wa gunia 4.6 kwa eka

Kwa sasa gunia la alizeti linauzwa 90,000(i hope litafika 150,000)

Nikisema niuze sasa maana yake ni
90,000 x 92 = 8,280,000

Kukokotoa Faida/hasara

Mauzo. 8,280,000
Gharama 5,500,000

8,280,000-5,500,000 = 2,780,000 FAIDA

Kwa sasa sina mpango wa kuuza alizeti wala kukamua
Nitaiweka stock hadi itakapo adimika bei itakua nzuri na mashudu yatakua bei juu pia
Kwa muda huu naanza kununua rasmi alizeti angalau gunia zingine 250 au 300 ili bajeti yangu ya 40m isogogee kidogo, kisha nitakuja kukamua na kuuza mafuta......nimekamua gunia moja nimepata lita 20 na point
Dengu nimeshindwa kulima sababu ya nvua mbuga imekauka sana

Namshukuru sana MUNGU na wote mlionipa moyo na hata walio nikatisha tamaa kwani walinipa chachu zaidi

Kikubwa nilicho jifunza kwenye kilimo ni usiwe mbahili kwenye mambo ya kitaalamu....... fuata exactly wataalam wanavyo shauri haswa kwenye
Muda wa kulima mapema
Kupanda kwa kanuni
Kupalilia kwa wakati
Uvunaji kuzuia kupoteza mazao mengi on process
Na mwisho simamia mwenye kila hatua

Kwa muda niliotumia na faida iliopo hadi sasa sio kubwa lakini kwangu mimi ni USHINDI mkubwa sana kwa maana ya UZOEFU
(Iwapo bei itafika 150,000 kama msimu uliopita basi nategemea kuuza 11m faida itakuja 5.5 sio mbaya)

Changamoto kubwa niliokutana nayo so far ni uzoefu na mvua kuondoka MAPEMA haswa kwenye eka nilizo lima mwishoni, vinginevyo ningepata hata wastani wa gunia 5-7 kwa eka

Next season nitarudi nikiwa na nguvu zaidi na ari zaidi
 
Kilimo!! Mvua zikizingua?

Sijaona gharama ya mbolea wala Madawa!! Au ndo hiyo 2m ya pembeni?
Mkuu MBUGA inajitosheleza na mbolea haswa kwa alizeti mbolea ni kwenye aridhi ya kawaida kichanga na mfinyanzi, na alizeti hainaga magonjwa ukanda huu

Kwa mujibu wa wataalamu nvua zitakua chache na mbuga huwa haitaki mvua nyingi kama ya mwaka juzi na jana
Ikizidi ndio itazingua

Kuhusu madawa dengu kuna msimu kukiwa na ukungu inahitaji madawa nimeweka m2 emergency
 
Ukiwa na mtaji kilimo cha kutegemea mvua usilime, nakupa mchanganuo ufuatao uone kidogo. Mwezi wa Tano alizeti inaanza kuiva Singida vijiji vya Misuna, com x, makunda, Tyandu, Kyengege, Maluga, Tumuli kwa uchache na wakati huo wewe mnunuzi wa stock unaenda kuanza manunuzi mwezi wa sita ambapo ndio alizeti imekomaa vizuri.

Umetenga milioni 13 unatakiwa ununue kila gunia elfu hamsini japo huwa kuna bei chini au zaidi ya hapo sasa tukadirie utanunua gunia 260 ambapo utaongeza gharama za stoo, mara nyingi unaweka mashineni hasa shelui kuna viwanda pale unaweka mzigo wako wataulinda siku zote hadi urudi kukoboa.
 
Kwa gunia 260 unarudi kuuza mwezi wa 10 au 11 au 12 kama hauna njaa kwa sasa gunia moja ya alizeti inauzwa laki naamini December na January itafika laki na 20, sasa hapo ndio unapiga 26m, ukitoa mtaji wako na runing cost kama 2m utabaki na faida ya 11m hapo ukumbuke pesa iko salama kabisa na haujabet
 
Mazao haya wewe fanya ununuzi tu, utatoka kama una mtaji nunua unachokiona kuliko kuexpect faida kubwa baadae uje kula mweleka ambao hautokuja kusahau maana huwezi kubet na pesa ukaweza. Na kilimo cha mvua hakiaminiki ukizingatia mwaka huu umeelezwa mvua sio ya kutosha.
 
Ukiwa na mtaji kilimo cha kutegemea mvua usilime, nakupa mchanganuo ufuatao uone kidogo. Mwezi wa Tano alizeti inaanza kuiva singida vijiji vya misuna, com x, makunda, tyandu, kyengege, maluga, tumuli kwa uchache na wakati huo wewe mnunuzi wa stock unaenda kuanza manunuzi mwezi wa sita ambapo ndio alizeti imekomaa vizuri, umetenga milioni 13 unatakiwa ununue kila gunia elfu hamsini japo hua kuna bei chini au zaidi ya hapo sasa tukadirie utanunua gunia 260 ambapo utaongeza gharama za stoo, mara nyingi unaweka mashineni hasa shelui kuna viwanda pale unaweka mzigo wako wataulinda siku zote hadi urudi kukoboa
Mkuu hii ni nzuri lakini changamoto zake ni muda na uaminifu
Kwenda kununua kiasi kikubwa peke yako ugenini inakua mtihani kidogo inabidi utumie madalali wa vijijini wanaojua kona zote, hapo lazima utadhulumiwa au utauziwa hadi mafamba

Ninapo lima ni nyumbani kabisa na nimepanga baada ya kumaliza kulima chenji ya m40 itakayo baki ntanunua alizeti hapa hapa vijiji vya kwetu ili ku boost kidogo

Madalali wanunuzi nao wasumbufu sana aisee
 
Leo nimenunua 1kg kwa 40,000

Heka moja 5-6Kg
Inaitwaje hiyo mbegu kuna mbegu ilijadiliwa sana humu nautafuta ule uzi siuoni nazan ndio hiyo mana naona bei zinaendana
 
Mkuu naomba nikushauri kitu Cha muhimu naomba uweke vibalua wa kuhamia ndege maana ndege hupunguza mavuno kwa asilimia 35- 80% ivyo jitahidi kuwa makini maana utalima eneo la mbugani kwaiyo ndege itakuwa ni tatizo kwa upande wako

Pia kuhusu palizi ni kwanzia week ya pili hadi ya sita toka kupanda

Kuhusu mbegu Kuna aina mbili moja inatoa mafuta mengi lkn mavuno madogo lkn nyingine mavuno mengi lkn mafuta kidogo kwaiyo inabidi uchague kutokana na soko lako
 
Data zako zko sahihi kwa approximately 50%...

Nikushauri, kuliko kutegemea mashudu yalipie garama za ukamuaji, ww ingia mfukon toa pesa, chukua shudu, peleka kiwanda cha Mount meru (Sunola) pale pale Singida. Utakuja unishukuru
 
Data zako zko sahihi kwa approximately 50%...

Nikushauri, kuliko kutegemea mashudu yalipie garama za ukamuaji, ww ingia mfukon toa pesa, chukua shudu, peleka kiwanda cha Mount meru (Sunola) pale pale Singida. Utakuja unishukuru
Ni wazo zuri sana maana kama ntapata idadi hiyo ya magunia basi shudu litakua jingi sana
Mkuu details hazipo sawa?

Mbona nimejitahidi sana kupandisha gharama na kushusha mavuno na mauzo kwa karibu nusu nusu?
 
Back
Top Bottom