Naishi Ndago na nina ishi mjini pia kwa vipindi tofauti tofauti. Kuhusu kilimo cha alizeti nafahamu nje ndani. Kuhusu watu wa Ndago ni kweli huwa wana fanya ziada kilimo cha alizeti walio wengi na huwa wana tumia aina ya kienyeji ya upandaji (kumimza)
Mkuu mwakani andaa shamba ekari moja kwenye mbuga isio jaa sana maji au kwenye nkulusi
Kama ni kichanga hakikisha unatumia mbolea ya kukuzia
Lima mapema kabisa mwezi wa 12 uwe umemaliza kulima alizeti
Panda mbegu ya kisasa kwa mstari na vipimo sahihi, ngolea libaki shina moja moja na mawili kwenye vichuguu au shamba lenye rutuba sana.
Palilia kwa wakati na palizi ya maana kama unavyopalilia mahindi( sio kuparaza kama wanavyofanya)
Kama aridhi ni kichanga weka mbolea ya kukuzia baada ya palizi
Vuna mapema usiache alizeti ikauke hadi ianze kupukutika na upepo au wakati wa kuvuna
Omba Mungu wako nvua zinyeshe za kutosha
Utanishukuru baadae
Usilime alizeti mwishoni mwezi wa pili huko
Usipande mbegu za kienyeji wala usipande kienyeji kwa kumwaga mbegu
Usiache mimea imebanana itazaa alizeti kama ngumi
Usianze palizi baada ya mimea kuzongwa na majani itadumaa
Usipalilie juu juu, palilia kama mahindi yanavyotaka