All TRUTH
JF-Expert Member
- Nov 20, 2011
- 5,453
- 2,569
Hongera sana tuView attachment 2236638
View attachment 2236639
MREJESHO WA MWISHO
GHARAMA za MAVUNO
Kuvuna Eka 20 x 30,000 = 6000,000
Kupiga na kupeta kwa mashine 1000 kwa gunia = 92,000
Mifuko. 50,000 500 kwa mfuko
Usafiri 100,000
Vibarua na mengineyo 100,000
Jumla 1,000,000
Ukichukua gharama za awali kuanzia kukodi shamba, mbegu, kulima, palizi nk jumla ilikua 4,500,000
Ukijumlisha na hii ya uvunaji 1,000,000 jumla kuu ya GHARAMA ZOTE INAKUA 5,500,000
MAVUNO
Nimepata jumla ya gunia 92..........wastani wa gunia 4.6 kwa eka
Kwa sasa gunia la alizeti linauzwa 90,000(i hope litafika 150,000)
Nikisema niuze sasa maana yake ni
90,000 x 92 = 8,280,000
Kukokotoa Faida/hasara
Mauzo. 8,280,000
Gharama 5,500,000
8,280,000-5,500,000 = 2,780,000 FAIDA
Kwa sasa sina mpango wa kuuza alizeti wala kukamua
Nitaiweka stock hadi itakapo adimika bei itakua nzuri na mashudu yatakua bei juu pia
Kwa muda huu naanza kununua rasmi alizeti angalau gunia zingine 250 au 300 ili bajeti yangu ya 40m isogogee kidogo, kisha nitakuja kukamua na kuuza mafuta......nimekamua gunia moja nimepata lita 20 na point
Dengu nimeshindwa kulima sababu ya nvua mbuga imekauka sana
Namshukuru sana MUNGU na wote mlionipa moyo na hata walio nikatisha tamaa kwani walinipa chachu zaidi
Kikubwa nilicho jifunza kwenye kilimo ni usiwe mbahili kwenye mambo ya kitaalamu....... fuata exactly wataalam wanavyo shauri haswa kwenye
Muda wa kulima mapema
Kupanda kwa kanuni
Kupalilia kwa wakati
Uvunaji kuzuia kupoteza mazao mengi on process
Na mwisho simamia mwenye kila hatua
Kwa muda niliotumia na faida iliopo hadi sasa sio kubwa lakini kwangu mimi ni USHINDI mkubwa sana kwa maana ya UZOEFU
(Iwapo bei itafika 150,000 kama msimu uliopita basi nategemea kuuza 11m faida itakuja 5.5 sio mbaya)
Changamoto kubwa niliokutana nayo so far ni mvua kuondoka MAPEMA haswa kwenye eka nilizo lima mwishoni, vinginevyo ningepata hata wastani wa gunia 5-7 kwa eka
Next season nitarudi nikiwa na nguvu zaidi na ari zaidi
Ukwaju
Hicho ndi kilimo
Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app