Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
tunataka waliovuna watupe mrmrejesho, mbona wanakula Kona na mwezi huu NI Mei mashamba yote ya ukanda wa kati wanavuna Sasa
watushushie hesabu zao km sio za daftarini za matikikiti maji
Mkuu alizeti gunia haitoi dumu mbili... ikitoa sana dumu moja tu na kicheleWakuu,
Binafsi huwa na Bet sana na bahati nzuri nimemuotea muhindi kama M 40
Na sasa nataka kubet kwenye kilimo
Mwaka huu naingia shambani kweli kweli sio utani, naingia FRONT na sio simu
Nakwenda kulima ekari 50 za alizeti MBUGANI kisha nikitoa naweka dengu
Eneo SINGIDA kwetu kabisa
Matumizi (makadirio ya juu kabisa) kwa ekari 50
[emoji117]Kukodi shamba m 2.5
[emoji117]Kulima shamba m 2.5
[emoji117]Kupanda m 1
[emoji117]Kupalilia shamba m 2.5
[emoji117]Mbegu lk 7
[emoji117]Uvunaji/upakiaji m 2
[emoji117]Mengineyo m 2
Jumla milion 13.2
Jumlisha hidden cost jumla iwe milioni 15
MAVUNO (makadirio ya chini)
Eka moja gunia 7 badala ya 15 za wataalamu
Ekari50 x Gunia 7
Jumla inakua gunia 350
Wastani gunia moja hutoa mafuta dumu 2 bei makadirio ya chini sh elf 50 kwa dumu( dumu linakwenda hadi laki+)
350 x 2 inakua dumu 700
Dumu700 x elf50 unapata Sh M35
Hapo nime assume mashudu yamelipia gharama ya ukanuaji
JUMUISHO
M35 -M15 = M20 Faida
DENGU
Ukitoa tu alizeti unavizia nvua za mwishoni kabisa unalima dengu shamba hilo hilo hulipi gharama za kukodi tena
[emoji117]Kulima m 2.5
[emoji117]Mbegu m 2
[emoji117]Kupanda lk 5
[emoji117]Madawa (emergency) m2
[emoji117]Kuvuna/kupakia 2m
[emoji117]Mengineyo m 1
Jumla m 10
Hidden cost m 2
Jumla m 12
MAUZO
Wastani gunia 4 kwa eka badala ya gunia 8 hadi 10 kwa eka za wataalamu
Ekari50 x Gunia 4 unapata gunia 200
Gunia la dengu lina wastani wa sh Laki 1
Laki 1 x gunia 200 unapata M 20
JUMUISHO
M20 - M12 = M8 Faida
FAIDA KUU (alizeti na dengu)
M20 +M8 = M28
NB
Nimeweka makadirio ya juu sana kwenye matumizi
Na nikaweka makadirio ya chini sana kwenye mavuno na bei
Dua zenu jamani
Ntaleta MREJESHO iwe nime Lost au nime Win
MREJESHO 24/03/2022
Wakuu kwema
So far mkeka wangu wa kilimo cha Alizeti unakwenda vizuri sana baada ya zile ODDS kubwa na ngumu kutick
ODDS ngumu kabisa zilikua ni MVUA na PALIZI
SHAMBA EKARI 20
Mpaka sasa nimelima ekari 20 tu...... hii ni baada ya wadau mbali mbali kushauri ekari 50 is too risk ikiwa huna UZOEFU na ikizingatiwa mamlaka ya hali ya hewa ilitabiri mvua zitakua chache
MBEGU (ASA)
Baada ya mchakato wa kitaalamu nikashauriwa nitumie mbegu za Serikali ASA na nilinunua mfuko wa kilo 2 kwa sh 5,000 tu, nilipata mchongo huu kwakuwa nilinunua kwa wingi
Sijatumia MBOLEA yoyote wala sijatumia viatilifu vyovyote kwasababu nimelima MBUGANI aridhi imeshiba na Alizeti haishambuliwi sana na magonjwa
Leo hii nimemalizana na PALIZI na mimea inakwenda vizuri kwa sehemu kubwa
Mpaka sasa SIJAKUTANA na gharama yoyote ambayo imenishtua kwa maana ya kwamba labda ni gharama ambayo sikuifikiria au gharama kuwa kubwa zaidi ya nilivyo KADIRIA
Zaidi mbegu imenipa UNAFUU mkubwa sana, nilipanga kutumia Hysuan Kg 2 kwa 35,000
Lakini nimetumia ASA Kg 2 kwa sha 5,000 na nilinunua mifuko ya Kg2 mifuko 80, yaani eka moja kwa mifuko 4, hapo nime save karibu 2m...... Naishukuru sana serikali kwa hili [emoji120][emoji120]
Ingawaje sijajua ubora wake baada ya mavuno
Ntaleta tena Mrejesho baada ya KUVUNA
MREJESHO WA GHARAMA
Shamba ekari 20
20 x 30,00 = 600,00
Shamba lilikua safii
Kulima
20 x 40,000 = 800,000
Mbegu (ASA)
80 x 5,000 = 400,000
Kupanda
20 x 30,000 = 600,000
Palizi
20 x 50,000 = 1,000,000
Mengineyo
1,000,000
Jumla kuu 4,500,000
Hadi sasa nimelaza shambani 4.5M
Bado gharama za kuvuna kupepeta na kuhifadhi
MREJESHO
kuna kama eka nne na nusu nililima mwishoni naona zimepelea mvua maana mvua ndio imeindoka haijarudi na alizeti ndio inaanza kufunga maua
View attachment 2203797
Ngoja avune kwanza kaka ili siku akikamua ajione hali halisiMkuu alizeti gunia haitoi dumu mbili... ikitoa sana dumu moja tu na kichele
Kaandika el tatu halafu akaweka koma baada ya 30...yani 30,00....sa hyo ni sh ngap hapo..mb
mbona pame andikwa 30,000 wewe efu 3 hiyo ume itoa wapi maana hata hesabu yenyew ya jumla ame kuandikia 600,000
Dada yangu nipitishie, mm nimeshavuna, bado eneo moja nitaenda May mwishoni, eka 15 za mwanzo nimepatwa gunia 18 nyingine imebaki shambani wataivuna baadaeMwenyekiti wa observers
Maendeleo ni mazuri
Mimi sijavuna sababu ya mvua
Ila soon navulbaar nakupitishia mafuta hapo.
Yaani inatakiwa usimamie na hizo walizookota ilitakiwa uzikusanye na udongo wake alafu uwape watu wengine Kazi ya kupeta.Dada yangu nipitishie, mm nimeshavuna, bado eneo moja nitaenda May mwishoni, eka 15 za mwanzo nimepatwa gunia 18 nyingine imebaki shambani wataivuna baadae
Walichoniudhi wananishauri niiuze kila gunia 90,000/ na kuna walanguzi kibao wanasarandia
Ila imenikata NI wastani wa gunia moja na nusu kwa eka, pia upepetaji mbaya, wamedondosha Sana Alizeti ambapo huenda nilipoondoka waliirudia
Ukweli ndio huo nimepigwa ngoja nisikie wenzangu km wanapaita guni 18 kwa eka HICHO NDIO NAKATAA
Dada yangu nipitishie, mm nimeshavuna, bado eneo moja nitaenda May mwishoni, eka 15 za mwanzo nimepatwa gunia 18 nyingine imebaki shambani wataivuna baadae
Walichoniudhi wananishauri niiuze kila gunia 90,000/ na kuna walanguzi kibao wanasarandia
Ila imenikata NI wastani wa gunia moja na nusu kwa eka, pia upepetaji mbaya, wamedondosha Sana Alizeti ambapo huenda nilipoondoka waliirudia
Ukweli ndio huo nimepigwa ngoja nisikie wenzangu km wanapaita guni 18 kwa eka HICHO NDIO NAKATAA
Wliniambia wana Duka la prmbejeo hapo kijijini na mbegu ilikuwa Record kilo moja 8,000/ hapo ndipo nilpoanza kupingwa, Kuna ingine kilo 40,000/ ISAN ipo ya KenyaUlipanda mbegu gani?
Kwa nini usikoboe ukauza mafuta?
Lita tano ni 32,000
Wliniambia wana Duka la prmbejeo hapo kijijini na mbegu ilikuwa Record kilo moja 8,000/ hapo ndipo nilpoanza kupingwa, Kuna ingine kilo 40,000/ ISAN ipo ya Kenya
Nasubiri wenzangu humu JF wapepete
Dada yangu nipitishie, mm nimeshavuna, bado eneo moja nitaenda May mwishoni, eka 15 za mwanzo nimepatwa gunia 18 nyingine imebaki shambani wataivuna baadae
Walichoniudhi wananishauri niiuze kila gunia 90,000/ na kuna walanguzi kibao wanasarandia
Ila imenikata NI wastani wa gunia moja na nusu kwa eka, pia upepetaji mbaya, wamedondosha Sana Alizeti ambapo huenda nilipoondoka waliirudia
Ukweli ndio huo nimepigwa ngoja nisikie wenzangu km wanapaita guni 18 kwa eka HICHO NDIO NAKATAA
Mleta mada kama uko serious njoo pm nna shamba Simanjiro ekari 15,000 nina ma trekta mawili. Mwaka jana nilianza Na ekari 100 za maharage tu. Mwaka huu nataka kuongeza mahindi, alizeti Na katarm. Njoo tuunganishe nguvu.
Inakubali na inalimwa sana Sumbawanga na chunya ata juzi nmetoka kuchukua mzigo sumbawangaMkuu vipi kilimo cha alizeti Kwa mikoa yenye mvuà nyingi kama nyanda za juu kusini ....je inastawi vizuri na mavuno yanakuaje?
Shukran mkuu......Namalizia kukusanya taarifa za kutosha ,kuanalyse .....nataka panapo majaaliwa next season nijitose mkuu...Inakubali na inalimwa sana Sumbawanga na chunya ata juzi nmetoka kuchukua mzigo sumbawanga
View attachment 2226759
Mavuno yameanza
Vipi una mashine ya kukamua pia au unalima tu
Mchango wako ni muhimu kwangu
KILA MTU AKIFIKIRIA KUNUNUA NA KUUZA NANI ATALIMA SASA ??Usilime..kanunue...nakutaadhalisha tu.
#MaendeleoHayanaChama