Naingia Shambani very serious kulima Alizeti

Naingia Shambani very serious kulima Alizeti

tunataka waliovuna watupe mrmrejesho, mbona wanakula Kona na mwezi huu NI Mei mashamba yote ya ukanda wa kati wanavuna Sasa
watushushie hesabu zao km sio za daftarini za matikikiti maji

Mwenyekiti wa observers
Maendeleo ni mazuri

Mimi sijavuna sababu ya mvua

Ila soon navulbaar nakupitishia mafuta hapo.
 
Wakuu,

Binafsi huwa na Bet sana na bahati nzuri nimemuotea muhindi kama M 40

Na sasa nataka kubet kwenye kilimo

Mwaka huu naingia shambani kweli kweli sio utani, naingia FRONT na sio simu

Nakwenda kulima ekari 50 za alizeti MBUGANI kisha nikitoa naweka dengu

Eneo SINGIDA kwetu kabisa

Matumizi (makadirio ya juu kabisa) kwa ekari 50

[emoji117]Kukodi shamba m 2.5
[emoji117]Kulima shamba m 2.5
[emoji117]Kupanda m 1
[emoji117]Kupalilia shamba m 2.5
[emoji117]Mbegu lk 7
[emoji117]Uvunaji/upakiaji m 2
[emoji117]Mengineyo m 2

Jumla milion 13.2
Jumlisha hidden cost jumla iwe milioni 15

MAVUNO (makadirio ya chini)

Eka moja gunia 7 badala ya 15 za wataalamu
Ekari50 x Gunia 7
Jumla inakua gunia 350

Wastani gunia moja hutoa mafuta dumu 2 bei makadirio ya chini sh elf 50 kwa dumu( dumu linakwenda hadi laki+)

350 x 2 inakua dumu 700
Dumu700 x elf50 unapata Sh M35
Hapo nime assume mashudu yamelipia gharama ya ukanuaji

JUMUISHO
M35 -M15 = M20 Faida

DENGU

Ukitoa tu alizeti unavizia nvua za mwishoni kabisa unalima dengu shamba hilo hilo hulipi gharama za kukodi tena

[emoji117]Kulima m 2.5
[emoji117]Mbegu m 2
[emoji117]Kupanda lk 5
[emoji117]Madawa (emergency) m2
[emoji117]Kuvuna/kupakia 2m
[emoji117]Mengineyo m 1
Jumla m 10
Hidden cost m 2
Jumla m 12

MAUZO
Wastani gunia 4 kwa eka badala ya gunia 8 hadi 10 kwa eka za wataalamu

Ekari50 x Gunia 4 unapata gunia 200
Gunia la dengu lina wastani wa sh Laki 1

Laki 1 x gunia 200 unapata M 20

JUMUISHO
M20 - M12 = M8 Faida

FAIDA KUU (alizeti na dengu)
M20 +M8 = M28

NB
Nimeweka makadirio ya juu sana kwenye matumizi

Na nikaweka makadirio ya chini sana kwenye mavuno na bei

Dua zenu jamani

Ntaleta MREJESHO iwe nime Lost au nime Win

MREJESHO 24/03/2022

Wakuu kwema
So far mkeka wangu wa kilimo cha Alizeti unakwenda vizuri sana baada ya zile ODDS kubwa na ngumu kutick
ODDS ngumu kabisa zilikua ni MVUA na PALIZI

SHAMBA EKARI 20
Mpaka sasa nimelima ekari 20 tu...... hii ni baada ya wadau mbali mbali kushauri ekari 50 is too risk ikiwa huna UZOEFU na ikizingatiwa mamlaka ya hali ya hewa ilitabiri mvua zitakua chache

MBEGU (ASA)
Baada ya mchakato wa kitaalamu nikashauriwa nitumie mbegu za Serikali ASA na nilinunua mfuko wa kilo 2 kwa sh 5,000 tu, nilipata mchongo huu kwakuwa nilinunua kwa wingi

Sijatumia MBOLEA yoyote wala sijatumia viatilifu vyovyote kwasababu nimelima MBUGANI aridhi imeshiba na Alizeti haishambuliwi sana na magonjwa

Leo hii nimemalizana na PALIZI na mimea inakwenda vizuri kwa sehemu kubwa

Mpaka sasa SIJAKUTANA na gharama yoyote ambayo imenishtua kwa maana ya kwamba labda ni gharama ambayo sikuifikiria au gharama kuwa kubwa zaidi ya nilivyo KADIRIA
Zaidi mbegu imenipa UNAFUU mkubwa sana, nilipanga kutumia Hysuan Kg 2 kwa 35,000
Lakini nimetumia ASA Kg 2 kwa sha 5,000 na nilinunua mifuko ya Kg2 mifuko 80, yaani eka moja kwa mifuko 4, hapo nime save karibu 2m...... Naishukuru sana serikali kwa hili [emoji120][emoji120]
Ingawaje sijajua ubora wake baada ya mavuno

Ntaleta tena Mrejesho baada ya KUVUNA

MREJESHO WA GHARAMA

Shamba ekari 20
20 x 30,00 = 600,00
Shamba lilikua safii

Kulima
20 x 40,000 = 800,000

Mbegu (ASA)
80 x 5,000 = 400,000

Kupanda
20 x 30,000 = 600,000

Palizi
20 x 50,000 = 1,000,000

Mengineyo
1,000,000

Jumla kuu 4,500,000

Hadi sasa nimelaza shambani 4.5M
Bado gharama za kuvuna kupepeta na kuhifadhi

MREJESHO
kuna kama eka nne na nusu nililima mwishoni naona zimepelea mvua maana mvua ndio imeindoka haijarudi na alizeti ndio inaanza kufunga maua

View attachment 2203797
Mkuu alizeti gunia haitoi dumu mbili... ikitoa sana dumu moja tu na kichele
 
mb

mbona pame andikwa 30,000 wewe efu 3 hiyo ume itoa wapi maana hata hesabu yenyew ya jumla ame kuandikia 600,000
Kaandika el tatu halafu akaweka koma baada ya 30...yani 30,00....sa hyo ni sh ngap hapo..
 
Mwenyekiti wa observers
Maendeleo ni mazuri

Mimi sijavuna sababu ya mvua

Ila soon navulbaar nakupitishia mafuta hapo.
Dada yangu nipitishie, mm nimeshavuna, bado eneo moja nitaenda May mwishoni, eka 15 za mwanzo nimepatwa gunia 18 nyingine imebaki shambani wataivuna baadae
Walichoniudhi wananishauri niiuze kila gunia 90,000/ na kuna walanguzi kibao wanasarandia
Ila imenikata NI wastani wa gunia moja na nusu kwa eka, pia upepetaji mbaya, wamedondosha Sana Alizeti ambapo huenda nilipoondoka waliirudia
Ukweli ndio huo nimepigwa ngoja nisikie wenzangu km wanapaita guni 18 kwa eka HICHO NDIO NAKATAA
 
Yaani inatakiwa usimamie na hizo walizookota ilitakiwa uzikusanye na udongo wake alafu uwape watu wengine Kazi ya kupeta.
 
Dada yangu nipitishie, mm nimeshavuna, bado eneo moja nitaenda May mwishoni, eka 15 za mwanzo nimepatwa gunia 18 nyingine imebaki shambani wataivuna baadae
Walichoniudhi wananishauri niiuze kila gunia 90,000/ na kuna walanguzi kibao wanasarandia
Ila imenikata NI wastani wa gunia moja na nusu kwa eka, pia upepetaji mbaya, wamedondosha Sana Alizeti ambapo huenda nilipoondoka waliirudia
Ukweli ndio huo nimepigwa ngoja nisikie wenzangu km wanapaita guni 18 kwa eka HICHO NDIO NAKATAA

Ulipanda mbegu gani?

Kwa nini usikoboe ukauza mafuta?

Lita tano ni 32,000
 
Ulipanda mbegu gani?

Kwa nini usikoboe ukauza mafuta?

Lita tano ni 32,000
Wliniambia wana Duka la prmbejeo hapo kijijini na mbegu ilikuwa Record kilo moja 8,000/ hapo ndipo nilpoanza kupingwa, Kuna ingine kilo 40,000/ ISAN ipo ya Kenya
Nasubiri wenzangu humu JF wapepete
 
Wliniambia wana Duka la prmbejeo hapo kijijini na mbegu ilikuwa Record kilo moja 8,000/ hapo ndipo nilpoanza kupingwa, Kuna ingine kilo 40,000/ ISAN ipo ya Kenya
Nasubiri wenzangu humu JF wapepete

Oooh zile za serikali

Mi nimepanda zote

Nilinganishe matokeo
 
Dada yangu nipitishie, mm nimeshavuna, bado eneo moja nitaenda May mwishoni, eka 15 za mwanzo nimepatwa gunia 18 nyingine imebaki shambani wataivuna baadae
Walichoniudhi wananishauri niiuze kila gunia 90,000/ na kuna walanguzi kibao wanasarandia
Ila imenikata NI wastani wa gunia moja na nusu kwa eka, pia upepetaji mbaya, wamedondosha Sana Alizeti ambapo huenda nilipoondoka waliirudia
Ukweli ndio huo nimepigwa ngoja nisikie wenzangu km wanapaita guni 18 kwa eka HICHO NDIO NAKATAA

Gunia 18 HAIPO hiyo mkuu
Ndio maana kwenye makadirio yangu nimeweka gunia 4 tu

Hapo kamua mafuta na uweke stoo mafuta angalau utarudisha gharama
Ukiuza alizeti itakukata
Wastani wa gunia moja na nusu per ekari sio mzuri

Mwezi huu navuna yangu
 
Mleta mada kama uko serious njoo pm nna shamba Simanjiro ekari 15,000 nina ma trekta mawili. Mwaka jana nilianza Na ekari 100 za maharage tu. Mwaka huu nataka kuongeza mahindi, alizeti Na katarm. Njoo tuunganishe nguvu.

fisi 2 nakutafuta.
Nichek inbox tuyajenge
 
4c1353f1-7599-405d-b6ae-f74182e5b0f8.jpg

Mavuno yameanza
 
Mkuu vipi kilimo cha alizeti Kwa mikoa yenye mvuà nyingi kama nyanda za juu kusini ....je inastawi vizuri na mavuno yanakuaje?
Inakubali na inalimwa sana Sumbawanga na chunya ata juzi nmetoka kuchukua mzigo sumbawanga
 
Back
Top Bottom