Naingiza milion 22 kwa mwezi kwa biashara ya kuuza Mapapai shambani

Naingiza milion 22 kwa mwezi kwa biashara ya kuuza Mapapai shambani

Kilimo cha mitandaoni hicho.
Kilimo halisi huwezi kuuza papai likiwa shambani kwa 1500/- labda shamba lako lipo pale Sokoni Kisutu au Ilala au Kariakoo au Mabibo.
Mimi nilipanda mipapai miche 700 mbegu ya kisasa Malikia F1. Naongea nikiwa na uzoefu.
We unauza papai shambani bei gan
Maana mapapai nauza shambani buku mpaka buku jero na namaliza
Labda yako unauza kipindi cha mvua ndio bei ndogo
 
Kilimo cha mitandaoni hicho.
Kilimo halisi huwezi kuuza papai likiwa shambani kwa 1500/- labda shamba lako lipo pale Sokoni Kisutu au Ilala au Kariakoo au Mabibo.
Mimi nilipanda mipapai miche 700 mbegu ya kisasa Malikia F1. Naongea nikiwa na uzoefu.
Tumia mbegu za kwetu sio za ulaya unafeli ndio maana hauuzi
 
Hiyo bei jumla ukifikisha sokoni tena mbegu ya kisasa papai kubwa sana na siyo msimu wa papai nyingi za kienyeji.
Kiangazi kikuu ukitoa papai kubwa Sana utauza 1500 hadi 2000 bei ya jumla ukifika sokoni kwa dalali.
Hapo bado dalali hajakusokota, pia kuna ushuru, usafiri na ulinzi.
Papai kubwa linauzwa 3000
We kwan unauzia wap papai zako
 
Haya kama mlivyosoma ni kweli

Hakuna biashara ina hela kama mapapai

Na hakuna biashara rahisi kama papai

Papai moja shamba linauzwa tsh 1500 moja
Mtaani wanauza tsh 3000 moja

Kilimo chake rahisi sana ila usilime wakati wa mvua, papai inataka maji kidogo tu kwa siku

Mbolea sio sana mche wa papai tsh 3000 mmoja

Sasa endelea kusema maisha magumu, nimekaa pale youtube uje nakufundisha kupata hela
Pole bro
 
Kitu kingine gharama za umwagiliaji siyo ndogo, Mbolea ya samadi yakutosha muhimu.
Ukiweza vitu hivyo viwili utavuna papai la pesa utafurahia kilimo.
We ni mshamba na mwongo asee
Papai haitaki maji kabisaaaa wala mbolea nyingi
Dah we jamaan we kwan unapanda nyanya,
 
Muda WA wewe kuwa na hela umefika ndio maana kilichokutoa unahisi pekee kiko sahihi Ila nikikwambia kuna watu wamepoteza pesa zao Kwa haya haya mapapai unaweza shangaa! All in all hongera Kwa ushuhuda mzuri
Kizuri kula na wenzio boss
Acha kulia lia
 
Back
Top Bottom