Naiomba timu yangu ya Simba Sports Club impe nafasi ya mwisho Ibrahim Ajibu Migomba, bado ana mchango mkubwa

Naiomba timu yangu ya Simba Sports Club impe nafasi ya mwisho Ibrahim Ajibu Migomba, bado ana mchango mkubwa

Ingawa ni kweli Ajibu ana matatizo yake Ila alicho ongea sahihi kabisa
Ulaya wanaenda ma engineer hata waandishi wa habari..
Skysports Wana Melissa Red katokea South Africa....

Hoja yake ina mashiko wala sio dharau...kama tunataka yeye aende Ulaya Kwa mpira ...Sisi wengine je taaluma zetu zinatupeleka wapi...
Mimi ni Daktari. Nipo huko unakodai ni peak.

Unachopaswa kufahamu ni kuwa, kuna fani ambazo hazina ulazima wa kudhihirika ubora wa fani yako. Mfano Mwl wa Kiswahili, aende wapi kama si kubaki nchini?

Lakini, hasemi kwa nia njema ya kumotivate bali kwa nia ya kukejeli. Unaulizwa swali kiungwana, unajibu kwa kubwabwaja. Ni sahihi?

Ndiyo hiyo 'ego'. Udhaifu wa mwingine usikufanye wewe kujiona kwamba unachokiendea ni sahihi.
 
Kuna walimu wa kiswahili pia nje ya nchi....
 
Kuna walimu wa kiswahili pia nje ya nchi....
Je, huko nje ndo peak ya Kiswahili? Hapana.

Tanzania ndiyo kilele cha mafanikio ya lugha ya Kiswahili. Ukitaka kujijua wewe ni Mwalimu bobezi toka huko nchini kwako nenda Tanzania. Ukitoboa, haswa tutasema unaiweza.

By the way, what I was trying to clarify ni hiyo ego ya huyo dogo.
 
Timu zote zimkatae? Simba alishindwa, Azam kashindwa, Singida pia kadorora.

Kinachomtesa huyo dogo ni ego. Nilipata kusikia interview yake moja. Wanamuuliza 'kila mtu alitegemea uende Ulaya kucheza mpira, kwa kiwango hiki unadhani utaweza kwenda?'.

Dogo kwa jeuri, anajibu 'siyo lazima mimi niende. Hata wao wanaweza kwenda'. Na wala hajali.

Mpira si kipaji tu. Mpira unahitaji nidhamu na juhudi. Kuna wachezaji wana vipaji vya kawaida sana, lakini wanakiwasha kila leo. Si kwa sababu ya vipaji vyao, ila kwa sababu ya nidhamu na kuheshimu majukumu yao.

Huyo dogo hapana. Anaweza kwenda IHEFU huko akadeke. Simba kwa sasa hatuihitaji wachezaji wa aina yake.

Kama wewe ndiye Ajib mwenyewe, nakuasa kama mdogo wangu, badilika. Acha uswahili, ongeza juhudi. Achana na maneno wanayokujaza kuwa wewe ni fundi. Ufundi wako pekee uonekane kwenye pitch, si midomoni kwa machawa wako.

Una nafasi ya kubadilika na kuwika kwa mara nyingine. Zingatia nidhamu na mazoezi kwa sana.

Nakutakia kila la kheri.
Kwenye ile interview alijibu fasaha sana, wee ulitaka ajibu vipii??
 
Ni mchezaji WA kawaida Sana. Anazidiwa na wachezaji wengi WA kitanzania. Bongo huwa tunatabia ya kusifia tu vipaji uchwara ni kama Haruna Moshi Boban alikuwa anasifiwa sijui anakipaji wakati kawaida Sana.
Boban yupi unamzungumzia wee? Hebu mpe heshima yake.
 
Mbona Morison mlishindwa kumlaani zaidi ya kukimbilia CAS na kuangukia pua
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] na leo anawachezesha kibwebwe huko yanga, yaan anawaburuza atakavyooo [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ingawa ni kweli Ajibu ana matatizo yake Ila alicho ongea sahihi kabisa
Ulaya wanaenda ma engineer hata waandishi wa habari..
Skysports Wana Melissa Red katokea South Africa....

Hoja yake ina mashiko wala sio dharau...kama tunataka yeye aende Ulaya Kwa mpira ...Sisi wengine je taaluma zetu zinatupeleka wapi...
Bora usemee wee, ajibu alijibu vizuri kabisaa
 
Mm nimeanza kwenda uwanjani kuiangalia Simba mwaka 1988, enzi hizo kuna Nyota Nyekundu ya akina Roster Ndunguru, faustine kibingwa, Abbas Kuka, Mohamed Mgalike, kulikuwa na Pilsner ya akina Said Mrisho, Idd Msigala, nk.

Simba ile ya Sunday Juma, Aston Pardon, kipa Mosses Mkandawile, Adam seleman, Juma Limonga, nikisema niwataje wote nitawachosha.

Kuna mchezaji kila siku namuota, sio mwingine ni Ibrahim Ajib, naiomba klabu yangu huyu mchezaji alikuwa katika kiwango kikubwa sana akiwa Yanga, Simba tukamrudisha lkn akakutana na changamoto na matokeo yake Chama akawa anamweka benchi, akavunja mkataba na kwenda Azam, baadae Singida, nahisi ss hv hata huko Singida ameshaachana nao.

Ibrahim Ajib bado ana uwezo mkubwa sana, Ajib anaipenda Simba, bado ana mchango mkubwa sana.

Nakuomba Try again, katika wachezaji wazawa muiteni Ajib mkae nae, huyo fundi bado ana kipaji sana, tutapoteza hazina hiyo.

Nina uhakika Ajib kwa kocha huyu mbrazil hawezi kosa namba.Ninaomba Ajib aitwe mazoezini kocha amuangalie na atoe tathmini kuhusu kiungo huyo ambaye wengi sio tu tunampenda bali pia tunamkubali.

Msinipuuze viongozi.Please
Mbona hii kama ID mpya ya popoma
 
Mchezaji mvivu, hana nidhamu ya mazoezi.. akacheze kwingine.
 
Back
Top Bottom