Naiona ile Spirit ya 1995 ikirejea kwa kasi, CHADEMA na Chama kipya vitapata Wabunge wengi lakini CCM itashinda Urais. PM atatoka Upinzani

HATOGOMBEA.

Bila tume HURU ya UCHAGUZI na KATIBA mpya,hapatafanyika uchaguzi wowote wa HAKI.
Fikra hizi ndizo zinazotakiwa kuondolewa akilini mwa waTanzania, na hasa vyama vya upinzani.

Huku ni kukubali kuwa uhalifu unalipa. Uvunjaji wa sheria unazawadiwa.

CCM wanafanya uhalifu kwa sababu wananchi wanawaruhusu kufanya hivyo. Wananchi wakikataa, CCM hawana njia yoyote ya kung'ang'aniza ushindi usiokuwa halali.

Hakuna chombo chochote cha "Dola" kilicho tayari kushiriki kuwahujumu wananchi wa nch hii. Hawawezi kukubali kutumiwa na CCM kufanya uhalifu dhidi ya wananchi.

Ndiyo maana tunasisitiza CHADEMA waweke mkazo zaidi kufanya kazi na wananchi na kuwaelimisha ili wazuie uhalifu unaofanywa na CCM.

Kwa hiyo mkuu 'Rabbon', pamoja na kutambua hili la umuhimu wa Tume Huru ya uchaguzi na uwepo wa Katiba Mpya (jambo lisilowezekana sasa kwa muda huu uliopo), msisitizo wangu ni kwa CHADEMA na wengineo kutilia mkazo kutambua aina ya uhalifu ufanywao na CCM nyakati za uchaguzi. Wakishazitambua njia zote muhimu zitumikazo, kazi inageukia katika kutafuta ufumbuzi, njia za kuzuia uhalifu.

Swala la kutoshiriki uchaguzi, hilo sahau kabisa. CCM wanalipenda sana wazo hilo.
 
Chama cha mambuzi kimeshindwa kutatua kero za raia kimejikita katika ujambazi wa rasilimali na ulafi wa madaraka ni aibu mno kuwa mwana CCM sasa kuliko kipindi chochote. 🀣
 
Mkuu ccm wana mbinu 36 za kuiba uchaguzi, mpk leo wametumia mbinu 6 tu. Hebu fikiria wakizitumia hizo mbinu 30 mwaka 2025 upinzani utatoboa?

Ili kuifikia ndoto ulionayo katiba mpya na bora yapaswa kuandikwa.
Kumbe ni Wezi?
 
Huu ujinga atutaruhusu, CCM itoke haraka
 
CCM inaenda kufa
 
Mkuu ccm wana mbinu 36 za kuiba uchaguzi, mpk leo wametumia mbinu 6 tu. Hebu fikiria wakizitumia hizo mbinu 30 mwaka 2025 upinzani utatoboa?

Ili kuifikia ndoto ulionayo katiba mpya na bora yapaswa kuandikwa.
kinacho nishangaza ni hicho. MAJAMBAZI KUJIGAMBA KWAMBA MNA MBINU ZA KUIBA UCHAGUZI. Pumbavu kabisa. Your days are numbered.
 
Samia hawezi kushinda 2025 (kwa uchaguzi huru na haki). Naye amejua ndiyo maana ameamua aingie kwenye uchaguzi na katiba chakavu ili ijaribu kumbeba. Maadui wa samia wameweza kumfarakanisha samia na wananchi. Ngoja nitoe mifano. 1. Wameweza kumchafua (amejichafua) suala la kuuzwa bandari. 2. Wameweza kueleza kwamba kikwete anatawala kwa mgongo wa samia. 3. Ndani ya ccm hakupo sawa pia. Timu samia vs timu magufuli. 4. Vikwazo vya uzanzibar. 5. Vikwazo vya jinsia. (hapo hadi wanawake wamesika wakisema "toka lini mwanamke akawa raisi?" nikagundua adui wa mwanamke ni mwanamke. 6. 7...
 
Kwa utabiri wako huu unaonekana bado sana kuzijua siasa za Tanzania. Tusubiri Oktoba, 2025.
 
Upo uwezekano wa kufanya marekebisho katika Katiba hii Ili kuruhusu kuundwa Tume huru ya Uchaguzi.

CDM kupitia Mnyika , pia Mwamakula wamependekeza vifungu kadhaa kwenye Katiba hii vibadilishwe Ili tuingie uchaguzi na Tume huru,

Wakikataa kurekebisha, tunadai Kwa maandamano ya Amani.

Hakuna kususia.
 
Hakuna kitu kama hicho. Never.
1.CCM ni kama ANC, ZANU PF, MPLA. CCM siyo kama UNIP, MPC au KANU.
2. CCM ina uwezo wa kula matapishi yake. Yaani CCM can undergo self initiated(sponteneous) mutation, changes. Wanaweza kumuondoa anayeweza kusababisha wao kukosa kura hata kama ni muhimu kwao au mkubwa ndani yao kiasi gani.
3.CCM siyo chama cha siasa 100% kwa hapa Tanzania. CCM ni mfumo wa utawala na uongozi Tanzania, siku hizi mnaita Chama Dola. Yaani kila watu muhimu ndani ya mfumo ni either makada, wanachama wa kawaida au affliated na CCM.
4. Tanzania is less urbanised. Raia wengi wa Tanzania wapo vijijini. They are less concerned na aina ya chama cha siasa. Na kama kujua kidogo, basi wanaijua CCM kutokana na sababu za kihistoria.
5. Udhaifu wa ndani wa chama kikuu cha upinzani hapa Tanzania yaani CHADEMA. Majority share holders wa CHADEMA wameshindwa kuachia shares ili zimilikiwe na umma kwa maslahi mapana ya Taifa na chama. Wanahofia wakiachia shares, basi chama kitakufa. Hapo watachomokaje?
6. Mapambano ya kinga njaa ndani ya vyama vingine yanapewa umuhimu kuliko sera, siasa na matamanio ya kushika dola/madaraka.
 
Namba 6 nimeielewa Sana πŸ˜‚πŸ”₯
 
Upuuzi,kwamba hao ropo ropo wanaweza Waziri ccm wabunge? Ina uhakika?

Jimbo lenyewe la Nkasi Kwa mbunge wao anaweza asishinde Kwa sababu waliompotisha ni Wana ccm kimkomoa Kessy na Magufuli,yule aliyeongoza kura za maoni anarejea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…