Hakuna kitu kama hicho. Never.
1.CCM ni kama ANC, ZANU PF, MPLA. CCM siyo kama UNIP, MPC au KANU.
2. CCM ina uwezo wa kula matapishi yake. Yaani CCM can undergo self initiated(sponteneous) mutation, changes. Wanaweza kumuondoa anayeweza kusababisha wao kukosa kura hata kama ni muhimu kwao au mkubwa ndani yao kiasi gani.
3.CCM siyo chama cha siasa 100% kwa hapa Tanzania. CCM ni mfumo wa utawala na uongozi Tanzania, siku hizi mnaita Chama Dola. Yaani kila watu muhimu ndani ya mfumo ni either makada, wanachama wa kawaida au affliated na CCM.
4. Tanzania is less urbanised. Raia wengi wa Tanzania wapo vijijini. They are less concerned na aina ya chama cha siasa. Na kama kujua kidogo, basi wanaijua CCM kutokana na sababu za kihistoria.
5. Udhaifu wa ndani wa chama kikuu cha upinzani hapa Tanzania yaani CHADEMA. Majority share holders wa CHADEMA wameshindwa kuachia shares ili zimilikiwe na umma kwa maslahi mapana ya Taifa na chama. Wanahofia wakiachia shares, basi chama kitakufa. Hapo watachomokaje?
6. Mapambano ya kinga njaa ndani ya vyama vingine yanapewa umuhimu kuliko sera, siasa na matamanio ya kushika dola/madaraka.
Mkuu 'Midimay', unastahili heshima kwa mawazo uliyoweka hapa. Ni mawazo yaliyotumia fikra makini.
Mimi sikubaliani na baadhi ya hayo mawazo.
CCM kwa sasa ni debe tupu kabisa linalosubiri kutobolewa, kwa sababu limekwishadhoofishwa na kutu ndani kwa ndani.
Ni watu wachache sana humo ndani ya chama hicho sasa hivi unaoweza kuwategemea kwa mengi uliyoeleza wewe; mmoja ni huyo Kinana, sina mfano mwingine tena.
Ninakubaliana nawe kwa sehemu kubwa juu ya uaminifu wa wananchi, hasa huko vijijini kwa chama hiki; uaminifu ambao unatokana na sifa zilizojengeka kwa muda mrefu, hasa baada ya kuundwa kwa chama hiki. Hawa wananchi wameshikilia kumbukumbu tu ya mambo hayo ya zamani, bila kutambua mabadiliko makubwa yaliyokwishatokea ndani ya chama hiki.
Sikubaliani tena nawe kuhusu maelezo yako kwa CHADEMA, hii ni kasumba tu inayotumiwa, hasa na hawa watu ndani ya CCM kuhadaa wananchi wasiokuwa na udadisi wa mambo nje ya chama cha CCM. CHADEMA siyo chama cha hisa tena.
Tatizo ninaloliona kwa CHADEMA ni kukosa uongozi wenye moto ndani ya matumbo yao. Viongozi ambao wananchi wangewasikia na kuwasikiliza kwa makini zaidi. Lissu anajaribu, ila anaharibiwa tu na mtindo anaoutumia kueleza mambo wananchi wayaelewe, basi.Sekretarieti ya CHADEMA iliyofanya kazi wakati wa Slaa ingejipanga vizuri sasa hivi, mambo yangekuwa mazuri sana kwa chama hicho.
CCM sasa hivi walichobaki nacho na kukitegemea, ni hilo la 'Dola' ulilolieleza wewe. Binafsi naamini kuwa, hata hiyo 'Dola' itakuwa na watu ambao wanayajali maslahi ya nchi hii. Kinachotakiwa tu ni kwa CHADEMA kujieleza kwa wananchi, na kuwaelimisha baadhi ya hao ambao bado wanadhani CCM ya Mwalimu, chama cha wakulima na wafanyakazi bado kipo kikiwakilishwa na CCM hii ya Samia!
CCM hiyo ilishakufa siku nyingi, CCM hii ni chama cha "Hawa ni Wenzetu", chama cha wasaka fursa kwa njia zozote ziwezekanazo kujinufaisha wenyewe.
Hii siyo CCM inayojali maslahi ya taifa hili.
Ni CCM iliyogeuka na kuwa adui namba moja wa taifa letu.