Fikra hizi ndizo zinazotakiwa kuondolewa akilini mwa waTanzania, na hasa vyama vya upinzani.HATOGOMBEA.
Bila tume HURU ya UCHAGUZI na KATIBA mpya,hapatafanyika uchaguzi wowote wa HAKI.
Huku ni kukubali kuwa uhalifu unalipa. Uvunjaji wa sheria unazawadiwa.
CCM wanafanya uhalifu kwa sababu wananchi wanawaruhusu kufanya hivyo. Wananchi wakikataa, CCM hawana njia yoyote ya kung'ang'aniza ushindi usiokuwa halali.
Hakuna chombo chochote cha "Dola" kilicho tayari kushiriki kuwahujumu wananchi wa nch hii. Hawawezi kukubali kutumiwa na CCM kufanya uhalifu dhidi ya wananchi.
Ndiyo maana tunasisitiza CHADEMA waweke mkazo zaidi kufanya kazi na wananchi na kuwaelimisha ili wazuie uhalifu unaofanywa na CCM.
Kwa hiyo mkuu 'Rabbon', pamoja na kutambua hili la umuhimu wa Tume Huru ya uchaguzi na uwepo wa Katiba Mpya (jambo lisilowezekana sasa kwa muda huu uliopo), msisitizo wangu ni kwa CHADEMA na wengineo kutilia mkazo kutambua aina ya uhalifu ufanywao na CCM nyakati za uchaguzi. Wakishazitambua njia zote muhimu zitumikazo, kazi inageukia katika kutafuta ufumbuzi, njia za kuzuia uhalifu.
Swala la kutoshiriki uchaguzi, hilo sahau kabisa. CCM wanalipenda sana wazo hilo.