Naiona ile Spirit ya 1995 ikirejea kwa kasi, CHADEMA na Chama kipya vitapata Wabunge wengi lakini CCM itashinda Urais. PM atatoka Upinzani

Upuuzi,kwamba hao ropo ropo wanaweza Waziri ccm wabunge? Ina uhakika?

Jimbo lenyewe la Nkasi Kwa mbunge wao anaweza asishinde Kwa sababu waliompotisha ni Wana ccm kimkomoa Kessy na Magufuli,yule aliyeongoza kura za maoni anarejea
Labda Dr Biteko PhD atende Miujiza!
 
Mkuu ccm wana mbinu 36 za kuiba uchaguzi, mpk leo wametumia mbinu 6 tu. Hebu fikiria wakizitumia hizo mbinu 30 mwaka 2025 upinzani utatoboa?

Ili kuifikia ndoto ulionayo katiba mpya na bora yapaswa kuandikwa.
Hizo ni story za zamani tena za kijiweni
 
Kama ni hivo basi WASHAFELI
 
Mkuu 'Midimay', unastahili heshima kwa mawazo uliyoweka hapa. Ni mawazo yaliyotumia fikra makini.
Mimi sikubaliani na baadhi ya hayo mawazo.

CCM kwa sasa ni debe tupu kabisa linalosubiri kutobolewa, kwa sababu limekwishadhoofishwa na kutu ndani kwa ndani.
Ni watu wachache sana humo ndani ya chama hicho sasa hivi unaoweza kuwategemea kwa mengi uliyoeleza wewe; mmoja ni huyo Kinana, sina mfano mwingine tena.

Ninakubaliana nawe kwa sehemu kubwa juu ya uaminifu wa wananchi, hasa huko vijijini kwa chama hiki; uaminifu ambao unatokana na sifa zilizojengeka kwa muda mrefu, hasa baada ya kuundwa kwa chama hiki. Hawa wananchi wameshikilia kumbukumbu tu ya mambo hayo ya zamani, bila kutambua mabadiliko makubwa yaliyokwishatokea ndani ya chama hiki.

Sikubaliani tena nawe kuhusu maelezo yako kwa CHADEMA, hii ni kasumba tu inayotumiwa, hasa na hawa watu ndani ya CCM kuhadaa wananchi wasiokuwa na udadisi wa mambo nje ya chama cha CCM. CHADEMA siyo chama cha hisa tena.
Tatizo ninaloliona kwa CHADEMA ni kukosa uongozi wenye moto ndani ya matumbo yao. Viongozi ambao wananchi wangewasikia na kuwasikiliza kwa makini zaidi. Lissu anajaribu, ila anaharibiwa tu na mtindo anaoutumia kueleza mambo wananchi wayaelewe, basi.Sekretarieti ya CHADEMA iliyofanya kazi wakati wa Slaa ingejipanga vizuri sasa hivi, mambo yangekuwa mazuri sana kwa chama hicho.

CCM sasa hivi walichobaki nacho na kukitegemea, ni hilo la 'Dola' ulilolieleza wewe. Binafsi naamini kuwa, hata hiyo 'Dola' itakuwa na watu ambao wanayajali maslahi ya nchi hii. Kinachotakiwa tu ni kwa CHADEMA kujieleza kwa wananchi, na kuwaelimisha baadhi ya hao ambao bado wanadhani CCM ya Mwalimu, chama cha wakulima na wafanyakazi bado kipo kikiwakilishwa na CCM hii ya Samia!
CCM hiyo ilishakufa siku nyingi, CCM hii ni chama cha "Hawa ni Wenzetu", chama cha wasaka fursa kwa njia zozote ziwezekanazo kujinufaisha wenyewe.
Hii siyo CCM inayojali maslahi ya taifa hili.
Ni CCM iliyogeuka na kuwa adui namba moja wa taifa letu.
 
Heshima mkuu 'Rabbon'.

"Marekebisho katika Katiba na kuundwa Tume Huru ya Uchaguzi" hakutakuwa na maana yoyote kama CHADEMA watategemea fadhila hiyo na kusahau kuwa hayo marekebisho kwa CCM ni kama kulaza akili za watu tu!

Rais bado atakuwa juu ya sheria zote, pamoja na uwezo wa kukanyaga kila kitu hata hayo marekebisho feki.
Hili ni muhimu watu walitambue, hasa kwa chama kama CHADEMA.

Dawa pekee ya kuyatibu maradhi haya, ni kwa wananchi kuwa tayari kukataa hujuma hizo; uhalifu wowote wanaoweza kuubuni CCM. Hiyo ndiyo dawa pekee.

Nafasi ipo nzuri sana kwa wananchi kuelezwa na kuelewa wajibu wao huo. Kazi hiyo (ngumu) inawaangukia sasa hivi CHADEMA, waifanye kwa umakini wote wanaoweza kuwa nao. Wawaelimishe wananchi.

Kwa bahati mbaya sana, hakuna mbadala wa hili kwa sasa, ukiondoa yaliyofanyika kwa Ali Bongo hivi karibuni.
 
Naandika nafuta, naandika nafuta,

Anyway nimezuiwa kujibu zaidi ya hapa.

Tusubiri.
 
Umemaliza kila kitu mkuu.....2025 tutakomaa na hawa Cartels mpaka kieleweke
 
kwenye hii ndoto ulikua unastitukastuka sana 🀣
 
Kabisa hata mimi naona kama CDM wakijipanga vizuri kutoa elimu na awareness ya namna ya kupambana na timu ya wezi wa kura toka CCM naamini coming 2025 itakuwa ni jino kwa jino na hawataamini solidarity ya wananchi.
 
CCM inaenda kufa
Hilo litakuwa jambo la kusikitisha sana, kama ndani ya chama hicho kilichojijengea heshima kubwa duniani kutakuwa hakuna aliyebakia kukinusuru kisifikie mwisho wake kama unavyoeleza hapa.

Hicho chama kina historia ya kipekee sana, inasikitisha tu kwamba kimefikia kwenye ngazi hii ya kutisha sana.
 
Mbowe hajakataa tamaa tuu ya kuwa waziri mkuu baada ya masaa 72?
 
Heshima kubwa kwako pia. Hasa kwa kuwa umetofautiana kwa heshima na kwa hoja.
 

Tafuta maisha yako hizo ramli hazitakusaidia
 
Asante kwa taarifa mkuu πŸ˜€
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…