Naiona Yanga yangu ikibomoka vipande vipande baada ya mechi na Rivers Utd

Naiona Yanga yangu ikibomoka vipande vipande baada ya mechi na Rivers Utd

Ili utopolo asonge mbele inatakiwa kwa mkapa ashinde goli zisizopungua tatu bila[emoji23][emoji23][emoji23]

Kitu ambacho ni ngumu, kule Nigeria wanaenda kuezekwa 6 bila wanarudi kulalamikia TFF[emoji28]
 
Kama kweli wewe ni shabiki wa Yanga, basi utakua umetudhalilisha sana mashabiki wenzako! Kwa huu mtazamo wako, ulistahili kabisa kuwa shabiki wa mbumbumbu fc!...
Usipanic mkuu, jamaa yupo sawa kwa mara nyingine tena mmebomoa timu yooote na kuleta wengi wapya., Hamboreshi timu ila mnaanzisha timu mpya.

Kwahesabu za kawaida tuu ilibidi muwaache wachezaji wazoeane bahati mbaya hawajazoeana mnawekeza kwenye mwananchi week wakati rever wanawapumilia kisogoni, Kazi mnayo mbona
 
Usipanic mkuu, jamaa yupo sawa kwa mara nyingine tena mmebomoa timu yooote na kuleta wengi wapya., Hamboreshi timu ila mnaanzisha timu mpya. Kwahesabu za kawaida tuu ilibidi muwaache wachezaji wazoeane bahati mbaya hawajazoeana mnawekeza kwenye mwananchi week wakati rever wanawapumilia kisogoni, Kazi mnayo mbona
Timu haijabomoka mzee!! Ukimuondoa Tuisila Kisinda, hakuna mchezaji mwingine ambaye alikuwa ni muhimu kwenye timu kwa 100%!! Hivyo kiufundi, timu iko imara sana! Maana wachezaji waliosajiliwa, kwa mtazamo wangu ni bora zaidi ya wale waliopewa mkono wa kwa heri.

Sasa unapokuwa na wachezaji wazuri, huhitaji msimu mzima kukijenga kikosi. Kama ni Heritiel Makambo, tayari anaifahamu Yanga in and out! Tusubiri muda ufike ili tuone kitakacho tokea. Lakini ukweli uko pale pale! Yanga msimu huu ina kikosi bora kabisa cha mashindano.
 
Kama kweli wewe ni shabiki wa Yanga, basi utakua umetudhalilisha sana mashabiki wenzako! Kwa huu mtazamo wako, ulistahili kabisa kuwa shabiki wa mbumbumbu fc!...
Wewe kweli ni mwananchi mwenzetu. Sio huyo mwanzisha uzi anaandika kama mbumbumbu fc
 
Naona mnamshambulia sana mleta mada lakini alichokiongea kinaweza kutokea kwa mashabiki wa Yanga. Yanga inapaswa kuwekeza akili kwenye mechi dhidi ya Rivers Utd lakini mpaka sasa hawajacheza mchezo wowote ule wa kirafiki ili kuona palipo na mapungufu...
Sasa mzee mechi ya kirafiki si mpaka mwalimu apate kikosi chake cha kwanza. Timu bado iko kambini, na muda bado unaruhusu kucheza mechi za kirafiki hata mbili huko huko Morocco.

Lakini hata hiyo siku ya Mwananchi, ukiondoa utambulisho wa wachezaji, bado timi itacheza mechi nyingine ya kirafiki na timu mwalikwa! Yanga hii haina sifa ya kutolewa na hao Rivers United kwenye hatua ya awali! Na hata ikitokea ikatolewa, bado sijaona Yanga ya kuishi kinyonge!

Labda itokee Viongozi na Wadhamini wa timu wawe wababaishaji kwenye malipo ya mishahara ya wachezaji, malipo ya mikataba yao, au fedha zao za motisha!
 
Yanga ya msimu huu ni wazi inatembelea nyota ya AS Vita, kitendo cha kusajili nyota wengi wapya wenye uwezo mzuri. Naitabiria kuwa itafika Groups stage.
 
Sasa mzee mechi ya kirafiki si mpaka mwalimu apate kikosi chake cha kwanza. Timu bado iko kambini, na muda bado unaruhusu kucheza mechi za kirafiki hata mbili huko huko Morocco...
Kuna kitu kinaitwa muda. Muda huwa hausubiri mtu hata siku moja, kama mpaka leo tarehe 22 bado mwalimu hana kikosi wakati zimebaki takribani wiki tatu tu kucheza first leg ya klabu bingwa. Ili kuendana na muda ilipaswa acheze mechi hata nne ya kirafiki ili kujiweka sawa.

Wiki ya mwananchi inapoteza muda tu wala halina impact yoyote katika kuongeza kitu kuelekea mechi ya klabu bingwa. Kama Yanga wanafanya tamasha la wiki ya mwananchi inamaana itapunguza wiki mbili nzima ya kufanya maaandalizi ya mechi ya klabu bingwa maana sio rahisi kucheza tena mechi ya kirafiki na timu ya maana baada ya kuisha wiki ya mwananchi.

Na tukija kwenye tukio lenyewe la wiki ya mwananchi ni kwamba huwa akuna mcheza ambaye anakuwa katika kiwango kibovu siku hiyo. Kila mchezaji anakuwa na kiwango kikubwa. Kumbuka Sarpong kwenye wiki ya mwananchi msimu uliopita. Alionekana kama bonge la straika kumbe hamna kitu.
 
Kama kweli wewe ni shabiki wa Yanga, basi utakua umetudhalilisha sana mashabiki wenzako! Kwa huu mtazamo wako, ulistahili kabisa kuwa shabiki wa mbumbumbu fc!..
kwa ulicho ongea ni sahihi kabisa,lakini hiyo ni angalizo kwa benchi la ufundi pamoja na wachezaji wasiifikirie sana mwananchi day...na badala yake wajiandae na hiyo mechi ili tuwapige hata goli 7 kwa mkapa
 
Yanga ya msimu huu ni wazi inatembelea nyota ya AS Vita, kitendo cha kusajili nyota wengi wapya wenye uwezo mzuri. Naitabiria kuwa itafika Groups stage.
itapendeza sana...mikia watanuna
 
Chonde chonde viongozi wangu hasa GSM itilieni mkazo mechi hii na msipoanglia kwa umakini inaweza ikawa chanzo cha nyie kuondoka Yanga.

Atleast yanga hiii inatakiwa kufika group stage caf champions leage.
Mbona ueleweki!!!!

Screenshot_2021-08-22_180554.jpg
 
NABI kocha wa uto amesema anahitaji siku 90 ili kuwa na kikosi cha ushindani, manake mtaingia club bingwa mkiwa bado hamna kikosi imara. UTO first round out.
 
Back
Top Bottom