Uchaguzi 2020 Naipenda CCM, Sipendi yanayojiri

Uchaguzi 2020 Naipenda CCM, Sipendi yanayojiri

Ninakipenda sana chama changu cha CCM, lakini sifurahishwi na yanatoendelea:

1. Kwa mara ya kwanza campaigne ya Urais na Wabunge haina muelekeo. Magufuli umefeli sana na kukiharibu chama kwa kuwashirikisha vijana/ watu wasio na ujuzi wa namna kampeni zinavyoendeshwa.

2. Magufuli chukua hatua za haraka sana kubadilisha kampeni team yako.

3. Magufuli dhambi inayokusubiri ni chama kufia mikononi mwako, na dola kuwapa chadema, wanaichukua bila taabu yoyote, kwani mumekiweka chama kiholela.

4. Mmetumia pesa nyingi sana za chama, kuwarubuni na kuwanunua wapinzani, ambao hawana la kutuongezea, na ununuzi wao umeleta mfarakano ndani ya chama.

Mheshimiwa Rais, chukua ushauri, na rekebisha team yako, akina Polepole , Bashiru na wenzao wamefeli.
Wamekusikia
 
Back
Top Bottom