Naipenda Tanzania Yangu Ndiyo Maana Ukweli Huu Unaniuma. Tusemezane Tuamke!

Davidmmarista

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2024
Posts
3,114
Reaction score
6,309
Jana usiku nilikuwa macho saa 7 nikitazama launch ya Artemis 2 live. Kwa wale hawajui, hii ni mission ya NASA itakayozunguka mwezi ndani ya siku 10 tu. Nilikuwa nasherehekea moyoni, nikijivunia ubinadamu, nikifikiri jinsi akili ya mtu ilivyofika mbali kiasi hiki.

Kisha nikafungua comments.
Wabongo walikuwepo kwa wingi kwenye social media mbalimbali kuhusu hizi post za Artemis. Na kama unavyotegemea, wengi walikuwa wanasema kitu kimoja tu "Launch ya Artemis ni uongo, CGI, hakuna binadamu aliyewahi kufika mwezini." Nikachoka kusoma lakini nikaendelea, kwa sababu nilihitaji kujua tupo mbali kiasi gani.
Sasa niambie, moon landing ni uongo? Binadamu amefika mwezini mara 6. Sita kamili. Apollo 11, 12, 14, 15, 16 na 17. Watu 12 wamesimama mwezini kwa miguu yao wenyewe. Na hii ilithibitishwa na Urusi ambao wakati ule walikuwa maadui wakubwa wa Marekani. Kama ingekuwa uongo, Urusi wangekuwa wa kwanza kushangilia na kuudanganya ulimwengu. Hawakufanya hivyo. Kwa sababu matukio yalikuwa ya kweli.

Na si hivyo tu wazee. Leo hii Curiosity Rover iko Mars inachunguza na kutuma picha. Parker Solar Probe inasafiri kwa 700,000km/h, imegusa ukingo wa jua. Voyager 1 na 2 ziliondoka 1977 na sasa ziko nje kabisa ya mfumo wetu wa jua, bado zinawasiliana na Dunia. Vyombo hivi vipo. Data ipo. Picha zipo. Nchi zaidi ya 100 zinafuatilia kila kitu hiki.

Uongo wa aina hiyo ungehitaji nchi zote hizo, wanasayansi maelfu, wahandisi, wapinzani wa kisiasa wote kukubaliana kudanganya pamoja kwa miaka 50+ bila mtu mmoja kuvuja siri. Fikiria kama hiyo ina mantiki.
Tatizo siyo NASA. Tatizo ni sisi wenyewe. Conspiracy theories zinaota vizuri mahali ambapo elimu haikupandwa(especially kwetu hapa). Sio kejeli, ni ukweli. Mtu ambaye hajawahi kuelewa jinsi sayansi inavyofanya kazi ataogopa na kukataa kila kitu anachokiona. Na badala ya kusema "sijui, nisome zaidi" anasema "ni uongo, ni Illuminati, ni agenda." Kwa sababu kuamini njama ni rahisi kuliko kujifunza.
Tatizo jingine kubwa ni kiburi cha ujinga. Yaani mtu anaamini kwa nguvu zote kitu ambacho hakijapata utafiti wowote, na yeyote anayemletea ukweli anaitwa mjinga au msaliti. Hali hii ni hatari zaidi ya kutojua, kwa sababu angalau asiyejua anaweza kufunzwa. Lakini anayekataa kujua ni mgumu kumfikia.

Ninajua wengine watasema mimi ni mkoloni wa akili labda, au naamini kila kitu cha mzungu. Jibu langu ni moja tu sayansi haina rangi. Haina kabila. Haina dini. Gravity inafanya kazi vivyo hivyo Tanzania kama inavyofanya kazi New York. Mwezi unazunguka dunia bila kujua wewe ni Mtanzania au la. Ukweli hauombi ruhusa yako kuwa ukweli.

Ningepenga Tanzania yetu iinuke. Ninataka tuwe sehemu ya mazungumzo makubwa ya dunia. Lakini haiwezekani kama bado tunapigana na ukweli wa miaka 50 iliyopita huku dunia ikisonga mbele. Hatuwezi kujenga taifa la kesho kwa akili ya jana iliyojaa mashaka ya kubuni.

Soma. Uliza maswali. Kaa na wasiwasi wako lakini uupeleke kwenye utafiti, si kwenye comments za kuchochea wengine. Hapa ndio utajua tofauti kati ya mtu anayetafuta ukweli na mtu anayetafuta kuthibitisha alichokuwa anaamini tayari.

Tutaamka lini? Sijui. Lakini natumai ni hivi karibuni.
 
Wengi wanaopinga mambo haya ni wale Anti - America na Pro Muslim wanaamini jambo likifanywa na US, ni uongo...
 
Bro USA imetuletea mambo mangapi, on my opinion I think the most intelligent invention ever done by man is the microprocessor ndio ubongo wa kila computer na smart machine.

Microprocessor imegunduliwa marekani I think ni bells lab/silicon valley invention. Bado huyu anti-US anatumia simu, anaenda hospital na kutumia vifaa venye microprocessor, anatumia network na internet, AI ambazo kitovu chake ni microprocessor it or binary bila kumdanganya.

Ujuaji ni mbaya sana, it's true sometimes the US wanazingua but not in technology that impacts the current world.
 
Ndugu yangu kama tu tanzania kuna msomi bado anaamini dunia ni tambalale. Yaani iko kama sahani. Na huyo kahitimu chuo sasa. Pata picha aliyeacha shule darasa la sita na leo ana tecno yake atayaelewa hayo mambo ya anga za mbali
 
Wengi wanaopinga mambo haya ni wale Anti - America na Pro Muslim wanaamini jambo likifanywa na US, ni uongo...
Plus Na chuki binafsi... Hii kitu nishajaribu kuelezea kwamba mwanadamu amefika mwezini lakini wanaamini ni uongo .. eti NASA walienda ku shoot video jangwani.just imagine
 
Ndugu yangu kama tu tanzania kuna msomi bado anaamini dunia ni tambalale. Yaani iko kama sahani. Na huyo kahitimu chuo sasa. Pata picha aliyeacha shule darasa la sita na leo ana tecno yake atayaelewa hayo mambo ya anga za mbali
Dah tupo nyuma sana aise, na tatizo muda mwingine mbali na kuilaumu serekali ni watu wenyewe. Watu Wengi wanaendeshwa na Imani instead of research and facts.
 
Plus Na chuki binafsi... Hii kitu nishajaribu kuelezea kwamba mwanadamu amefika mwezini lakini wanaamini ni uongo .. eti NASA walienda ku shoot video jangwani.just imagine
It would be harder to fake moon landing 6 times than going there.
 
Naweza kuamini allien wapo lakin issue za apollo kufika mwezini zinacontroversies nyingi mpaka unaacha kila mmoja aamini anachojua...
 
Hata wewe mkuu pamoja na code zote unazopiga lakn issue ya apollo mission hujui kitu zaidi ya kuaminishwa kile wanachotaka uamini...
Hata ile ya NEIL AMSTRONG imejaa uongo mtupu...
sitak hapa kuskia stori za apollo mission
 
Ndugu yangu kama tu tanzania kuna msomi bado anaamini dunia ni tambalale. Yaani iko kama sahani. Na huyo kahitimu chuo sasa. Pata picha aliyeacha shule darasa la sita na leo ana tecno yake atayaelewa hayo mambo ya anga za mbali

Shida sio kuto kuelewa mambo ya anga, shida ni kua na Opinions kwenye mambo ambayo huyaelewi.
 
Naweza kuamini allien wapo lakin issue za apollo kufika mwezini zinacontroversies nyingi mpaka unaacha kila mmoja aamini anachojua...
Kwahiyo hii issue ya Artemis 2 unadhani wameshoot movie tu boss?

Chandrayaan ya wahindi 2024 hiyo Moon Rover waliokuta mwezini unadhani ni uongo?
 
Nilianza kufuatilia sayansi ya anga miaka 1987 kuna Astronomer mmoja wa iliyokuwa Soviet ya zamani (USSR) alivunja rekodi ya kukaa angani na chombo cha Kirusi kwa siku 236 ilikuwa rekodi ya dunia kwa miaka hiyo ya 1987 ingawa ilimletea matatizo kidogo kiafya..
 
Jana usiku nilikuwa macho saa 7 nikitazama launch ya Artemis 2 live. Kwa wale hawajui, hii ni mission ya NASA itakayozunguka mwezi ndani ya siku 10 tu. Nilikuwa nasherehekea moyoni, nikijivunia ubinadamu, nikifikiri jinsi akili ya mtu ilivyofika mbali kiasi hiki.

Kisha nikafungua comments.
Wabongo walikuwepo kwa wingi kwenye social media mbalimbali kuhusu hizi post za Artemis. Na kama unavyotegemea, wengi walikuwa wanasema kitu kimoja tu "Launch ya Artemis ni uongo, CGI, hakuna binadamu aliyewahi kufika mwezini." Nikachoka kusoma lakini nikaendelea, kwa sababu nilihitaji kujua tupo mbali kiasi gani.
Sasa niambie, moon landing ni uongo? Binadamu amefika mwezini mara 6. Sita kamili. Apollo 11, 12, 14, 15, 16 na 17. Watu 12 wamesimama mwezini kwa miguu yao wenyewe. Na hii ilithibitishwa na Urusi ambao wakati ule walikuwa maadui wakubwa wa Marekani. Kama ingekuwa uongo, Urusi wangekuwa wa kwanza kushangilia na kuudanganya ulimwengu. Hawakufanya hivyo. Kwa sababu matukio yalikuwa ya kweli.

Na si hivyo tu wazee. Leo hii Curiosity Rover iko Mars inachunguza na kutuma picha. Parker Solar Probe inasafiri kwa 700,000km/h, imegusa ukingo wa jua. Voyager 1 na 2 ziliondoka 1977 na sasa ziko nje kabisa ya mfumo wetu wa jua, bado zinawasiliana na Dunia. Vyombo hivi vipo. Data ipo. Picha zipo. Nchi zaidi ya 100 zinafuatilia kila kitu hiki.

Uongo wa aina hiyo ungehitaji nchi zote hizo, wanasayansi maelfu, wahandisi, wapinzani wa kisiasa wote kukubaliana kudanganya pamoja kwa miaka 50+ bila mtu mmoja kuvuja siri. Fikiria kama hiyo ina mantiki.
Tatizo siyo NASA. Tatizo ni sisi wenyewe. Conspiracy theories zinaota vizuri mahali ambapo elimu haikupandwa(especially kwetu hapa). Sio kejeli, ni ukweli. Mtu ambaye hajawahi kuelewa jinsi sayansi inavyofanya kazi ataogopa na kukataa kila kitu anachokiona. Na badala ya kusema "sijui, nisome zaidi" anasema "ni uongo, ni Illuminati, ni agenda." Kwa sababu kuamini njama ni rahisi kuliko kujifunza.
Tatizo jingine kubwa ni kiburi cha ujinga. Yaani mtu anaamini kwa nguvu zote kitu ambacho hakijapata utafiti wowote, na yeyote anayemletea ukweli anaitwa mjinga au msaliti. Hali hii ni hatari zaidi ya kutojua, kwa sababu angalau asiyejua anaweza kufunzwa. Lakini anayekataa kujua ni mgumu kumfikia.

Ninajua wengine watasema mimi ni mkoloni wa akili labda, au naamini kila kitu cha mzungu. Jibu langu ni moja tu sayansi haina rangi. Haina kabila. Haina dini. Gravity inafanya kazi vivyo hivyo Tanzania kama inavyofanya kazi New York. Mwezi unazunguka dunia bila kujua wewe ni Mtanzania au la. Ukweli hauombi ruhusa yako kuwa ukweli.

Ningepenga Tanzania yetu iinuke. Ninataka tuwe sehemu ya mazungumzo makubwa ya dunia. Lakini haiwezekani kama bado tunapigana na ukweli wa miaka 50 iliyopita huku dunia ikisonga mbele. Hatuwezi kujenga taifa la kesho kwa akili ya jana iliyojaa mashaka ya kubuni.

Soma. Uliza maswali. Kaa na wasiwasi wako lakini uupeleke kwenye utafiti, si kwenye comments za kuchochea wengine. Hapa ndio utajua tofauti kati ya mtu anayetafuta ukweli na mtu anayetafuta kuthibitisha alichokuwa anaamini tayari.

Tutaamka lini? Sijui. Lakini natumai ni hivi karibuni.
Umeongea kisomi sana. 80% wa wana JF hawatakuelewa, kwa sababu hawana uwezo wa kuona mambo kwa jinsi unavyoyaelewa. Watasoma comment moja tu ya watu wa conspiracy theory kwamba "Launch ya Artemis ni uongo, CGI, hakuna binadamu aliyewahi kufika mwezini" na watakubishia hadi asubuhi
 
Seran watu Hawaamini kuwa wamarekan na mataifa mengne yashafika mwezini . Ila wanaamin haya yaliyopo kwenye vitabu vya Hadith za Mtume.

Ajab kweli kweli.

Quran 54:1 : "saa imekaribia na mwezi umepasuka."

Hadith kutoka Sahih al-Bukhari.
Riwaya ya Abdullah ibn Mas'ud.
Kutoka
“Mwezi ulipasuka katika zama za Mtume Muhammad ukawa vipande viwili; kipande kimoja kilikuwa juu ya mlima na kingine chini yake. Mtume akasema: ‘Shuhudieni.".

Hadithi nyingne(Sahih al-Bukhari).
Riwaya ya Anas ibn Malik
“Watu wa Makka walimwomba Mtume awaonyeshe muujiza, basi akaonyesha kupasuka kwa mwezi mara mbili (yaani ukaonekana vipande viwili).”
 
It would be harder to fake moon landing 6 times than going there.
Very well said! Na pia why would you fake Apollo 13 after you managed to mislead people with Apollo 11 and 12, especially knowing that Russia was watching after you lied on Apollo 11 and 12? If Americans are lying about moon landing, then the Russians are supporting their lies. After all, it was Russia that made the first attempt to land on the Moon, the Soviet Luna 2 mission of September 1959, which was a planned hard impact (crash) landing. It successfully became the first man-made object to reach the Moon's surface.
 
Back
Top Bottom