Naipenda Tanzania Yangu Ndiyo Maana Ukweli Huu Unaniuma. Tusemezane Tuamke!

Naipenda Tanzania Yangu Ndiyo Maana Ukweli Huu Unaniuma. Tusemezane Tuamke!

Mmh, Juhudi zote zile walizofanya kina Wernher Von Braun, Arthur Rudolph, Kurt Debus, Hurbetus Strughold, Walter Dornberger kukomaa na real scientific experiments za Kila kitu kuhusu anga.

US walikwenda kweli mwezini bila Shaka na kule walivyofika mwezini walikutana na suprises kadhaa ndio maana walisitisha kidogo kwa muda mrefu safari za mwezini, kina Neil Armstrong na wenzake kama utakuwa umeona zile picha zao wakiwa mbele ya press hata nyuso zilionesha kuna kitu hakikuwa sawa huko walipotoka then walisainishwa makaratasi ya kutosema chochote kile in details...

Kwani unafikiri Hadi wanatangaza Jeshi rasmi la anga (SPACE FORCE) mwaka 2019 walikuwa na maana gani muda wote huo na ni nini maana ya SPACE FORCE ilihali Wana US AIR FORCE na kwanini wakae muda wote huo bila kuwa na SPACE FORCE, nini maana ya FORCE Kwanza kiusalama?...
 
Jana usiku nilikuwa macho saa 7 nikitazama launch ya Artemis 2 live. Kwa wale hawajui, hii ni mission ya NASA itakayozunguka mwezi ndani ya siku 10 tu. Nilikuwa nasherehekea moyoni, nikijivunia ubinadamu, nikifikiri jinsi akili ya mtu ilivyofika mbali kiasi hiki.

Kisha nikafungua comments.
Wabongo walikuwepo kwa wingi kwenye social media mbalimbali kuhusu hizi post za Artemis. Na kama unavyotegemea, wengi walikuwa wanasema kitu kimoja tu "Launch ya Artemis ni uongo, CGI, hakuna binadamu aliyewahi kufika mwezini." Nikachoka kusoma lakini nikaendelea, kwa sababu nilihitaji kujua tupo mbali kiasi gani.
Sasa niambie, moon landing ni uongo? Binadamu amefika mwezini mara 6. Sita kamili. Apollo 11, 12, 14, 15, 16 na 17. Watu 12 wamesimama mwezini kwa miguu yao wenyewe. Na hii ilithibitishwa na Urusi ambao wakati ule walikuwa maadui wakubwa wa Marekani. Kama ingekuwa uongo, Urusi wangekuwa wa kwanza kushangilia na kuudanganya ulimwengu. Hawakufanya hivyo. Kwa sababu matukio yalikuwa ya kweli.

Na si hivyo tu wazee. Leo hii Curiosity Rover iko Mars inachunguza na kutuma picha. Parker Solar Probe inasafiri kwa 700,000km/h, imegusa ukingo wa jua. Voyager 1 na 2 ziliondoka 1977 na sasa ziko nje kabisa ya mfumo wetu wa jua, bado zinawasiliana na Dunia. Vyombo hivi vipo. Data ipo. Picha zipo. Nchi zaidi ya 100 zinafuatilia kila kitu hiki.

Uongo wa aina hiyo ungehitaji nchi zote hizo, wanasayansi maelfu, wahandisi, wapinzani wa kisiasa wote kukubaliana kudanganya pamoja kwa miaka 50+ bila mtu mmoja kuvuja siri. Fikiria kama hiyo ina mantiki.
Tatizo siyo NASA. Tatizo ni sisi wenyewe. Conspiracy theories zinaota vizuri mahali ambapo elimu haikupandwa(especially kwetu hapa). Sio kejeli, ni ukweli. Mtu ambaye hajawahi kuelewa jinsi sayansi inavyofanya kazi ataogopa na kukataa kila kitu anachokiona. Na badala ya kusema "sijui, nisome zaidi" anasema "ni uongo, ni Illuminati, ni agenda." Kwa sababu kuamini njama ni rahisi kuliko kujifunza.
Tatizo jingine kubwa ni kiburi cha ujinga. Yaani mtu anaamini kwa nguvu zote kitu ambacho hakijapata utafiti wowote, na yeyote anayemletea ukweli anaitwa mjinga au msaliti. Hali hii ni hatari zaidi ya kutojua, kwa sababu angalau asiyejua anaweza kufunzwa. Lakini anayekataa kujua ni mgumu kumfikia.

Ninajua wengine watasema mimi ni mkoloni wa akili labda, au naamini kila kitu cha mzungu. Jibu langu ni moja tu sayansi haina rangi. Haina kabila. Haina dini. Gravity inafanya kazi vivyo hivyo Tanzania kama inavyofanya kazi New York. Mwezi unazunguka dunia bila kujua wewe ni Mtanzania au la. Ukweli hauombi ruhusa yako kuwa ukweli.

Ningepenga Tanzania yetu iinuke. Ninataka tuwe sehemu ya mazungumzo makubwa ya dunia. Lakini haiwezekani kama bado tunapigana na ukweli wa miaka 50 iliyopita huku dunia ikisonga mbele. Hatuwezi kujenga taifa la kesho kwa akili ya jana iliyojaa mashaka ya kubuni.

Soma. Uliza maswali. Kaa na wasiwasi wako lakini uupeleke kwenye utafiti, si kwenye comments za kuchochea wengine. Hapa ndio utajua tofauti kati ya mtu anayetafuta ukweli na mtu anayetafuta kuthibitisha alichokuwa anaamini tayari.

Tutaamka lini? Sijui. Lakini natumai ni hivi karibuni.
Nilisoma humu jamvini hadi aibu kwa memba wakongwe wanavyochangia.
Vita ya US, Israel Vs Iran imeonyesha udhaifu mkubwa sana kwa baadhi ya member waandamizi hapa jamvini.
 
Back
Top Bottom