Naipongeza serikali kwa kuanzisha kodi hii ya nyumba na sehemu za biashara kwa wamiliki

Mm mijengo yangu nitasema nimeweka wake zangu sipangishi kwa mtu.
 
.... Issue sio kuongeza vyanzo vya mapato, issue ni haya mapato mnayokusanya hadi sasa yanafanya kazi gani za kuonekana kama sio kuishia mifukoni mwa wajanja. hospitalini huduma mbovu, majengo ya shule machakavu na yana hadhi duni, barabara mitaani mbovu hata wakati najenga hiyo nyumba nishaingia hasara mara nyingi kwa gari kumwaga mzigo njiani kwa ubovu wa barabara leo hii nimemaliza nataka nianze kurudisha gharama zangu unasimama unakenua unataka kodi kwa msaada gani ulionipa wakati najenga... upuuzi ni kupenda kuvuna usipopanda... Boresheni Miundombinu na huduma za kijamii watu watakuwa wanatoa kodi kwa roho nyeupe na kwa uzalendo.
 
Serikali bila kuwa na industry strategy ni kazi bure kwasababu itategemea Kodi Kwa kuwakamua wasio nacho Ila kungekuepo na viwanda uchumi wa nchi ungeoxeka. Hakuna nchi Inaendelea bila kuwa na strategy ya kukuza viwanda
 
Hivi wakuu ile tunayolipa kwa kukatwa unaponunua luku ni tofauti na hii.?
 
Iyo kodi atakayeilipa ni mpangaji tu. Usitegemee kabisa mwenye nyumba alipe iyo kodi
 
Hakuna nchi iliyofanikisha maendeleo ya wananchi wake kwa kuwachonganisha na kuwanyonya
 
Sasa kama hawana database kodi ya majengo mbona inalipwa kupitia ununuzi wa Luku? Wao wamesema mpangaji ndiye atakayeilipa hiyo kodi, jambo ambalo ni sawa kabisa kwa sababu ukisema mwenye nyumba akatwe juu kwa juu italeta usumbufu pale mpangaji anapohama na vyumba kuwa vitupu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…