MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Huu mfumo wa manunuzi serikalini kidigitali (National e-Procurement System of Tanzania) kwa kifupi NEST ni mfumo mzuri ambao utasaidia kupunguza upigaji na kuleta fair play kwenye kutoa tenda za serikali.
Ni kitu kizuri kuwahi kufanywa na serikali. Wajasiriamali wenye kampuni ndogondogo wataambulia chochote kitu toka serikalini badala ya wachache kutafuna wenyewe.
Pia serikali itapata huduma na bidhaa kwa bei nzuri kwasababu ya ushindani uliopo. Gharama zitapungua sana kwa upande wa serikali. Kupitia hizi Tsh 10k wanazolipa wafanyabiashara kama fee ya tenda serikali itakusanya sana.
Pamoja na kusifu bado mfumo wa NEST una changamoto nzito mno. Kwanza ni mfumo mzito mno kuufungua.
Yaani hiyo tovuti ya NEST kufunguka inachukua muda mno. Hadi ujaze tenda na ku-submit lazima uwe na uvumilivu wa hali ya juu.
Na hapo naongelea kwa sisi wa mijini ambapo network haisumbui sana. Sasa mtu wa huko Wampembe sijui inakuwaje? Inasikitisha.
Lakini kwa upande wa taasisi za serikali zinazo-upload tenda documents nao wanapitia wakati mgumu kutokana na uzito wa mfumo. Ninajiuliza wakuu wa shule hasa za vijijini wanapitia hali gani toka huu mfumo uanze kutumika?
Ninawasihi wahusika wa NEST wachukue hatua za haraka kutatua haya matatizo kwenye mtandao wao. Hii hali ikiendelea nao watakuwa kwenye kundi la wahujumu wa jitihada za serikali.