Naipongeza TCRA kwa kumkomesha Polepole and the Likes: Massage sent!

Jamaa alikuwa ni Janga la kitaifa
 
ingekuwa mtu ambaye hakwepo kwenye serikali iliyopita ningesikiliza mada zake ,lakini mtu yule yule aliyekuwepo kwenye awamu iliyopita akijidai na kiburi leo anafundisha SoMo wengine ambalo yeye alishindwa wakati yupo ndani ya mfumo.
😅😅😅slowx2 ni mnafiki sana. Sasa watz washamgundua.
 
Karma at work.
 
Polepole anavuna alichopanda yeye na genge lake.
 
Polepole alishiriki huu upuuzi wa CCM leo analipa alichopanda, hope atajirekebisha na kuwa mpiganaji wa kweli sio njaa tuu,wapiganaji wa kweli aliokuwa anawabeza baadhi wapo jela, wengine uhamishoni na wengine wamepoteza maisha, hata humu jamaa yetu wa JF almost wamfunge na kumfilisi kabisa, dadeki wakoloni weusi ni hatari kuliko weupe
 
TCRA hawajatenda haki kwa Polepole, hapa ndani tunajadili mtu zaidi kuliko hoja.

Kama great thinkers hoja za Polepole zina tija au hapana?
 
Imekula kwake yeye na viroboto wenzake
 
Pascal Mayalla ume raise concern muhimu sana kwenye hili. Nadhani sasa TCRA ijirekebishe iepukane na kutiliwa mashaka ktk utendaji kazi wake. Iite kole ni kole na sio Kijiko kikubwa.
Naafiki.TCRA hapo imetumia ubabe.Hapa naamini kuwa kuna nguvu kubwa imetumika kusukuma TCRA kwa nguvu bila hii taasisi kukaa na kufikiri au kufanya ref.kwenye mambo mengine yaliyofanyika na yanayoendelea kufanyika na wao wanafumbia macho.

Mimi Polepole simpendi kwa sababu katika utawala uliopita alikuwa miongoni mwa viongozi wakuu na alishiriki kwa kiwango kikubwa kugandamiza uhuru na haki za watanzania na zipo clip nyingi tu zinazodhihirisha hili.Lakini hata hivyo sio juu yetu kulipa kisasi ila tusimame katika misingi ya haki.

TCRA hapa inaonyesha wazi kuwa,imelazimishwa kumfunga mdomo Polepole bila wao kujitambua kuwa kuna utaratibu wa kufuata pale mteja wao anapoonekana anakwenda kinyume na makubaliano ya mkataba waliopeana.Kwa maana nyingine hata wao TCRA wamejisahau kuwa wao pia wanawaambia wateja wao wabalance habari wakati wao hawabalance habari zao wenyewe.Hawa kina Polepole watabalance vipi wakati mizania ya TCRA upande mmoja umelemewa mpaka ukagota chini kabisa na mwingine unaninginia kule juu.

TCRA wangetaka kabalance hii habari yao wangemwita Humprey kwa maandishi (barua) na kumwelekeza au kumwonya kuhusu huo wao wanaouita upotoshaji (sasa hivi hakuna wa kumpotosha tena Mtanzania,wote wamefunguka macho) ili arekebishe pale wao wanapoona sio sawa.Hilo ni onyo la ana kwa ana au onyo kwenye mfumo wa mazungumzo.

Ni mara nyingi tumeona hili likifanyika kwenye vyombo vingi vya habari hasa magazeti,Tv na redio.Iweje leo hii TCRA haraka haraka nadhani kwa kukurupushwa inamwita tayari na hukumu wanayo mkononi.TCRA walipochukua fedha za Humprey na kumpa kibali wameshajisahau kuwa na wao hawajamtendea haki? Je akida kurudishiwa fedha zake watazirejesha?

TCRA walichotakiwa kufanya.
1.Kumwita na kumpa onyo.
2.Kumpa muda maalumu wa kurekebisha mapungufu waliyoyaona wakati anaendelea na shughuli yake kwani kibali anacho.
3.Kwenda kukagua kama marekebisho hayo yamefanyika.Kama hayakufanyika utaratibu wa makubaliano ya No.1 yanafuata.

Nb.Nashindwa kuelewa.Kibali kinatolewa baada ya mwombaji kutimiza masharti yaliyowekwa na Tcra au ni vinginevyo.Nauliza hivyo kwa sababu inaonekana wazi kuwa,Humphrey alipewa kibali kwa title aliyokuwa nayo (Katibu mwenezi wa ccm) hivyo matakwa ya kisheria hayakufuatwa.Ndiyo double standard hiyo.

Zamani kidogo baada ya mtaalamu msomi aliyekuwa mkurugenzi wa TBC Tido Mhando wakati nikiwa mkereketwa waTbc alifanya vizuri mno kubalance habari.Tunaposema kubalance habari wengine hawaelewi.Labda kidogo tu niwape hapa.Ni kitendo cha kusema au kusikia kuwa pointi A amesema kuwa pointi B shule yake imefungiwa kwa sababu 123.Then unamfuata pointi B wewe mhabarishaji sasa na kumuuliza nimepata habari zako 123 kuhusu kufungiwa shule je wewe unasemaje. kwa ufahamu wangu.Lakini wakati wa kampeni mambo yake ya kubalace yakamletea shida na yaliyompata wenye kumbukumbu mtakumbuka.

Maana yangu ni hii TV ya kwanza ambayo ingepaswa kufungiwa enzi hizo baada ya Mhando kwa kukiuka sheria ya kubalance habari ni TBC na TCRA ilikuwepo tu,na nakumbuka ilifungia magazeti mengi tu ila ikafunika kombe.Sijui sasa hivi ikoje maana mie sinayo tena hiyo channel.

Swala lililojitokeza kuwa Humphrey habalance habari kwani yeye si sawa tu na mwalimu anayetoa elimu,sawa sawa na waandishi wa vitabu, labda Tcra walitaka abalance nini.

Nadhani umefika wakati kwa vyombo binafsi na watu binafsi wa habari kujiunga kwa pamoja kwa umoja wao kuwa na chombo HURU cha kwao cha kuwatetea mambo yanapokwenda ndivyo sivyo bila kujali itikadi za vyama vyao na bila kuwepo mamluki.
 
well, noted
 
Polepole ajifunze kuheshimu awamu ya sita na nyingine nyingi tu zijazo elimu yake ya ujasiriamali awafundishe wanawe sisi watanzania tumemchoka pia ni mtu kigeugeu
Mko wangapi watanzania mnaoandika hiyo quote yako, jisemee na usitusemee!

Mimi ni mtanzania ninamsupport mh Polepole 100%
 
Pole pole kapigwa 'bambi' watoto wa mjini wanaielewa vyema. Kazimwa kiakili.
 
Atulize mzuka. Kama watu miili ya watu iliokotwa Coco Beach ikiwa ndani ya viroba na akakaa kimya asiongee chochote basi na sasa atulie tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…