Hakuna namna ya tz kupitia huko kwa sababu uhuru kenya ulipokelewa na kundi ambalo halina taswira ya kitaifa bali jimbo/majimbo fulani. Awamu 1, jimbo1(Jomo Kenyatta), awamu ya pili jimbo2( Moi), awamu ya tatu jimbo 1(Kibaki), awamu ya nne jimbo 1 na mtoto wa raisi wa awamu 1(Uhuru Kenyatta).
Mamlaka ktk Kenya hazijawahi kutoka nje ya hayo majimbo mawili hivyo hata juhudi za kina Raila kwenye rainbow coalition walitumika tu ila hii ndiyo picha halisi.
TANZANIA INAHITAJI NINI KWENDA KWENYE HII SHIDA?.
Uhuru wa tz ulienda kwa wawakilishi wa kweli na wenye maadili ya utaifa kwanza. Imebaki hivyo mpaka sasa. Nyerere, mwinyi, mkapa na kikwete. Ndiyoo! wote ni TANU au CCM lakini at least huwezi kuwahusisha na jamii yoyote ya kitanzania kwani kila mtanzania anaweza kuingia na kukwea ngazi zote bila saana! kukwazwa na asili wala dini yake, labda kidoogo pesa.
Mnyonge mnyongeni ila haki yake mumpe, CCM imejaribu kutunza utaifa na usawa kwa kiasi kikubwa na kwa namna fulani hata demokrasia kiujumla, kuliko nchi zenye katiba zinazoonekana nzuri kwenye makaratasi lakini hazitekelezeki.
Unaweza kusema CCM haiwezi kuachia upinzani hivyo tz iko nyuma kidemokrasia! labda kweli lakini ikumbukwe kuwa watanzania wengi hata wa upinzani wanakubaliana mambo mengi sana hata ya kiuchumi na itikadi za siasa hadi kuna watu wengi sana wa upinzani wanakubaliana na serikali ya awamu ya 5 na kinyume chake.
Sioni nchi ya aina hii inahitaji kuelekea iliko kwa mfano Kenya etc., kufanya nini? mkondo wetu ni mwingine. Kuna vyama vikiongoza, tz inaweza kuanza kuzungumzia kuelea route ya Kenya ambayo sishauri ifuatwe.