Nairobi, Kenya: NASA wakijiandaa kumuapisha Odinga, bustani ya Uhuru Park imefungwa kwa muda usiojulikana

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Serikali ya Kaunti ya jiji la Nairobi nchini Kenya, leo Januari 24, 2018, imetangaza kuifunga bustani ya Uhuru Park kwa ajili ya matengenezo kwa muda usiojulikana.

Hilo linajiri zikiwa zimesalia siku sita tu kabla ya viongozi wa muungano wa upinzani nchini Kenya NASA kumuapisha kiongozi wao Bw. Raila Odinga kama Rais wa wananchi na Bw. Kalonzo Musyoka kama Naibu Rais wa wananchi. Hafla ambayo NASA walipanga kuifanyia katika bustani hiyo ya Uhuru Park.


Kulingana na ilani iliyotelewa kwa umma na kutiwa sahihi na Kaimu Karani wa Kaunti Leboo Ole Morintat, kwamba bustani ya Uhuru Park imefungwa kwa ajili ya matengenezo kwa muda usiojulikana, ili iweze kuwa na manufaa zaidi kwa wageni wanaoitembelea.
 
Ingekua Tanzania chadomo wangeandamana mpaka kuzimu Heheheh baba wa demokrasia Africa huyo anafanya vitu vyake
 
Odinga atulie tu. Yanini kutafuta mtifuano?
 
Waliopo madarakani,majizi,mabaguzi ya kikabira,waliopo upinzani,jinsi wanavyotoka mishipa ya shingo kwa kuongea kwa ajiri ya wananchi,unaweza ukafikiri ukiwapa madaraka,mambo yatakuwa mazuri,waaapi!na wao ni majizi na mabaguzi ya kikabira,ukiyapa nchi,yatafanya yaleyale yanayofanywa na jubilee,ubaguzi wa kikabira,na kikanda,
Yanaongea sana kwa sababu yamekosa ulaji,ktk uchaguzi uliopita,
Siku wananchi watakapo jua hakuna cha mluya,mluo,mkamba,mkalenjin,mkikuyu wala mmasai,
Zipo kabila mbili tu,aliye fukara/maskini,asiyeweza kuzifikia fulsa ili ajikwamua na shida za dunia,na wale wenye ukwasi wa kutisha,wao na familia zao,watu wanaomiriki ardhi kama mkoa mzima wa Dar,
MTU kama Raila,kwa rasilimali zote alizonazo,kitu gani amefanya cha kuwanufsisha watu,RAIA wa kawaida kiuchumi,kampuni ngapi,anamiriki,ameajiri watu wangapi,?
MTU kama Trump,ni bilionea wa real estate,makampuni yake yanatoa ajira,kwa watu kibao duniani,hawa wanasiasa wetu,kwenye elimu kubwa tu,ma Dr,Prof,ma engineer,nini wamefanya,mpaka tuwape nchi,wamevumbua nini,wana maono gani,au wanaona matumbo yao tu,
Mwalimu Nyerere,na Mandela,hawakuwa na Mali,lakini kwa uongozi wao,maono yao,walizijenga jamii,zikawa kama walivyotaka,TZ ilieshimika dunia nzima,likitokea jambo Africa nzima ilisubiri,TZ iseme kwanza,Nyerere huyo
Hawa wasasa HV wanataka madaraka tu,ili wale,nchi imeishapata Raisi,badala ya kujenga nchi,mnaendeleza siasa,uchumi unadolola,haya ni matumizi mabaya ya demokrasia,
 
Waafrika mkiitwa Shithole mnamaindi ili hali matendo yenu ysnadhihirisha huo ushithole.

Dunia gani kwa watu waliostaarabika yakatokea mambo ya kipuuzi kama haya!

sasa si tuwaulize hao mido inkamu... kwamba huyu rais mwingine atakaa ikulu ya wapi?? na msahafu wa nchi ipi? msahafu wa nchi una ruhusu kuapisha rais mwingine ndani ya muhula??
 
Odinga ana msongo mkubwa wa mawazo kwani ikopa ela ya kampeni akitegemea akishinda alipe sasa hajashinda hajui atazilipaje.

Sasa kavurugwa kabisa anamwambia Ruto ajiunge odm.
 
Kuapishwa Raila will set a precedent EA hadi maziwa makuu.
 
Odinga ana msongo mkubwa wa mawazo kwani ikopa ela ya kampeni akitegemea akishinda alipe sasa hajashinda hajui atazilipaje.

Sasa kavurugwa kabisa anamwambia Ruto ajiunge odm.
Umeona ee? Amesema ili Ruto awe rais lazima ajiunge na chama chake cha ODM. Hahahaa mbavu zangu! πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€ Huyu mzee anata kumnyang'anya Eric Omondi kazi yake laivu laivu.
 
Umeona ee? Amesema ili Ruto awe rais lazima ajiunge na chama chake cha ODM. Hahahaa mbavu zangu! πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€ Huyu mzee anata kumnyang'anya Eric Omondi kazi yake laivu laivu.
Na anaimudu kweli kweli.ongea yake tuu ni comedy tosha
 
***Mwalimu Nyerere,na Mandela,hawakuwa na Mali,lakini kwa uongozi wao,maono yao,walizijenga jamii,zikawa kama walivyotaka,TZ ilieshimika dunia nzima,likitokea jambo Africa nzima ilisubiri,TZ iseme kwanza,Nyerere huyo
Hawa wasasa HV wanataka madaraka tu,ili wale,nchi imeishapata Raisi,badala ya kujenga nchi,mnaendeleza siasa,uchumi unadolola,haya ni matumizi mabaya ya demokrasia***QUOTE]


Umenena vyema sana mkuu ndio maana wkt mwingine nashindwa kumlaumu Bw Shithole Countries
 
I'm waiting for a positive reaction from His Excellency President Kenyatta.
This is childish and cannot be tolerated once more.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…