Nairobi pachimbika...fujo baina ya wakenya na wasomali mitaa ya Eastleigh!

Nairobi pachimbika...fujo baina ya wakenya na wasomali mitaa ya Eastleigh!

Na mwengine huyu hapa anatia fitina na kujaribu kujenga chuki.
 
Mwingine yuko kule msimbazi anapiga domo.

Chuki za ubaguzi hazina nafas ktk nchi hii, hao Wakenya wanasukumwa na ubaguz jamani msiige huo ujinga, kwani huyu amewakosea nini?
 
mbona kuna wasomali ni raia halali wa Kenya iyo imekaaje?
 
mbona kuna wasomali ni raia halali wa Kenya iyo imekaaje?

Ndo hapo ambapo nashindwa kuelewa lengo la mleta mada. Uswazi kuna Wasomali kila kona, hoteli nyingi Kariakoo ni zao, maduka mengi ya kompyuta Kariakoo ni yao na ni wazaliwa wa hapahapa. Hawa nao mtawasukumizia Kismayu ama Mogadishu?
 
Si wasomali wote ni wauaji. Kikubwa ni uwezo wetu wa kuchambua punje na mchanga. Wako wanaokimbia kwao ajili wamechoshwa na matendo ya kinyama wanayofanyiwa. NI binadam hawa. Hatuhitaji kuwatupa. Mungu kawaumba kama sisi na wanahaki ya kujiokoa na kupata msaada wa kibinadamu kama binadamu yeyote mwingine. Kuwa wasomali hawakuomba lakini pia wanajutia sana kuzaliwa kule kulingana na vichaa wachache wanaoharibu ile nchi. Hawa tusiwatupe ndugu zetu. Na kwa jinsi ccm inavyoendesha nchi, bila Mungu kuingilia kati hali ya ukimbizi itatukumba sisi ama watoto wetu. Iondoeni ccm na hila zake.

Lakini pia wapo wasomali wabaya ambao wanatamani kueneza uharamia wao africa na dunia nzima. Nao wanaingia katika mkumbo ule ule wakijifanya ni waathirika wema kumbe ndio wadau wa uharibifu huko Somalia. Sasa inatakiwa intelligencia inayoweza kugundua alshabah watavamia maandamano ya CDM, iende mbele zaidi. Baada ya kujua kwamba wamepanga kuvamia maandamano ya CDM, inteligencia yetu isiishie hapo. Iende hatua moja mbele ya kuwakamata na kuwachukulia hatua. Kuwalea lea huku mnataarifa zao, msubiri wafanye uharibifu halafu ndipo mchukie wasomali wote, hapana. Mnapoona kundi la watu wanafanya uhalifu ama wanania ya uhalifu japo kwa nje wanaonekana ni wakimbizi, vikundi vya dini, siasa ama taasisi yoyote ya kijamii, ichuukuliwe hatua kali mara moja. Si watu wakuonea haya hawa. Si wema. Wameingia Somalia kama Al shabab, Nigeria Boko Haram, Taaliban, Alqaida na nini sijui. Matunda yao tunayaona. Sas Tanzania tunapoona mambo ya uamsho ama CUF sijui n ini, tusisubiri hadi waote mizizi ndio tuanze kuhangaika nao. Mara moja wachukuliwe hatua ikiwa ni pamoja na harakti zao kupigwa marufuku katika ardhi ya Tanzania. Lakini tusipofanya hivyo, tusije kujilaumu pale tutakapokuwa katika majanga kama tunayoyaona katika nchi zingine. UKICHEKA NA NYANI, UTAVUNA MABUA!
 
Hii ilikuwa ni juzi ambapo ilibidi polisi watumie nguvu kuvuia wananchi waliokuwa wanaandamana kutaka wasomali wote wafukuzwe kenya kutokana na kuchoshwa na milipuko na utekaji watalii. JE TANZANIA TUNASUBIRI MPAKA HAWA WASOMALI WATULIPUE NDIO TUSHTUKE?

Hauna tofauti yoyote na wale Waafrika kusini waliochoma moto wenzao (pamoja na Watanzania), Wasomali wa Tanzania wamekukosea nini? unajua kuna Watanzania wangapi wanaishi ugenini, nao Je wakifukuzwa huko waliko ni sawa?

Acha kutafuta vinsingizio na mchawi wa matatizo yako, jaribu kuyatatua mwenyewe!, Kwanza kama ni uhalifu na wizi watu wanaoiibia Tanzania sio Wasomali, ni wazungu wa kwenye migodi, mahotelini, vitaluni, n.k mbona hao hujawasema?

 
Wanaacha kushinikiza serikali yao kuacha kuingilia mambo ya ndani ya nchi huru ya SOMALIA kijeshi alafu waombe msamaha kwa WASOMALI. Alafu tuone kama milipuko itaendelea.

Huitaji kuwa jiniasi kufahamu hili la UVAMIZI WA KENYA NCHINI SOMALIA.

NASEMA TENA MBONA HAKUKUA NA HAYA MAMILIPUKO MIAKA 10 NYUMA?

KUWAFUKUZA WASOMALI NI KUKIUKA HAKI ZA BINADAMU SIKUBALIANI KWA HILI
 
Wakenya waache sumu ya ubaguzi maana wakianza na wasomali-wakenya, watakuja kwa wajaluo-wakenya, wagikuyu-wakenya na sumu hiyo itandelea na kuifanya nchi isitawalike.

Sisi Tanzania pia tuna wasomali-waTanzania ambao wengine ukiwauliza kwenu wapi watakwambia Arusha au Kilimanjaro hivyo tusitazame sura za watu na kuwahukumu kama wageni.
 
Tambueni kuwa hapo ni wivu tu maana islii ilikua eneo la chini haoa wasomali wameibadilisha kua eneo la kbiashara pia kenya ku mikoa 4 ya wasomali ss msihukumu tu kwa sababu ndg zao wanavita pia nahgalia

ogopa umasikini utalaumu hata kivuli chako mnyonge mnyongeni ila haki yake m[patieni
 
Tambueni kuwa hapo ni wivu tu maana islii ilikua eneo la chini haoa wasomali wameibadilisha kua eneo la kbiashara pia kenya ku mikoa 4 ya wasomali ss msihukumu tu kwa sababu ndg zao wanavita pia nahgalia

ogopa umasikini utalaumu hata kivuli chako mnyonge mnyongeni ila haki yake m[patieni

Sahihisha spelling kwenye bold na kwingineko tupate kukuelewa.
 
hawa Somalians ni watu hatari sana! Kenya imekuwa mwema kwao na kuwakaribisha sasa wanaivuruga nchi. Fukuzeni wote hao kabla Nairobi haijawa Mogadishu
Wasomali ni raia wa Kenya kama walivyo Wakisii,Wakale na wengineo kwa hiyo sio haki kuwa wafukuzwe,je waende wapi,ingekuwa ni Tz au UG ningekubaliana nawe sababu hatuna Wasomali ambao ndio asili yao kwa hizi nchi ,bali ni wahamiaji lakini si kwa Kenya,HAO MNAO MPAKA KUCHEE
 
Back
Top Bottom