Si wasomali wote ni wauaji. Kikubwa ni uwezo wetu wa kuchambua punje na mchanga. Wako wanaokimbia kwao ajili wamechoshwa na matendo ya kinyama wanayofanyiwa. NI binadam hawa. Hatuhitaji kuwatupa. Mungu kawaumba kama sisi na wanahaki ya kujiokoa na kupata msaada wa kibinadamu kama binadamu yeyote mwingine. Kuwa wasomali hawakuomba lakini pia wanajutia sana kuzaliwa kule kulingana na vichaa wachache wanaoharibu ile nchi. Hawa tusiwatupe ndugu zetu. Na kwa jinsi ccm inavyoendesha nchi, bila Mungu kuingilia kati hali ya ukimbizi itatukumba sisi ama watoto wetu. Iondoeni ccm na hila zake.
Lakini pia wapo wasomali wabaya ambao wanatamani kueneza uharamia wao africa na dunia nzima. Nao wanaingia katika mkumbo ule ule wakijifanya ni waathirika wema kumbe ndio wadau wa uharibifu huko Somalia. Sasa inatakiwa intelligencia inayoweza kugundua alshabah watavamia maandamano ya CDM, iende mbele zaidi. Baada ya kujua kwamba wamepanga kuvamia maandamano ya CDM, inteligencia yetu isiishie hapo. Iende hatua moja mbele ya kuwakamata na kuwachukulia hatua. Kuwalea lea huku mnataarifa zao, msubiri wafanye uharibifu halafu ndipo mchukie wasomali wote, hapana. Mnapoona kundi la watu wanafanya uhalifu ama wanania ya uhalifu japo kwa nje wanaonekana ni wakimbizi, vikundi vya dini, siasa ama taasisi yoyote ya kijamii, ichuukuliwe hatua kali mara moja. Si watu wakuonea haya hawa. Si wema. Wameingia Somalia kama Al shabab, Nigeria Boko Haram, Taaliban, Alqaida na nini sijui. Matunda yao tunayaona. Sas Tanzania tunapoona mambo ya uamsho ama CUF sijui n ini, tusisubiri hadi waote mizizi ndio tuanze kuhangaika nao. Mara moja wachukuliwe hatua ikiwa ni pamoja na harakti zao kupigwa marufuku katika ardhi ya Tanzania. Lakini tusipofanya hivyo, tusije kujilaumu pale tutakapokuwa katika majanga kama tunayoyaona katika nchi zingine. UKICHEKA NA NYANI, UTAVUNA MABUA!