Japo this tusan guy ni nafuu kidogo, huchanganya changanya, kuna wakati anatiririka pumba mtupu, lakini wakati mwengine anakua na mambo yenye tija.
Lakini kuna wengine kutwa kuponda Kenya kwa kila kitu na cha kushangaza hutawaona sehemu yoyote JF kwenye mada za Kitanzania. Walau akina barbarossa utamwona leo ameibukia mada za Kenya baadaye utamwona kule kwa siasa na taarifa za Bongo akijadili na Watanzania wenzake.
Wale hukomaa na Kenya huwa naona kuna kitu kiliwatendekea kwetu, aidha walifukuzwa Kenya wakaishia kuwa na majungu miaka yote. Lazima kuna kitu maana sio kawaida. Yaani hutomkuta hata siku moja anajadili matukio ya kwao na kwa jinsi yalivyo mengi siku hizi ya akina Roma Mkatoliki, Gwajima, Dai, Bashite n.k. Hutawaona huko hata siku moja, lakini wacha Kenya itajwe kwa lolote, wanatiririka kama nzi.