Ndugu wanamichezo wenzangu, nimefikiria na kuja na wazo kuhusu timu ya Azam, kama itawezekana basi viongozi wa Azam wafikirie kuinunua timu ya Pan Africa na jina la timu iwe Azam Pan Africa.
Sababu kubwa ya kufanya hivyo ni kwamba Pan Africa bado ipo na ina mvuto lakini uwezo wa kujiendesha hadi kufikia kiwango cha juu ni mdogo sana.
Ikumbukwe kuwa Pan bado ina wapenzi wengi, kwa upande wa Azam wao wana uwezo wa kupata mahitaji yote lakini wanakwama sana katika kufikia malengo na kupata wapenzi kindakindaki.
Kwa hivyo basi muunganiko wa Pan na Azam utaifanya timu kuwa na uimara na hasa katika uwakilishi na kuchukua ubingwa mbalimbali.
Napenda kuwakilisha.