GE2025 Naishauri Serikali na wananchi yafuatayo baada ya uchaguzi kumalizika

GE2025 Naishauri Serikali na wananchi yafuatayo baada ya uchaguzi kumalizika

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

mwenye shamba

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2015
Posts
1,031
Reaction score
1,900
Ndugu watanzania wenzangu, kwanza nitoe pole kwa watanzania wote kwa yale yaliyotokea.

Nikiwa kama mtanzania nina haki ya kuishauri serikali yangu na wananchi wenzangu yafuatayo.

(Neno langu sio sheria na siwezi kuwa sahihi kwa yote)

1. Serikali na chama cha mapinduzi (CCM) wajitafakari kwa haya yaliyotokea kwa kufanya yafuatayo

A. Kuwaomba radhi watanzania kwa mauaji yaliyotokea

B. Kuwapa watu haki ya kuzika watu wao ili angalau mioyo yao isiumie mara mbili.

C. Kuacha kabisa kauli na matamko ya kibabe kwani kwa kipindi hiki watachochea zaidi chuki na hasira za wananchi

D. Wahakikishe wanasiasa walioko mahabusu wanaachiwa mara moja.

E. Isiwapuuze vijana na ihakikishe kila inapoona kuna dalili za hasira ya umma basi isizipuuze hasira hizo na badala yake iwasikilize na kuwatekelezea hayo wanayoyahitaji hata kama si yote.

F. Jeshi la polisi wajitoe kwenye matumizi ya nguvu na badala yake waangalie katiba na sheria za nchi, vinginevyo wataendelea kuchukiwa na umma zaidi na zaidi.

G. Serikali ijikosoe yenyewe,lazima ikili makosa yake na ijiunde upya iwe na nguvu ya raia na si mafisadi.

H. Wana CCM wote waachane na habari za mapambio na kusifu kila kitu hata vile vya kukosoa

2. Sisi wananchi nasi tufanye yafuatayo.

A. Tusiwaamini sana hawa wanaharakati hususani walioko nje, ni ukweli usiopingika kuwa wanao ushawishi wa kutosha lakini si wa kuwaamini katika kila jambo.

Machale ya wengi yanawaona kama watu wanaotumiwa na wengine kwa maslahi ya wengine,ila tusiwapuuze kwenye kila agenda.

B. Raia tuisamehe serikali yetu kwa haya maovu iliyoyatenda maana ni ukweli usiopingika kuwa hawa watu wametukosea sana.

C. Tuipende nchi yetu,hususani hiki kipindi,ni nyakati ambazo tusipoamua kwa akili tutajikuta tunapata adui mwingine anaitwa UASI na tutajikuta tunacheza mziki wa risasi kila siku.

NENO LANGU SIO SHERIA
 
Back
Top Bottom