Naitafuta muvi hii hata sijui inaitwaje

Naitafuta muvi hii hata sijui inaitwaje

Hivi ile iliokuwa inaonyeshwa Chanel 10 mchezo wa kuigiza kuna binti kipofu halafu kuna nyimbo inaimba "haya daima Mapito haya kwetu mapito"
Inaitwaje?
 
Hiyo Movie inaitwa TAMARI na
ina kithemes chake kinaimbwa
[emoji445] ukiwa na tamari eeeh maisha yako ya fahari[emoji445]
Moja kati ya MOVIE zilizothaminiwa na mashirika ya umoja wa mataifa
Movie nzuri inakumbusha mazingira ya zamani posta ilivyokuwa mausha halisi ya watanzania na inaonesha mazingira halisi ya tanzania ilivyokuwa hasa setting ya mwisho milimani MOROGORO msamvu edhi hizo
 
Muvi hii ni ya kiswahili niliiangalia muda mrefu sio bongo muvi ni zile muvi nadhani zinafadhiliwa na wahisani.nakumbuka sehemu chache sana kwenye hiyo muvi.kuna watoto wawili wa kike na wa kiume mama yao alikufa au aliachwa na baba yao,baba akawa akaoa mwanamke mwengine, yule mwanamke akawa anawatesa wale watoto mwishowe wakakimbilia mitaani.yule wa kike baadae alipata kazi ya uhausigeli kwa mama mmoja,lakini mume wa yule mama akawa anataka kumrubuni yule mtoto afanye nae mapenzi.

Mama yule mwenye huyo mume siku alimfuma mmewe akivutana na yule mtoto,yule mama akamfukuza yule mtoto,na mtoto akarudi mtaani,kuna sehemu yule mtoto anaonekana yuko na makahaba.Mwishoni mwa muvi kaka yake na huyu mtoto alikamatwa na polisi kwa kujihusisha na uwizi dada yake akawa analia.Ni sehemu hii tu ndio nakumbuka.Katika muvie hii kuna wimbo wanaimba "maisha,maisha,maisha".sijui hii muvi inaitwa neria au?sina uhakika.
TVT ndio walikuwa wakipenda sana kuionyesha hiyo movie
 
Hiyo Movie inaitwa TAMARI na
ina kithemes chake kinaimbwa
[emoji445] ukiwa na tamari eeeh maisha yako ya fahari[emoji445]
Moja kati ya MOVIE zilizothaminiwa na mashirika ya umoja wa mataifa
Movie nzuri inakumbusha mazingira ya zamani posta ilivyokuwa mausha halisi ya watanzania na inaonesha mazingira halisi ya tanzania ilivyokuwa hasa setting ya mwisho milimani MOROGORO msamvu edhi hizo
Ipi mkuu inayoitwa tamari aliyoiulizia jamaa hapo juu yako au niliyoiulizia mimi
 
Ipi mkuu inayoitwa tamari aliyoiulizia jamaa hapo juu yako au niliyoiulizia mimi
Hiyo uliyouliza inaitwa tamari na huyo msichana dadaake JUMA anaitwa TAMARI

Mwishoni BABU wa kijiji yupo mjini POSTA katika mizunguko yake TAMARI anamuona anamuita babu then huyo babu anamnunulia chips pale pembezoni mwa bank ya NBC kipindi hicho daladala za ubungo kimara mbezi zinapack mbele ya bank ya NBC

Babu anarudi na TAMARI morogoro kisha yule mzee anatoka na babajuma wanakwenda mjini kumtia gerezani juma
Tunaoneshwa wapo katika mnyama ABOOD scania matata wanakuja dsm kumfata juma

Mwusho movie inaishia kwenye kikao cha kijiji MOROGORO baba juma na mamajuma wanapatanishwa

ama siyo hiyo mzee baba
 
Ndio hiyo mwamba
 
Hamna mwenye muvi hii anipatie au aniunganishe niipate
 
Umeambiwa nenda ofisi za TBC kitengo cha maktaba 😎
Yaani nifunge safari toka huku nilipo nitumie takribani 150,000 kwenda tu TBC kwa ajili ya movie.Are you serious?
 
Back
Top Bottom