Naitafuta muvi hii hata sijui inaitwaje

Hivi ile iliokuwa inaonyeshwa Chanel 10 mchezo wa kuigiza kuna binti kipofu halafu kuna nyimbo inaimba "haya daima Mapito haya kwetu mapito"
Inaitwaje?
 
Hiyo Movie inaitwa TAMARI na
ina kithemes chake kinaimbwa
[emoji445] ukiwa na tamari eeeh maisha yako ya fahari[emoji445]
Moja kati ya MOVIE zilizothaminiwa na mashirika ya umoja wa mataifa
Movie nzuri inakumbusha mazingira ya zamani posta ilivyokuwa mausha halisi ya watanzania na inaonesha mazingira halisi ya tanzania ilivyokuwa hasa setting ya mwisho milimani MOROGORO msamvu edhi hizo
 
TVT ndio walikuwa wakipenda sana kuionyesha hiyo movie
 
Ipi mkuu inayoitwa tamari aliyoiulizia jamaa hapo juu yako au niliyoiulizia mimi
 
Ni movieza wahisani kuna iyo kuna sindonga
 
Ipi mkuu inayoitwa tamari aliyoiulizia jamaa hapo juu yako au niliyoiulizia mimi
Hiyo uliyouliza inaitwa tamari na huyo msichana dadaake JUMA anaitwa TAMARI

Mwishoni BABU wa kijiji yupo mjini POSTA katika mizunguko yake TAMARI anamuona anamuita babu then huyo babu anamnunulia chips pale pembezoni mwa bank ya NBC kipindi hicho daladala za ubungo kimara mbezi zinapack mbele ya bank ya NBC

Babu anarudi na TAMARI morogoro kisha yule mzee anatoka na babajuma wanakwenda mjini kumtia gerezani juma
Tunaoneshwa wapo katika mnyama ABOOD scania matata wanakuja dsm kumfata juma

Mwusho movie inaishia kwenye kikao cha kijiji MOROGORO baba juma na mamajuma wanapatanishwa

ama siyo hiyo mzee baba
 
Ndio hiyo mwamba
 
Hamna mwenye muvi hii anipatie au aniunganishe niipate
 
Umeambiwa nenda ofisi za TBC kitengo cha maktaba 😎
Yaani nifunge safari toka huku nilipo nitumie takribani 150,000 kwenda tu TBC kwa ajili ya movie.Are you serious?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…