Naitwa Analyse, na hii ndio safari yangu ya maisha...

Naitwa Analyse, na hii ndio safari yangu ya maisha...

Inaendelea.....


...Mwenyeji wangu hakupatikana hadi kunakucha. Usiku huo ilibidi nijilaze mle mle stand ya mkoa. Na hata asubuhi nilipomtafuta, alipongundua ni mimi, mtandao ukaanza kuzingua. Mara hanisikii vizuri. Simu hakupokea tena, na mimi nikaamua kuachana nae.

Nilitoka nje ya stand,nikawa natembea tembea tu bila kujua naenda wapi. Mida ya mchana nikajakustukia nipo eneo linaitwa Tabata. Njaa kali, sina hela. Kiufupi sina kitu chochote cha thamani. Nikaingia kwa mama ntilie, nikamlilia shida nione kama atanisaidia, akagoma. Nikamwambia hata nifanye kazi yoyote nipate hata ukoko. Akanijibu, kazi zipo, ila msosi wote una order yani hadi huo ukoko. Nikaishia kunywa maji kisha nikaondoka.

Usiku ukapita bila kula chochote zaidi ya maji. Kesho yake ikakata tena bila chochote. Kwanza sina sehemu maalumu, natembea tu bila kujua naenda wapi, cha msingi naenda mbele. Ilipofika siku ya pili usiku, nikaona kabisa hapa nakufa. Maana mwili haukuwa na nguvu hata kidogo, ukiomba msaada unaishia kupewa maji, tena na yenyewe ni baada ya kuulizwa maswali kibao.

Sijui akili au ujasiri ulitoka wapi, ila nakumbuka kuna sehem inaitwa Vingunguti, njiani niliokota kava la simu jeusi. Baada ya kuwa na lile kava, nikatafuta kiroba cha unga kilocho tupu, ndani nikakiweka mawe kadhaa na mabox, alaf nikaingia kwa mama ntilie. Nikauliza chai ipo? Akasema ipo, chapati nazo zipo? Akajibu zipo. Huku natetemeka na moyo unadunda kuliko maelezo, nikamwambia " Naomba chai ya maziwa na chapati 5"

Zikaletwa, nikazipiga, nikaongeza na chai. Chapati zilipoisha na chai ipo nusu. Nikatoa kava la simu na kujifanya naongea na simu huku nasogea nje ya kibanda, hapo ule mzigo wangu nimeuacha pale ndani. Nikasimama mlangoni huku naongea "Me nishafika, na mzigo ninao hapa, njoo na usafiri unichukue maana nataka kuondoka"... Nilipoona yule mama ntilie hanifatilii, nikazidi kusogea mbele, nilivyokata kona tu, nilitoka mbio sio za nchi hii. Sijui kule ilikuwaje,na sikuwahi kurudi tena.

Kulipokucha nikaendelea kutafuta kibarua. Nikafanikiwa kupata kwa wale wafyatua tofali kwa mashine. Zikifyatuliwa tu,unabeba fasta na kwenda kupanga sehemu. Speed,uzito wa tofali,inama inuka jumlisha kuwa sijapata msosi wa uhakika kwa siku kadhaa...nilipatwa na kizunguzungu nikaanguka na tofali la watu. Bosi aliwaka kichizi. Akasema nimlipe. Sina hela,ikabidi nimwambie kwa uungwana akate hela yake ktk posho yangu alaf anipe iliyobaki ambayo nastahili kupata kwa kazi ambayo nishafanya. Boss akasema makubaliano ni ufanye kazi siku nzima,kwa muda huu mchache uliofanya sina cha kukulipa,kwanza ushanitia hasara,SEPA.


Ikabidi niondoke.

•••••••••• ••••••••••••• •••••••••••••• •••••••••••••••••

Mungu si Athumani, katika kuendelea kujielezea kwa watu niliokuwa nakutana nao nilibahatika kupata kazi ya kusimamia ng'ombe wa mzee mmoja maeneo ya tabata. Dar majani hakuna, unayatafuta kwa tabu sana, alafu mzee akawa anasumbua malipo. Sema hakuna jinsi, si nilikimbia kusoma Vishazi?.

Nakumbuka siku moja katika pita pita natafuta sehemu ya kukata nyasi, nikakuta Don mmoja bomba la maji limepasuka nje ya fensi yake, na maji yanavuja sana. Akaniita na kuniuliza kama namfahamu fundi bomba yoyote maeneo yale.. Bila kuvunga ikabidi nijifanye fundi bomba. Yule Don akaniambia sasa hapa inabidi uwe na konekta , tunazipataje? Nikaropoka "itabidi tununue, moja inauzwa 7000" ila kiukweli hata sikuelewa hizo konekta ndio nini na bei sijui. Jamaa akasema mbona unataja bei kubwa hivyo? Ngoja nikuelekeze sehemu wanapouza kwa 6000. Akanielekeza kisha akanipatia hela. Ila kabla sijaondoka akaniuliza ninapokaa. Nikamuelekeza akapajua.

Baada ya kununua zile konekta, nikarudi, nikachimba sehemu iliyopasuka. Ili niweze kupaunga, ikabidi nikate bomba. Presha na wingi wa maji vikanizidia, nikaanza kutetemeka pale. Kila nikitaka kuziba, maji hayo. Yule Don ikabidi aniulize "Hivi ww ni fundi kweli?.. Na jibu nini kwa mfano? Bahati nzuri simu yake ikaita, aliongea kidogo alaf akaondoka eneo lile. Hapo na mm akili ikarudi, maana kusimamiwa kulinitoa mchezoni. Nikapata wazo la kutumia moto kutanua bomba, alaf nikayazungushia na mifuko ya nailoni, mwisho nikabana na mpira . Maji yakaacha kutoka,zile konekta nikaweka mfukoni maana sikuzitumia. Nikafukia, nikamuita yule Don, akapaangalia na kuridhishwa ila akasema hela nifate kesho ili aangalie kama kweli zoezi limefanikiwa kwa 100%.

Kesho yake mapema sana, yule Don akaja home pale kumuulizia fundi bomba (mimi). Inaonekana usiku presha ya maji ilizidi pakafumuka. Sasa yule mzee ninayekaa nae anashangaa mimi kuitwa fundi bomba. Ikabidi amwambie ukweli yule Don kuwa mimi sio fundi. Hapo nishasemwa sana. Ikabidi aitwr fundi kweli, nikawarudishia konekta zao. Sema yule Don akaniambia ukiwa na shida unasema, sio unajitwika majukumu sio yako utakuja kupata matatizo mjini hapa, akanipa elfu 5 nikasepa..

Nikaendelea na kazi ya kulisha mifugo kwa yule mzee. Ila mkewe alikuwa na nongwa sana. Ukiacha kazi za mifugo,alikuwa ananipa kazi ya kufulia nguo wanae, kudeki, kumwagilia bustani, kusafisha mtaro uliokuwa nje ya nyumba. Pia kuna siku akataka nimfulie nguo zake yeye sidiria, nguo za kulalia na tight. Niligoma kufua, akaongea sana. Na kumbuka akatoka kwa hasira. Sijui alisahau nini ndani , akarudi na kunikuta napiga deki, nilipomuona na mm ndio nikamwaga sabuni ya unga na maji kwenye zile malumalu. Kaja na hasira, alipiga mwereka sio wa nchi hii,alijibamiza chini hadi nikamuonea huruma. Usiku wa siku hiyo ndio ilikuwa siku ya mwisho mimi kufanya kazi na kulala kwenye nyumba hiyo...
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] ubanifurahisha kuna visehemu huna haja ya kuandika kireeefu unarukia hitimisho tu

Mfano....."alijibamiza chini hadi nikamuonea huruma. Usiku wa siku hiyo ndio ilikuwa siku ya mwisho mimi kufanya kazi na kulala kwenye nyumba"

Wala hujajisumbua alivyojibamiza sijui akafoka akasema atamwambia mumewe na mumewe alivyokuja sijui ikawaje na blah blah kibao

Kongole mwana, pamoja
 
Nilizaliwa miaka kadhaa iliyopita. Katika familia ya watoto 7,mimi nilikuwa wa 6.

Kama watoto walivyo, nilikuwa mtundu kiasi ila sio mtukutu. Nakumbuka nikiwa darasa la 5,niliitwa mbele na ticha nikafanye swali la hesabu. Nikafanya swali kwa mbwembwe, nilikuwa nasumbuliwa na mafua, kabla sijaondoka pale mbele nikatoa leso ili nijifute. Wakati naitoa, kibox cha condom kikaanguka, darasa zima full kicheko. Ticha wa mathe ndio ticha wa nidhamu..nikaambiwa nitangulie ofisini.

Nikala bakora zangu za kutosha, kisha ndio nikaombwa maelezo, kila nikijitetea hawanielewi. Ukweli sio kwamba nilikuwa na dem au nilishaanza mapenzi, ni ile tu utoto utoto, unaokota kibox cha condom alaf unakaa nacho uangaliage zile picha. Kesi iliisha baada ya mzazi kuitwa.

Miaka ikakata, siku zikaenda. Darasa la saba mwishoni, wakati natoka kujisomea nikiwa na wenzangu wawili, ghafla tukasikia miguno kwenye darasa moja, kuchungulia tunakuta mlinzi wa shule yupo na muuza ubuyu [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]. Jamaa akatukimbiza maana ndio alikuwa
anajiandaa kupiga show alaf tumemtibulia.

Kitoto toto, tunakimbia huku tunacheka, nikaenda kuliparamia lori la mchanga wakati navuka barabara. Nikapelekwa hospital na kushonwa nyuzi 18,maana nilipasuka kichwani na usoni. Nikauguza majeraha, baada ya miezi kadhaa nikapona.

Baada ya kumaliza la saba, wazee wakaona nisisome shule za day, wakaamua kunipeleka seminari huko mkoani Iringa, mbali kabisa na mkoa wangu. Sijawahi ona shule ambazo wako strict kama seminari. Sema siku zikakata pia, wakati nipo kidato cha 3,hata mawazo sijui yalitokea wapi, me na rafiki yangu Shedy tukapanga tuuze nguruwe wa kanisa. Nakumbuka tulivibana vizuri ili visitoe sauti (vitoto viwili),kumbe wakati tunaishia, kuna sister akatuona (aliutambua mzura wangu). Wala hatukupigwa, tuliambiwa tutaje tulipowapeleka ili tusamehewe. Tukataja, wakafatwa. Tukashangaa wik end wazazi wetu wamefika, wakakabidhiwa barua zetu za kufukuzwa shule, tukaambiwa tusepe.

Mshua aliongea sana siku hiyo, njia nzima hadi tunafika home. Kwanza hakuninunulia chochote cha kula njiani, maji nilikunywa kwavile yanatolewa ndani ya bus. Kufika home,ilifanywa mipango nikajiunga na shule fulani ya private ili nimalizie O level. Nikiwa kidato cha 4,me na mdogo wangu ndio tukafanya ule msala wa kumfungia dingi kwa nje,alaf tukala ndizi zote..

Kufupisha,fatisha hii link kusoma kilichotokea maana nilishawahi kuandika hiki kisa:



Nikamaliza form 4,majibu yakatoka. Nakumbuka nilipata 3 ya mwisho mwisho huko. Nilikuwa napenda sana hesabu,ila cha ajabu nilipataga D. Na post zilivyotoka nikapangiwa HKL. Afadhali History,sikuwahi kulipenda somo la Kiswahili wala English,leo hii nikasome vishazi na ngeli shurutia ambazo nilivutwa sana masikio lakini sikuzielewa? Nikampanga faza anipeleke private Advance, akagoma. Msimamo wangu ukabaki me HKL siwezina sitaki. Faza akakausha. Baada ya wiki akaniita, akaniambia kati ya vitu viwili kimoja lazima nikiweze "KUSOMA HKL AU KUJITEGEMEA". Kikao kikaishoa hapo, nikaambiwa nikafikirie.

Nikiwa peke yangu chumbani, nikawa natafakari mavitabu, tamthilia, riwaya, ushairi ntakayoenda kusoma Advance, nikaona ngoma nzito ikiwa Mabala the Farmer kilikuwa kinanitoa jasho. Wiki moja baadae mshua akaniita tena, akanipigia hesabu zote za gharama zinazohitajika kuanzia nitakapoenda shule, alaf akanikabidhi cash pamoja na joining instructions ya shule. Akasema

"Vitu vyote utakavyohitaji kununua vimeandikwa humo na hela hii hapa, shule inafunguliwa tarehe 21,itakapofika siku hiyo nisikuone hapa kwangu, either uende shule au hiyo hela iwe mtaji wako wa kuanzia maisha"

Kikao kikaishia hapo. Ndani naona hapakaliki, nikaenda uwanjani kuangalia mpira ili kupoteza mawazo. Siku kama mbili mbele nikiwa nimekaa na washkaji, zikaanza story kuhus Dar es salaam. Kwamba ukijituma, na kuwa mjanja mjanja unafanikiwa. NIKAPATA WAZO LA KWENDA DAR.

Tarehe 15 /05 nikapanda bus kwenda Dar. Kabla sijatoka toka, Maza aliniuliza kama naenda shule, nikamwambia hapana, nachukua uelekeo mwingine.


Nakumbuka Dar es salaam tuliingia mida ya saa tano usiku. Bus ilisimama nikaona watu wanawahi kushuka, na mimi nikabeba vitu vyangu nikashuka. Kufika chini nauliza hapa ndio ubungo? ( Ndio sehem pekee niliyokuwa naijua) . Jamaa akanijibu "Hapa Mbezi dogo". Nikapaniki. Ikabidi nitafute sehemu nikae chini nitafakari vizuri. Kuna gari ilikuwa imepaki, nikakaa kwa chini, nikijiuliza nafanyaje.

Nilikuja kugundua badae chini ya lile gari kumbe kuna watu ndio sehemu yao ya kulala, na niligundua baada ya kile kifurushi changu nilichoweka chini kutoweka "NILIDATA"

•••••••• •••••••••• •••••••• •••••

Kwenye kile kifurushi ndio kulikuwa na nguo zangu pamoja na hela. Nikajaribu kuulizia, hakuna aliyenijali, naishia kutukanwa tu kuwa nawarushia stimu.

Mpaka kuna kucha, sikuupata mzigo wangu. Kuna Mzee mmoja ndio alinionea huruma akaninunilia chai na kunipa nauli ya kunifikisha ubungo, maana jamaa aliyetarajia kunipokea ilibidi nikutane nae ubungo. Kwavile namba zake nilikuwa nazo kwenye karatasi, niliongea nae kwanza kupitia simu ya yule mzee na kumuelezea kwa ufupi yaliyotokea.

Nikapanda daladala hadi ubungo. Kufika, nikaingia hadi ndani mule, nikaazima simu ya mtu, nikampigia tena jamaa yangu kumwambia kuwa nimefika. Wakati namsubiria, nikajiegesha sehemu.

Nikiwa pale, nilishuhudia tukio ambalo siwezi kuja kulisahau. Mbele yangu kulikuwa na Mwanaume wa makamo, kwa mavazi yake ni kama mchunganji, alikuwa anaongea na simu. Akatokea mtu mwingine kwa nyuma yake amebeba makaratasi kibao,ameyabana kwapani huku akiwa anakunywa maji ya uhai, yalipobaki nusu akaenda na kuyamwaga nyuma ya yule mchungaji, kisha akasubiri. Mchungali alipomaliza kuongea na simu, lile jamaa likamuuliza "Nani aliyekuruhusu kukojoa eneo ili?"

Mchungaji akashangaa, nahisi akumuelewa jamaa, ila alipotaka kuondoka, wakaongezeka wengine. Kuna mmoja akampiga kofi, yule aliyemwaga maji akamuuliza " Yani unakojoa eneo la wazi alafu unakuwa mkali?, Twende nae ofisini" Mchungaji akapaniki, wakamwambia atoe faini au akalale ndani. Mchungaji kujisachi, hela hana, atoe simu ili ampigie ndugu yake, simu hakuna. Mchungaji akalia. Ikabidi waazime simu, akampigia ndugu yake ili aje na hela ya faini.

Japo mchungaji alidata, ila mimi nilidata mara 100 zaidi yake. Ikabidi niweke vocha kwenye simu ya mtu tena, piga sana namba ya mwenyeji wangu ila haipokelewi, mwisho wa siku ikawa haipatikani tena. Kucheki muda,saa moja kasoro usiku. Nikazidi kudata.....



***** ***** ******* ******* ******

Imeendelea post #27

Imeendelea tena post #68

Imeendelea tena post #137


Imeendelea tena post #177
Bado inaendelea nimeishia 177#
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] ubanifurahisha kuna visehemu huna haja ya kuandika kireeefu unarukia hitimisho tu

Mfano....."alijibamiza chini hadi nikamuonea huruma. Usiku wa siku hiyo ndio ilikuwa siku ya mwisho mimi kufanya kazi na kulala kwenye nyumba"

Wala hujajisumbua alivyojibamiza sijui akafoka akasema atamwambia mumewe na mumewe alivyokuja sijui ikawaje na blah blah kibao

Kongole mwana, pamoja
Thanks man. Najaribu kufupisha isiwe ndefu sana.
 
.... Fursa nyingi mwanzoni huwa na changamoto, lakini fursa ya hazina ya mjerumani ina zaidi ya changamoto. Tulifika hadi Nyasa. Ulizia sana alipo huyo mzee, maana huyu jamaa sio kusema kwamba alikuwa anajua pakumpata, na yeye alisikia tu habari zake. Tulizunguka sana kwenye vijiji vya kule, mwisho wa siku tukafanikiwa kuelekezwa hadi nyumbani kwake kabisa. Tulipokelewa vizuri, tukaeleza shida yetu, wakatuelewa. Wakatwambia hizo habari mnazoziongea kuhusu mzee ni za kweli, ila zinaendelea kuenezwa kila siku japokuwa mhusika mwenyewe (yule mzee) ameshafariki yapata mwaka sasa. NIKACHOKA.

Ikabidi tuondoke, tukiwa njiani kuna mzee mwingine akatudaka. Akasema kama shida yenu ni hiyo naweza kuwasaidia. Ikabidi tumskilize. Tukafika kwake, nae akatupa maelezo ya kina. Kisha akatwambia, kama kweli mmezamilia kuzitafuta hizi hazina, basi kuna vitu muhimu inabidi muwe navyo. Cha kwanza inabidi muwe na vichaa/matahira wawili, hawa watawasaidia kuwakinga kipindi mnaingia kufukua hazina, alaf kitu cha pili inabidi muwe na Mjerumani au Muisrael kwa ajili ya kutafsiri baadhi ya mambo.

Kwangu masharti yote mawili niliyaona magumu, tena sana. Namtoa wapi mjerumani au muisrael? Pia hao vichaa, sawa hata tukiwapata, ni vipi tutaweza kuwadhibiti tukiwa nao (maana vichaa wanajulikana mambo yao),mnaweza mkaona hazina, yeye ghafla akatimua mbio, sasa kama wao ndio kinga, hapo tufate hazina au tuwakimbize? Na bora angekuwa mmoja, wapo wawili. Vipi kila mmoja akikimbia na njia yake?

Nadhani yule mzee aliona wasiwasi wangu, akasema msiwe na shaka vijana, nitawasaidia hayo mambo yote mawili, cha msingi muwe na kiasi cha pesa hata kidogo. Nikasema sawa mzee, pesa kidogo ipo. Vizuri, basi leo pumzikeni kwavile mmetembea umbali mrefu sana hadi kufika hapa, tusubirie kesho asubuhi tuanze mchakato wenu uliowaleta. Alitufanyia mpango wa msosi, tukala. Mzee pamoja na umri kwenda ila alikuwa anaishi peke yake, kibachela. Hakuwa na kitu cha thamani zaidi ya dhana za kilimo.


Kesho yake tulichelewa sana kuamka, sijui ni sababu ya uchovu au vipi. Nakumbuka tuliamka kwenye mida kama ya saa nne hivi. Pako kimya kabisa, wanaskika ndege tu. Katika safari yetu, mimi nilikuwa na begi la mgongoni, jamaa yangu nae hivyo hivyo, sema lake lilikuwa dogo kidogo. Ila cha ajabu asubuhi hiyo tulikuta mabegi yote yapo wazi, vitu vimetupwa tupwa ovyo. Kuangalia vizuri, hela hakuna na mzee hayupo. Baharia wa nchi kavu nimelizwa. Aisee nilitamani kulia. Kilichonisaidia, huwa nikiwa ugenini hela zangu siweki zote sehemu moja. Nakumbuka kuna baadhi zilikuwa kwenye begi, zingine kwenye mfuko wa suruali, na nyingine niliweka kwenye viatu (nilitoa kapeti la ndani ya kiatu, nikaweka mtonyo alafu nikalirudisha). Nilifanya hivyo kwenye viatu vyote viwili.

Yule Mzee mpaka leo naamini ujana wake aliulia Dar es salaam. Maana hela za kwenye begi aliziona, za kwenye suruali aliziona na za kwenye viatu aliziona. Sema za kwenye viatu alichukua kwenye kiatu kimoja, nahisi baada ya kukuta hela kwenye kimoja hakufikiria kama ningeweza kuweka na kwenye kingine. Jamaa yangu yeye alipigwa zoote.

Ikabidi tutoke nje tunaita, ila hamna kitu. Ikabidi tuchukue vitu vyetu tusepe. Njiani ni mashamba tu, bahati nzuri mbele tukakuta familia inalima. Tukajaribu kuwaelezea mkasa wetu. Tulivyowaelekeza nyumba tuliyokuwa pamoja na yule mzee alivyo, bahati nzuri wakamjua. Wakatwambia ile ni nyumba ambayo hutumiwa kipindi cha mavuno au wakati wa kulima, ila haikaliwi na mtu. Wakatuelekeza anapokaa. Tukamfata.


Fika mpaka kwake, tukamuulizia, wakatuelekeza yupo kilabuni, tukaelekezwa tukaenda. Pale kilabuni mzee tulimkuta yupo chakali, ashalewa pombe zao za kienyeji zile. Anatuuliza mnasemaje? Nilikuwa nimefura kwa hasira, nikamwambia Mzee tunasafari ndefu, tupe hela zetu tusepe. Kwa sauti ya kilevi mzee anasema hela ameshalipia madeni, iliyobaki ndio ile ameinunulia pombe, hana kitu labda na sisi tukae tunywe.

Nilimwangaliaa yule mzee wee, ila nkakosa cha kumfanya. Mzee ikabidi atuchane ukweli, robo ya ujana wake ameipotezea kwenye kusaka hazina ya mjerumani, na mpaka anazeeka hajawahi hata kuiona picha ya hiyo pasi ya Mjerumani. Mwishoni akatwambia "Nimepoteza hela nyingi sana vijana wangu kwenye kusaka hizo hazina, nimedhurumiwa mara nyingi sana, tena nyie mnabahati walau niliwapa hata chakula, mwenzenu hata maji nilikuwa sipewi na hela inaenda, hii hela fanyeni kama mmelipia twisheni tu ya maisha, nyie vijana bado mnanguvu mtapata zingine"

Hasira tuliyokuwa nayo sijui niielezee vipi, Mzee nae anatuangalia kilevi, hana hata chembe ya wasi wasi. Ikabidi tusepe tu, hakuna namna.

*** *** *** *** *** *** ***

Kufika town jamaa ananiuliza tunafanya nini kutokea hapa? Nikamwambia sina cha kufanya na wewe, we endelea tu na harakati zako (Hasira za kupoteza hela nyingi kwa wakati mmoja zilikuwa bado zipo kichwani).

Nikarudi kwenye kufanya vibarua vyangu huku natafakari kitu cha kufanya. Kuna siku likanijia lile wazo " Kama mnataka mali, mtazipata shambani". Nikaamua kujikita kwenye kilimo. Amini na kwambia "KAMA UNATAKA STRESS, BASI UTAZIPATA SHAMBANI" maana kama hujaparalaizi basi unaweza ukafa kabisa.


Maisha ni safari,kuna mnaosafiri kwa ndege,wengine kwa miguu,ila wote tunaelekea sehemu moja. Usitishwe na umbali wa unakoenda,tiwa nguvu na ulikotoka,nia ndio kila kitu


Sikiliza kilichonikuta Baharia wa nchi kavu.....



........
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]

Nimecheka sana hadi machozi yametoka...eti hiyo hela kama mumelipia twisheni ya maisha.....
 
Back
Top Bottom