Naitwa Analyse, na hii ndio safari yangu ya maisha...

Naitwa Analyse, na hii ndio safari yangu ya maisha...

.... Fursa nyingi mwanzoni huwa na changamoto, lakini fursa ya hazina ya mjerumani ina zaidi ya changamoto. Tulifika hadi Nyasa. Ulizia sana alipo huyo mzee, maana huyu jamaa sio kusema kwamba alikuwa anajua pakumpata, na yeye alisikia tu habari zake. Tulizunguka sana kwenye vijiji vya kule, mwisho wa siku tukafanikiwa kuelekezwa hadi nyumbani kwake kabisa. Tulipokelewa vizuri, tukaeleza shida yetu, wakatuelewa. Wakatwambia hizo habari mnazoziongea kuhusu mzee ni za kweli, ila zinaendelea kuenezwa kila siku japokuwa mhusika mwenyewe (yule mzee) ameshafariki yapata mwaka sasa. NIKACHOKA.

Ikabidi tuondoke, tukiwa njiani kuna mzee mwingine akatudaka. Akasema kama shida yenu ni hiyo naweza kuwasaidia. Ikabidi tumskilize. Tukafika kwake, nae akatupa maelezo ya kina. Kisha akatwambia, kama kweli mmezamilia kuzitafuta hizi hazina, basi kuna vitu muhimu inabidi muwe navyo. Cha kwanza inabidi muwe na vichaa/matahira wawili, hawa watawasaidia kuwakinga kipindi mnaingia kufukua hazina, alaf kitu cha pili inabidi muwe na Mjerumani au Muisrael kwa ajili ya kutafsiri baadhi ya mambo.

Kwangu masharti yote mawili niliyaona magumu, tena sana. Namtoa wapi mjerumani au muisrael? Pia hao vichaa, sawa hata tukiwapata, ni vipi tutaweza kuwadhibiti tukiwa nao (maana vichaa wanajulikana mambo yao),mnaweza mkaona hazina, yeye ghafla akatimua mbio, sasa kama wao ndio kinga, hapo tufate hazina au tuwakimbize? Na bora angekuwa mmoja, wapo wawili. Vipi kila mmoja akikimbia na njia yake?

Nadhani yule mzee aliona wasiwasi wangu, akasema msiwe na shaka vijana, nitawasaidia hayo mambo yote mawili, cha msingi muwe na kiasi cha pesa hata kidogo. Nikasema sawa mzee, pesa kidogo ipo. Vizuri, basi leo pumzikeni kwavile mmetembea umbali mrefu sana hadi kufika hapa, tusubirie kesho asubuhi tuanze mchakato wenu uliowaleta. Alitufanyia mpango wa msosi, tukala. Mzee pamoja na umri kwenda ila alikuwa anaishi peke yake, kibachela. Hakuwa na kitu cha thamani zaidi ya dhana za kilimo.

Kesho yake tulichelewa sana kuamka, sijui ni sababu ya uchovu au vipi. Nakumbuka tuliamka kwenye mida kama ya saa nne hivi. Pako kimya kabisa, wanaskika ndege tu. Katika safari yetu, mimi nilikuwa na begi la mgongoni, jamaa yangu nae hivyo hivyo, sema lake lilikuwa dogo kidogo. Ila cha ajabu asubuhi hiyo tulikuta mabegi yote yapo wazi, vitu vimetupwa tupwa ovyo. Kuangalia vizuri, hela hakuna na mzee hayupo. Baharia wa nchi kavu nimelizwa. Aisee nilitamani kulia. Kilichonisaidia, huwa nikiwa ugenini hela zangu siweki zote sehemu moja. Nakumbuka kuna baadhi zilikuwa kwenye begi, zingine kwenye mfuko wa suruali, na nyingine niliweka kwenye viatu (nilitoa kapeti la ndani ya kiatu, nikaweka mtonyo alafu nikalirudisha). Nilifanya hivyo kwenye viatu vyote viwili.

Yule Mzee mpaka leo naamini ujana wake aliulia Dar es salaam. Maana hela za kwenye begi aliziona, za kwenye suruali aliziona na za kwenye viatu aliziona. Sema za kwenye viatu alichukua kwenye kiatu kimoja, nahisi baada ya kukuta hela kwenye kimoja hakufikiria kama ningeweza kuweka na kwenye kingine. Jamaa yangu yeye alipigwa zoote.

Ikabidi tutoke nje tunaita, ila hamna kitu. Ikabidi tuchukue vitu vyetu tusepe. Njiani ni mashamba tu, bahati nzuri mbele tukakuta familia inalima. Tukajaribu kuwaelezea mkasa wetu. Tulivyowaelekeza nyumba tuliyokuwa pamoja na yule mzee alivyo, bahati nzuri wakamjua. Wakatwambia ile ni nyumba ambayo hutumiwa kipindi cha mavuno au wakati wa kulima, ila haikaliwi na mtu. Wakatuelekeza anapokaa. Tukamfata.

Fika mpaka kwake, tukamuulizia, wakatuelekeza yupo kilabuni, tukaelekezwa tukaenda. Pale kilabuni mzee tulimkuta yupo chakali, ashalewa pombe zao za kienyeji zile. Anatuuliza mnasemaje? Nilikuwa nimefura kwa hasira, nikamwambia Mzee tunasafari ndefu, tupe hela zetu tusepe. Kwa sauti ya kilevi mzee anasema hela ameshalipia madeni, iliyobaki ndio ile ameinunulia pombe, hana kitu labda na sisi tukae tunywe.

Nilimwangaliaa yule mzee wee, ila nkakosa cha kumfanya. Mzee ikabidi atuchane ukweli, robo ya ujana wake ameipotezea kwenye kusaka hazina ya mjerumani, na mpaka anazeeka hajawahi hata kuiona picha ya hiyo pasi ya Mjerumani. Mwishoni akatwambia "Nimepoteza hela nyingi sana vijana wangu kwenye kusaka hizo hazina, nimedhurumiwa mara nyingi sana, tena nyie mnabahati walau niliwapa hata chakula, mwenzenu hata maji nilikuwa sipewi na hela inaenda, hii hela fanyeni kama mmelipia twisheni tu ya maisha, nyie vijana bado mnanguvu mtapata zingine"

Hasira tuliyokuwa nayo sijui niielezee vipi, Mzee nae anatuangalia kilevi, hana hata chembe ya wasi wasi. Ikabidi tusepe tu, hakuna namna.

* * * * * * ***

Kufika town jamaa ananiuliza tunafanya nini kutokea hapa? Nikamwambia sina cha kufanya na wewe, we endelea tu na harakati zako (Hasira za kupoteza hela nyingi kwa wakati mmoja zilikuwa bado zipo kichwani).

Nikarudi kwenye kufanya vibarua vyangu huku natafakari kitu cha kufanya. Kuna siku likanijia lile wazo " Kama mnataka mali, mtazipata shambani". Nikaamua kujikita kwenye kilimo. Amini na kwambia "KAMA UNATAKA STRESS, BASI UTAZIPATA SHAMBANI" maana kama hujaparalaizi basi unaweza ukafa kabisa.

Maisha ni safari,kuna mnaosafiri kwa ndege,wengine kwa miguu,ila wote tunaelekea sehemu moja. Usitishwe na umbali wa unakoenda,tiwa nguvu na ulikotoka,nia ndio kila kitu

Sikiliza kilichonikuta Baharia wa nchi kavu.....

........
Umenichekesha sana ety kama unazitaka stress utazipata shambani[emoji16][emoji16][emoji16]
 
Mzee kawafanyia utapel afu kadai mmemlipa hela ya tuition [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] aisee mzee noma huyo
 
Safi sana analyse kwetu ni anyelwisye ni wale wale tu mikasa ni karibia ile ile.
Sema faza alikata moto mapema tu ila ilikua ni ile life ya mbio mbio tu.
Akitulia mtu poa sana,
ila akiamua pale home hapakaliki,na mara nyingi ilikua ni vita mimi nayeye tu.
Nimekuja kumuelewa badae sana maana maswali ya huyu ni mdingi wangu kweli?
Nishajiuliza sana.
Ila sura sasa.
Hasa hilo pua😂😂😂.
Hapo unakubali huyu dingi yangu tupambane tu.
 
Kilimo kimenigharimu hela zangu Sana three consecutive years nawaza pengine mambo yatakua Sawa lkn hola,changamoto ninyingi ktk kilimo chakitanzania,gharama zauendeshaji haziongei lugha Moja na soko,changamoto zahali yahewa,na ukosefu wa elimu juu yakudhibiti magonjwa ya mazao,nililima hekari 7,zaufuta 2018nikavuna chini yagharama nilizotumia,2019nikalima ekari kumi nkavuna chini yagharama zauendeshaji,2020nikalima ekari 30,tena na vibarua watano wakila nakunywa nyumbani kwangu kilichonikuta,ilibidi nikamuombe mama msamaha kwani nilikopa hela zake nikaendeshee kilimo,amewahi mara kadhaa kuniambia huwezi kufanikiwa ktk kilimo nikambishia ningumu,naukajaribu mtama,ekari kuminatano ,nkavuna chini yakiwango lkn,nimakuta soko liko chini mno,yaani soko liko chini Hadi nikaanza kumbembeleza wanunuzi,nilishangaa Sana,nimeapa kutombishia mzazi napia kilimo Kwa Tanzania licha yakua kinaitwa UTI wa mgongo daa! nikipengele kikubwa mno.

Sent from my M2006C3MG using JamiiForums mobile app
 
Hasa hilo pua[emoji23][emoji23][emoji23].
Hapo unakubali huyu dingi yangu tupambane tu.
Pamoja chief. Tuzidi kupambana
 
Kilimo kimenigharimu hela zangu Sana three consecutive years nawaza pengine mambo yatakua Sawa lkn hola,changamoto ninyingi ktk kilimo chakitanzania,gharama zauendeshaji haziongei lugha Moja na soko,changamoto zahali yahewa,na ukosefu wa elimu juu yakudhibiti magonjwa ya mazao,nililima hekari 7,zaufuta 2018nikavuna chini yagharama nilizotumia,2019nikalima ekari kumi nkavuna chini yagharama zauendeshaji,2020nikalima ekari 30,tena na vibarua watano wakila nakunywa nyumbani kwangu kilichonikuta,ilibidi nikamuombe mama msamaha kwani nilikopa hela zake nikaendeshee kilimo,amewahi mara kadhaa kuniambia huwezi kufanikiwa ktk kilimo nikambishia ningumu,naukajaribu mtama,ekari kuminatano ,nkavuna chini yakiwango lkn,nimakuta soko liko chini mno,yaani soko liko chini Hadi nikaanza kumbembeleza wanunuzi,nilishangaa Sana,nimeapa kutombishia mzazi napia kilimo Kwa Tanzania licha yakua kinaitwa UTI wa mgongo daa! nikipengele kikubwa mno.

Sent from my M2006C3MG using JamiiForums mobile app
Broh, usipokuwa mtu wa kujiongeza, hela zako zitaishia ardhini. Sio kila kitu ni chakila mtu, wapo watakaofanikiwa kwenye kilimo, lakini pia Kuna sisi ambao kilimo kitakataa. Usipojifunza kuadapt, ni rahisi kupoteana.
 
Dah nilikuwa naupita huu uzi jana usiku nikasema hebu leo niusome.. kumbe nilikuwa napitwa na mkasa makini..

Respect kwako Analyse. Najuta kuchelewa kuusoma huu mkasa..

Ila nimecheka sanaaaa[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Sent from my SM-J530F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom